Hapo nimekuelewa. Kwamba kuna kosa lilifanyika kwa kuwa na mandege mengi kuliko uwezo wa kuyahudumia kwa faida. Tungeanza na chache halafu tukawa tunaongeza kadiri ya faida tuipatayo.
Umuhimu wake uko wapi wakati tunapata hasara? Kwanini izo pesa tusizipeleke kwenye miradi ambayo italeta faida kwa wananchi wote,
Mkuu ivi wewe una akili kweli?
Hakutaka kabisa kuonekana anafeli kwenye jambo kwakweliYan alitengeneza machinery ya propaganda na maigizo na akafanikiwa kweli. Sijui ni uzalendo gani waliokuwa wanahubiri
Halafu ndugu yangu naona mwenyekiti wa UVCCM ndugu Kheri James anaomba radhi kama kuna mahali chama kilikosea au kiongozi anayetokana na CCM alimkosea mtu. Ana maana gani?yes yes ila sasa kosa limeshatokea hata mkianza kutukana na vijembe haisadii chochote zaidi mapendekezo yangefaa zaidi, yawezekana alikua na nia nzuri ila approach was bad
Hata mi nimeuliza swali tu, Doa moja linatisha kabisa kusababisha shati jeupe lisivalike, Tutazidi kupata majibu mbele kwa mbele subira muhimumangapi mengine amedanganya maana inaonekana we mjuaji sana, tuambie mengine
Hapa hashambuliwa marehemu yanashambuliwa mabaya aliyoyafanya ili waliopo warekebishethats a nistake ofcourse, but ni marehem tayar sasa mnapoteza mda kushambuliana na marehem
Tumedanganywa mangapi? Bungeni wabunge wa upinzani walipiga kelele kwamba ATCL haipati faida bali ni hasara tu, mbona wabunge wa CCM walikuja juu kwa kelele za TAARIFA na kueleza kwamba shirika linatengeneza faida kama Rais alivyokua akisema, hii ni kusema hawa wabunge wa CCM kuna mengi walikua wanatudanganya kwa lengo la kumkingia kifua Rais na chama chao!!?? Watanzania tuungane tuanze upya hakuna namna. Tumuunge mkono mama.we can call that a weakness ofcourse, uwazi ni muhimu sana
Hiyo ndiyo shida na wale waliotaka kuonyesha alipofail wakawa eti wanatumiwa na mabeberuHakutaka kabisa kuonekana anafeli kwenye jambo kwakweli
hakuna biashara inaanzishwa apo apo inamke profit, for an airline bussiness its even worse you have to do trial and error nyingi tafauti but you still need to pay your workers.
Ngoja tumuone mama yetuHiyo ndiyo shida na wale waliotaka kuonyesha alipofail wakawa eti wanatumiwa na mabeberu
Gawiwo linakikokotoo chake halihusiani na faida uliza ueleweshwe. Tatizo lenu you are overdoing hoja itakapojibiwa mtaaibika maana mnakubaliana na conclusive statements badala ya kutoa room of doubt. Haya endeleeni na sherehe.Usisahau hili shirika lilitoa gawaio kwa serikali ikimaanisha ilikuwa ikipata faida
ATCL kupata faida ni kama ndoto tu maana siasa ni nyingi katika uendeshaji. Kwa mfano safari za Chato kama zilikuwepo ni wazi zitakuwa zilikuwa za hasara tu. Sema ATCL inaweza kukumbatiwa kwa malengo ya kuleta faida indirectly. Kwa mfano ikileta watalii ambao labda wangepitia Nairobi nk. Lakini hiyo nayo lazima ipimwe kiutaalamu isije ikazidi kiwango.anaweza kujibu hayo maswali ni yeye mwenyewe but mm i think airlines ni muhimu sana, serikali inaweza kuikumbatia ATCL mpaka ikapata faida
Mnaanza kujichanganya mapema mnamsema vibaya mwenda zake kwa kujipendekeza kwa mkalia kiti kwa sasa kana kwamba hakuwepo wakati wa uamuzi wa kitu chochote iwe mapato na matumizi.Mambo sasa yanaanza kujianika kwenye mkeka wa uhakika. Ukweli unauzidi nguvu uongo kama mbegu inapochomoza kwenye udongo. Ukweli unaanza kutamalaki kama mashabiki kindakindaki au mwalimu na chaki. Tumedanganywa sana na kwa muda mrefu.
CAG amemwambia Mhe. Rais kuwa ATCL imekuwa ikijiendesha kwa hasara ya mabilioni ya shilingi za kitanzania kwa miaka mitano sasa. Lakini Mwendazake na wenzake wamekuwa wakituamisha kuwa ATCL imekuwa ikijiendesha kwa faida. Katika kuchagiza hilo, ATCL imekuwa ikitoa hadi gawio kwa Serikali. Tulikuwa tukidanganywa.
Serikali ya Mwendazake ilijaa propaganda na uongo mkubwa. Tumeanza kuona upande wa pili wa tulichokuwa tukiambiwa. Ukweli unaupiga kumbo uongo uliotaka kudumu kwa muongo mzima. Amini nawaambia, hilo ni tone tu kwenye bahari ya propaganda zilizokuwa zikiendelea wakati wa uongozi wa Mwendazake. Mengi yanafuata baada ya tuta.
Ndugu yangu Kichere, angekuwepo Mwendazake ungeiwasilisha Ripoti ile inayoanika ATCL na hasara zake?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Ebu niambie hospital ipi ya kata imeleta hasara kwa taifa kama ATCL?kwahio ukipata hasara ndo kwamba huo mradi hauna umuhimu? kwahio tuanze kungoa reli na zile hospital za kata ambazo huduma nyingi zinatolewa bure tuzivunje pia?
Kama gawio halihusiani na faida ni nini hicho basi ni gawio la mtaji?Gawiwo linakikokotoo chake halihusiani na faida uliza ueleweshwe. Tatizo lenu you are overdoing hoja itakapojibiwa mtaaibika maana mnakubaliana na conclusive statements badala ya kutoa room of doubt. Haya endeleeni na sherehe.