Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

Nilisema na Nasema hivi, Ulimwengu upo tu, Hauna mwanzo wala mwisho.
Ni nini kinachokuthibitishia kwamba ulimwengu upo tu hauna Mwanzo Wala mwisho?
Ukianza kuweka ulazima wa chanzo cha kitu fulani, basi hata hicho chanzo cha hicho kitu, kitahitaji chanzo.
Kwa ivo hofu yako ni kushindwa kuelezea mwanzo wa chanzo??
Kitu lazima kiwe kwa namna moja tu.
Jee Kwa mnatiki yako hii unaweza kumuelezeaje Popo?
Ila mimi ni Binadamu, Na siwezi na Haiwezekani niwe ng'ombe.
Kitu gani kinachokuaminisha kwamba kesho ikifika huwezi kuwa Ng'ombe? Fikra kwamba ukiwa binadamu utabakia binadamu daima umeitoa wapi?
 
Kwanza lazima ujue kwamba, Sayansi haina majibu ya kila kitu.

Na sayansi, Haisemi kwamba inajua kila kitu.

Sayansi yenyewe ina nadharia (theory) mbalimbali zilizo jaribu kuonesha chanzo cha ulimwengu ila na zenyewe bado zina mkanganyiko (contradiction) mkubwa sana.

Hazijaweza kuthibitishika, mfano wa theory hizo ni Bing bang theory.

Ila kwa kutumia Einstein relativity ambayo inasema kwamba 👇
" The rate at which time passes depends upon your frame of reference"

Yani ina maanisha kwamba wewe huwezi kujua usivyo vijua, kwa sababu
"frame of reference" yako ni vile unavyo vijua tu.

Huwezi kuelezea kitu ambacho kipo nje ya frame of your reference.

Yani ni sawa na kuhoji,
what is the North of the North Pole?
 
Mi naongelea mateso, utumwa, kunyanyaswa, vita, etc Kuna watu wanachinjwa na magaidi huko...a lot of things...hasa why God allows this ..bado Kuna natural disasters ma earthquakes Nini
Kwani hayo uliyoyaorodhesha ni mambo mabaya!!??

Hakuna shida kuua, kumfanya mtu mtumwa, kuwa na Vita au kunyanyasa wengine
 
Safi sa Safi hapa sasa ndio tunajifunza vitu vya msingi kuliko zile porojo tu sasa una habari kwamba Einstein mwenyewe alikuja Akakiri kwamba Anaamini katika uwepo way Mungu kutokana na hiyo uliyoeleza hapo juu yaani "lack of frame of reference" about exactly source ya Universe?
Sio huyo tu hadi kina Gallileo Galilei wote walisarenda kwamba there is God running the things in this Universe!
 
Kiislamu mwenye kuchoma ni Allah, mwanadamu ni haramu kuadhibu au kuwa kitu kwa kukichoma.

Uwe unasoma ninacho kiandika, hili nililielezea huko nyuma.
Nimeuliza kama utaweza kumtafsiri mtu anae mchoma mtoto wake kwa kosa lolote kama ana upendo au la, wewe unanijibu mwenye kuchoma ni Allah!

Wala Sijauliza kama ni haramu kuchoma mtu. Nimeuliza tafsiri ya watu wenzako tu ju ya upendo.
Wala sijauliza kuhusu Allah.

Jibu swali langu tafadhali.
Mzazi mwenye kumchoma mtoto wake aliyekosea wewe binafsi utamuona mzazi huyo kama mwenye upendo sana na mtoto wake??
 
Ni nini kinachokuthibitishia kwamba ulimwengu upo tu hauna Mwanzo Wala mwisho?
Kinacho nithibitishia kwamba ulimwengu upo tu, Hauna mwanzo wala mwisho ni kwamba 👇

Hakujawahi kuthibitishika na Hakuna chanzo chochote kile, kilicho tambuliwa na kuthibitishwa kwamba ndicho chanzo cha ulimwengu.

Kama wewe unaweza kuki thibitisha chanzo hicho, kilete hapa tukione.

Kwa ivo hofu yako ni kushindwa kuelezea mwanzo wa chanzo??
Mwanzo na mwisho HAVIWEZI
ku elezeka wala ku elezewa kwa namna yoyote ile, kwa vile HAVIPO

Kama unaweza vielezee na uvithibitishe uwepo wake.
Jee Kwa mnatiki yako hii unaweza kumuelezeaje Popo?
Popo ni mnyama Popo, hawezi kuwa nje ya yeye kuwa mnyama Popo.

Kuwa na sifa moja tu ya kuruka hakumfanyi yeye kuitwa ndege.
Kitu gani kinachokuaminisha kwamba kesho ikifika huwezi kuwa Ng'ombe?
Kesho hiyo mpaka ifike na nibadilike niwe ng'ombe ndio utakuwa uthibitisho wa kwamba inawezekana kweli, binadamu kubadilika na kuwa ng'ombe.

Ila kwa sasa Haiwezekani kwa vile hakuna uthibitisho huo.
Fikra kwamba ukiwa binadamu utabakia binadamu daima umeitoa wapi?
Nimeitoa kwenye mazingira yaonekanayo, kwamba Hakuna kitu kimoja Kinacho weza kuwepo kwa namna mbili na hakuja wahi kuwepo hivyo katika mazingira ya dunia hii.
 
Einstein kukiri uwepo wa Mungu, Bado haku thibitishi uwepo wa huyo Mungu.

Ni hofu zake tu,

Ni kwamba 👇

Hatuwezi kujua Tusicho kijua.

Kama Mungu huyo yupo, Eleza yupo kwa namna gani?

Na ume wezaje kujua yupo?

Uchunguzi gani ulifanyika kujua Mungu yupo?
 
Hofu??? Kumbe Unatambua kwamba kuna Hofu??? Umeitambuaje wakati Hujaithibitisha??? (Self Contradictory)????
 
Hofu??? Kumbe Unatambua kwamba kuna Hofu??? Umeitambuaje wakati Hujaithibitisha??? (Self Contradictory)????
Ulijifunza Nomino dhahania katika kiswahili?

Nomino dhahania ni maneno yanayo onyesha vitu visivyokuwa katika uhalisia wa kuonekana. Ila vipo katika hali ya kufikirika tu.
(dhana za kufikirika)

Maneno haya hutumika kuonyesha Hali za kibinadamu zisizo katika uhalisia wa kuonekana, kushikika au kusikika.

Na mifano ya maneno hayo, Nomino dhahania hizo ni kama vile:
Woga, wasiwasi, hofu, Akili, tamaa, kiburi, chuki, aibu, njaa, kiu n.k

Vyote hivi HAVIPO katika uhalisia ila ni dhana za kufikirika tu.

Hivyo "Hofu" haipo kwenye uhalisia ila ni dhana ya kufikirika tu.

Imagination just an illusion.
 
O k kwa hiyo wewe Una Akili au huna?
 
Hakujawahi kuthibitishika na Hakuna chanzo chochote kile, kilicho tambuliwa na kuthibitishwa kwamba ndicho chanzo cha ulimwengu
Kimantiki Kwa fikra zako unataka kusema ulimwengu una umri Gani?

Wewe unaweza kusema tu ya umri wako.jee kabla yako hakukuwa na watu ambao wanaweza kuchukuliwa kama rejea Kwa mambo yaliyotokea katika zama zao?



Jee idadi ya watu ulimwenguni miaka 3,000 iliyopita ilikuwa sawa na Sasa na nini kinafanya watu waongezeke na dunia kuonekana kuchakaa Kwa kadri miaka inavyopita?
 
Ama kwa mtoto anae kufa katika tukio hilo, yeye anakuwa muda wake wa kufa umefika, na yeye atakuja kupewa mtihani siku ya Kiama, akifaulu analipwa pepo na alifeli anaingizwa motoni.
mtoto mdogo wa kiislam alikufa Muhammad alienda kwenye msiba , Aisha alamwambia Muhammad huyu mtoto mchanga ataenda mbinguni maana ni muislamu na hajawahi kufanya dhambi , Muhammad akamwambia inaweza kuwa tofauti na akaenda motoni kwani Allah anapanga wa motoni na WA peponi kabla hawajazaliwa
  • A'isha, said Allah's Messenger, there is happiness for this child who is a bird from the birds of Paradise for it committed no sin nor has he reached the age when one can commit sin. He said: 'A'isha, it may be otherwise, because Allah created for Paradise those who are fit for it while they were yet in their father's loins and created for Hell those who are to go to Hell. He created them for Hell while they were yet in their father's loins. Sahih Muslim 2662c
 
Angalii hii video jamaa alitaka kumpiga bastola huyo jamaa aliyevaa nguo nyekundu ila ilikuwa haikupangwa jamaa kupigwa bastola.
Ukichukua manati na kumlenga ndege [emoji211] kisha uka mkosa kwa mara ya kwanza, ukajaribu tena mara ya pili uka mpata,

Hapa utasemaje?

Ni kwamba, Mara ya kwanza ulikuwa Huja lenga kwa shabaha( Target) iliyo sahihi, Target yako haikuwa na accuracy.

Ila unge lenga kwa shabaha iliyo sahihi unge muua ndege [emoji211] huyo kwa mara hiyo ya kwanza tu.

Huyo jamaa aliye piga bastola, Ni kwamba Hakuwa na Shabaha (Target) yenye accuracy ndio maana alimkosa huyo jamaa aliye vaa nguo nyekundu.

Hivyo point yako hii ya kwamba "Jambo fulani hupangwa" Haina mantiki yeyote.

Kama unabisha, Jamaa huyo angepata nafasi ya pili (Second chance) ya kufyatua bastola..Huyo jamaa wa nguo nyekundu angefumuliwa ubongo na kufa papo hapo.
 
1 Wakorintho 1:25
[25]Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.
Because the foolishness of God is wiser than men; and the weakness of God is stronger than men.
 
😂😂Unaweza kumlenga mpqkq akakimbiq na usimpate... Angalia bastola na nafasi wapo karibu sio labda kumpiga mpaka akafa ni kiasi cha kumpata haijampata yaani hata kutoka risasa.

Nina hakika hiyo risasi ingetoka asingekuwa mzima tena kama alivyopigwa AKA kule south Africa.
 
hakika mtoto huyo Akifa yeye anakuwa wa kwanza kuenda katika Pepo
Hiyo hakika Muhammad kaipinga

mtoto mdogo wa kiislam alikufa Muhammad alienda kwenye msiba , Aisha alamwambia Muhammad huyu mtoto mchanga ataenda mbinguni maana ni muislamu na hajawahi kufanya dhambi , Muhammad akamwambia inaweza kuwa tofauti na akaenda motoni kwani Allah anapanga wa motoni na WA peponi kabla hawajazaliwa
  • A'isha, said Allah's Messenger, there is happiness for this child who is a bird from the birds of Paradise for it committed no sin nor has he reached the age when one can commit sin. He said: 'A'isha, it may be otherwise, because Allah created for Paradise those who are fit for it while they were yet in their father's loins and created for Hell those who are to go to Hell. He created them for Hell while they were yet in their father's loins. Sahih Muslim 2662c
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…