Swali la kwanza liko wazi sababu mzazi amekusudia kumuua mwanae kwa adhabu ya kifo kwa njia ya kumuua, tunasema mzazi alikuwa na nia njema ya kuadhibu ila lengo (kama amekusudia kumuua) lake sio jema, au kama hakukusudia kumuua ila alitumia njia ya kumchoma moto kwa ajili ya kumuadhibu ikatokea mtoto akafa, basi hapo anakuwa na kosa moja la kutumia njia ambayo si sahihi kumuadhibu ila upendo uko pale pale, ndio maana akaamua kumuadhibu.
Hayo mawazo umeyatoa wapi.
1. "mzazi alikua na nia njema ya kuadhibu"
2. "Mzazi hakukusudia kumuua"
Nauliza kuhusu mzazi aliyekusudia
kuua.
Si kuua tu bali kuua kwa moto.
Kuua (kwa moto) ndiyo adhabu aliyokusudia kuitoa. Nia yake ni kumuua. Lengo lake ni kumuua. Moto ni njia aliyotumia kumuua.
Kumchoma moto mpaka afe kwake ndiyo adhabu yenyewe.
Mtoto angeungua pasipo kufa, basi mzazi angeona hajatimiza kusudio lake.
Sijauliza kuhusu Mzazi aliyeamua kumchoma mtoto wake moto ikatokea akafa.
Nauliza mzazi aliyeamua kumuua mtoto wake kwa kumchoma moto.
Elewa neno
kuua.
Pia, swali limeulizwa kama
kitendo cha mzazi kumuua mtoto wake kwa moto ni cha upendo.
Unaposema "upendo uko palepale" unakusudia upendo wa hicho kitendo?
Kwamba hicho kitendo(cha kuua kwa moto) ni cha upendo?
Sijauliza kama mzazi ana upendo kwa mtoto. Nimeuliza kama
kitendo cha kumuua kwa moto ni cha upendo.
Elewa neno
kitendo.
Kitendo cha mzazi kumuua mtoto wake kwa kumchoma moto kama adhabu kitakua cha upendo?
Swali la pili
Kitakuwa cha huruma.
Unasema kitendo cha mzazi kumuua mtoto wake kwa kumchoma moto kama adhabu kitakua cha
huruma.
Huruma ni nini?
Kwa uelewa wangu huruma ni hali ya mtu kumtakia mwenzake wema katika shida. Yaani, ni uwezo wa kushiriki hisia za wengine, hasa taabu, huzuni au maumivu.
Kama una maana nyingine ya huruma nisaidie.
Nikisema kitendo cha mzazi kumuua mtoto wake kwa kumchoma moto kama adhabu kitakua kitendo cha kushiriki hisia za mtoto wake kama taabu na maumivu yaani kumpa maumivu mtoto akiungua na moto mpaka afe ni kumtakia mtoto wake wema katika shida na maumivu nitakua sawa?
Wewe unaweza kumuua mtoto wako kwa kumchoma moto mpake afe pale anapokosea kwa kumhurumia??
Swali la tatu
Huenda kikawa na furaha au kikawahuzunisha, inategemea.
Inategemea nini?