Kuanza na "je" maana yake swali linaulizwa
Yani wewe kigezo chako cha kupima kujiamini au kutokujiamini kwa mtu ni matumizi ya "je" kwenye sentensi?
Swali kubwa lilikuwa kwamba dunia na vitu vyake lazima viwe na muumbaji haviwezi kujileta.
Kusema dunia itakuwepo, ilikuwepo na itaendelea kuwepo na vitu vyake ndani, haina mwanzo wala mwisho na haina mtengenezaji kwako ni jibu jepesi ambalo unadhani hakuna atakaeniamini
lakini ukiulizwa mungu alitokea wapi unakubali kwamba mungu hana mtengenezaji, alikuwepo, ataendelea kuwepo, hana mwanzo wala mwisho na kwako hili unaona sio jibu jepesi.
Kama unakubali mungu anaweza kuwepo bila mtengenezaji kwanini nikikwambia hivyo hivyo kwa dunia unaona ni jibu jepesi ambalo haliwezi kuaminika?
Sent from my M10_Max using
JamiiForums mobile app