Uongo na Ukweli Kuhusu TANESCO Kuzuiwa Kufanya Maintenance

Chige na ripoti yake..mama na wafugaji wake...Marope na maintenance zake...Katelephone na umeme wake wa kumwagaa....aargh,hii miluzi mbona mingi?!..nchi ngumu hii jamani!😩😤
Hakuna cha miluzi mingi wala nini!

Miluzi inaonekana mingi kwa sababu tunachukua kila kinachosemwa na yeyote ili mradi ana madaraka mahali, badala ya kutafuta chanzo kikuu cha taarifa husika!

Kwavile vyanzo vikuu taarifa zake zinakuwa in a written form, basi taarifa hiyo ikisomwa na hata watu 10M, bado ujumbe utabaki ule ule!!
 
Jamaa hawataki kuelewa hata ukiwapa ushahidi.Kazi ipo
 
Hizo spea zinachukua mda gani kufika nchini?
Je tanesco hawana spea kwa jili ya dharula?
Spea za maintanance zinasubili kuagizwa kwenye shirika la umma linalotegemewa na nchi nzima wakati wakurekebisha?

Kwanini waziri wakati anaingia madalakani hakuona umuhimu wa kuongeza uzalishaji kwa hiyo kinyerezi 3 mpaka umeme ulete shida ndo aje kusema wanahakikisha watajenga lakini akaona aingie mkataba wa kuwalipa wahindi ambao watakuja kuweka mifumo ya uendeshaji kwa kitu ambacho sio stable?
 
Uzalishaji angeongeza kwa kutumia nini
 
HAHAHAHA mkuu hongera kwa kumpambania Makamba watu wanahitaji umeme.... umeme ukiwa na shida watu watajua tuu na watasema wala tusijifiche kwenye visingizio hahahah yani hapa watu wanaona wazi kuna shida...... pamoja na hayo yote miaka hiyo yote hakukuwa na shida kubwa kama hii.... na kila mtu anajua na wala watu hawahitaji matakwimu hahaha
 
Baada ya maelezo yako marefu, je wanatuhakikishia kuwa kwa vile sasa wanaweza kufanya matengenezo inavyotakiwa Tanzania haitakuwa na tatizo la upungufu wa nishati ya umeme? Je, matengenezo ya muda na kiasi gani yataondoa tatizo la mgao?

Kwanza tunashukuru umeelewa kuwa kilichokuwa kinaendelea wakati wa Magufuli sio utendaji bora,bali ni kusaka sifa za kijinga. Na sifa hizo za kijinga hazikuwa huko kwenye umeme tu, bali ni kwenye mambo mengi tena ya msingi.
 

Kiutaalamu lazima mtambo ufanyiwe maintanance baada ya masaa kadhaa ya kutembea bila hivyo kitu kinabuma…

Anyway daata zako zenyewe hapo zinaonyesha maintanance ilikuwa inafanyika…halafu daah ebu wacha nisiseme…

Wananchi wa Tanzania tunakipato cha chini tunahitaji umeme wa bei nafuu…ili tusonge…kwanini usishauri kutumia upepo na solar hio gesi ikasubiri kwanza maana bado hatuko tayari…
 
Huyu mwanzisha mada sijui alifanywa nini na JPM!

Kwa ufupi, hatukuwa na tatizo la umeme la kiwango hiki na hili wewe mtu mmoja huwezi kutufundisha! Wananchi wanajua!

Kama issue ni mitambo kutofanyiwa maintenance toeni schedule tuone toka mmeanza kufanya maintenance tuone improvements otherwise ni porojo.

Upungufu wa maji umesababishwa na nini? Mbona for 5 good yrs ilishafutika? Au JPM alifichaje yaani?
 
Chief usiwasikilize hawa,hizi ni propaganda tu za kuwasha mitambo ya emergency ya akina Symbion na IPTL ili upigaji wa raslimali za taifa uendelee,time will tell

Uliishi kwenye propaganda za kijinga, kiasi kwamba ukikutana na ukweli ndio unatamani iwe propaganda. Muda wote wa utawala wa Magufuli tulisema ni mtu mpika data na msaka sifa za kijinga. Kwa bahati mbaya hata hawa wanaojifanya kurekebisha mambo sasa ni waongo wenzake, tofauti ni kuwa yeye alikuwa muongo kuliko wao.
 

Mmmh, upungufu wa maji umesababishwa na nini?! Ukweli una tabia ya kuumiza. Magufuli alikuwa ni tapeli mwenye roho mbaya, hawa wa sasa ni matapeli wenye tabia za ujanja ujanja.
 
Muhimu ni kuwa wakati wa Magufuli na Kalemani hakukuwa na mgao wa umeme!
Hakuna na sijaona sababu ya wewe kuukataa ukweli ila kilichopo na ninachokiona kwako ni maradhi which entered into the minds of the majority of people has also entered your mind.
 
Wekeni data zote kuhalalisha upigaji,lakini Magufuli kawa prove wrong within a short time,najua mna nguvu kubwa ya propaganda,mtafanikiwa kwa muda tu ,si daima
Wewe unadhani kutetea huko ni uzalendo? Au utakwenda mbinguni?

Haujajibu bali umepiga kelele. Kama data zake ni za kupika weka zako za ukweli.
 
Nimekusoma mwanzo mwisho huku nikizoom data ulizoweka kusindikiza facts zako.

Lakini inaonesha hii post inaisagia kunguni awamu iliyokwenda zake.

Mimi naona ni vyema sasa kukubaliana na option ya Waziri Makamba kwamba TANESCO iingie kwenye phase ya kubinafsishwa au kugawanywa.

Haya madudu yanayofanyika na yanayopangwa dawa yake ni moja tu, nayo ni maamuzi magumu ya kuiweka TANESCO kwenye ubia na wawekezaji. Au ugawanywe isiwe stop centre ya umeme nchini. Au zialikwe kampuni binafsi kuongeza ushindani.

Hekaya hazitaisha kwa fikra mgando
 
Kweli mkuu!
Miaka mitano ilituumiza sana wapiga dili. We need to compensate.
Na hilo Bwawa lao watasubiri saaaaana!
 
Ndugu, jikite kwenye data hapo juu, achana na politics!
Ukiamua kubeba yote mawili, shauri yako.
 
Baada ya maelezo yako marefu, je wanatuhakikishia kuwa kwa vile sasa wanaweza kufanya matengenezo inavyotakiwa Tanzania haitakuwa na tatizo la upungufu wa nishati ya umeme? Je, matengenezo ya muda na kiasi gani yataondoa tatizo la mgao?

Naona haujamuelewa kwa makusudi. Au urefu wa maelezo ndio yamekufanya usiyasome kwa umakini? Alichokisema huyu ndugu ni kuwa hata hiyo Ubungo II ikitengamaa upungufu utaendelewa kuweko. Kinachosababisha upungufu ni upungufu wa uzalishaji katika vinu vyetu vinavyotegemea maji. Vinu vya maji vinatoa 574 MW wakati cha Ubungo II ni 105 MW. Kama vinu hivyo vitakuwa vinazalisha katika 50% capacity, vitakuwa vizalisha 287 MW tu na kuacha pengo la 287 MW . Katika pengo hilo, Ubungo II itaziba 105 MW tu na kuacha pungufu ya 182 MW.

Mimi naamini kuwa lawama zote mnakiwa mbebe nyie ambao mlikuwa mnausifia mradi wa Stiegler pamoja na kuonywa sana na mabeberu kuwa ule mradi hauna mantik. Hizo pesa zilizotupwa kule zingetumika kujenga mitambo ya gesi asilia tatizo hili lisingekuweko. Lakini kwa vile bado mmeushupalia ule mradi ( ambao ni tembo mweupe) huu mgao hautaisha hivi karibuni. Na sijui mwekezaji gani atawekeza katika nchi ambayo nishati ni kitu cha kubahatisha.
Mliwakosea sana watanzania wenzenu mlipoacha kuwa critical thinkers na kugeuka waimba mapambio. Haya ndio mazao yake.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…