Ng'wanamangilingili
JF-Expert Member
- Aug 22, 2015
- 5,778
- 4,859
Kwa hiyo JPM angekuwepo leo tungekuwa katika giza hili la mgao lingemuangukia jumba lake bovu? ceteris peribus?Kama ambavyo wadau mbalimbali wamekuwa wakisema mara kadhaa, Mkakati wa Taifa kuhusu uzalishaji wa umeme ulikuwa:-
View attachment 2015968
Yaani, malengo hadi kufikia June 2020, tulitakiwa tuwe tumezalisha 4,915 MW. Hiyo ni Performance Audit Report iliyotolewa na CAG March 2019.
Hata hivyo, ripoti ya wizara inasema hadi kufikia mwishoni mwa 2019, tulikuwa tunazalisha ONLY 1,565.72 MW... ni takribani 33% TU ya malengo!
View attachment 2015977
Kutofikiwa huko kwa malengo kulitokana na kuhamishia nguvu ZOTE kwenye Bwawa la Nyerere, na hata zile Kinyerezi III na Kinyerezi IV, zikatekelezwa!!!
Of course, labda waliamini kwamba 1,602.32 zingetosha kutufikisha hadi kuanza kutumia Bwawa la Nyerere!! Sasa sijui walizingatia kila siku kuna wateja wapya wa umeme, na kwamba kuna kuharibika kwa mitambo... only God knows!!!
Tuje kwenye Ubungo II ambayo tunaambiwa ni mbovu, huku wengine wakihoji ikiwa ubovu umeanza baada ya JPM kufariki!!! Au ni janja janja tu ya kutaka kuhujumu Mradi wa Bwawa la Nyerere!!!
Je, maintance ilikuwa inafanyika?! Jibu lipo kwenye ripoti kwamba:-
View attachment 2015999
Utaona hapo, Mashine #1 na #2 zilipitisha zaidi ya saa 10,000 tangu siku zilipotakiwa kufanyiwa maintanance!! Yaani Machine #1 iliendelea kuburuzwa kwa mwaka 1 na miezi tangu ilipotakiwa kufanyiwa ukarabati, huku Mashine #2 ikiburuzwa kwa zaidi ya miezi 18 bila kufanyiwa maintanance tangi siku ilipotakiwa kufanyika!!
Je, ikiwa hiyo ni ripoti iliyoandikwa kutoka kwenye takwimu za 2018, je maintance ilifanyika? Na kama ilifanyika, ilifanyika lini?
TANESCO wenyewe, hawa hapa chini:-
View attachment 2016022
Kumbe, hata baada ya miaka 3 baadae, bado Ubungo II ilikuwa haisomeki!!!
Sasa ikiwa tatizo lililopo miaka na miaka, ni mjinga tu ndie anaweza kuamini kwamba hivi sasa Ubungo II ipo operational, lakini sie wapiga deal za kuuza majenereta tunafahamu mambo bado si shwari!!!
Ina maana shida ni kukosekana kwa vifaa peke yake ndo maana haya mambo ya maintanance yanachelewa namna hii?!
Again, CAG's Performance Audit Report iliyotolewa March 2019 inasema:-
Kumbe, jamaa ilikuwa wakitaka kufanya maintanance, wanapigwa STOP, na matoke yake mitambo ikawa inaburuzwa tu hivyo hivyo!!!
View attachment 2016037
Wadau walipozungumzia hilo suala, wakaitwa majina yote ya ovyo ili mradi tu....!!
Ndipo tunarudi pale pale, mbona hilo tatizo la upungufu wa umeme halikuwepo wakati wa JPM!!!
Swali ambalo nimekuwa nikiwauliza wanaotoa hiyo hoja ni kwamba nyie wenzetu mlikuwa mnaishi Tanzania ipi ambayo haikuwa na matatizo ya umeme!!
Anyway, inawezekana wenzetu ni watoto wa kishua mnaoishi kwenye viunga vya Ikulu... lakini sie tulio huku Ushenzini, hususani kwenye miji na vitongoji vikongwe vyenye uchakavu wa miundombinu, kwetu tatizo liliendelea kuwepo muda wote!!
But on top of that, ripoti hapo inaonesha, TANESCO walikuwa wanapigwa STOP kufanya maintenance pale Ubungo II kwa sababu hatukuwa na hifadhi ya kutosha ya umeme kwenye Grid ya Taifa.
Hofu ikawa kwamba, kutokana na kutokuwa na hifadhi ya kutosha, kama mitambo ingezimwa kwa ajili ya maintenance, basi huenda tungelazimika kuingia kwenye mgao!!
Sasa kama tulikuwa tunaogopa kuzima Ubungo II ambayo umeme unaotoka pale is ONLY 105MW, nini kinaweza kutokea kukiwa na upungufu wa maji ambapo, total power generated from hydro, ni 574MW?!
View attachment 2016047
Kama unakataa nchi haipo kwenye ukame, basi tatizo hili la sasa ni la kutegenezwa na mafisadi na wapinzani wa Bwawa la Nyerere, huku sie vibaraka wao tukikesha kuwapanga watu!
Akili za kuambiwa, changanya na zako!
Lakini itoshe tu kusema kwamba, ushabikiwa kijinga unaliangamiza taifa!!!
Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app