Mimi sijui niko tofauti, mtu hata awe na nini aseme nini huwa hainisumbui kabisa. Ila nimeona kuna baadhi ya watu humu, inawasumbua na mbaya zaidi ni Fake ID.
Mtu akianza kusema gari, nyumba, biashara, kusafiri nje si ni vitu vya kawaida? Ila mtu akigusia kati ya hivyo na vingine, ataandamwa, tumeshajua una gari, una nyumba!!!
Tutafute pesa, tuache makasiriko, mtu hata kama anadanganya, ni anajidanganya mwenyewe, mwisho wa siku anabaki kwenye ulimwengu wa kuishi maisha mazuri kimtandaoni, kiuhalisia yuko vilevile.
Tuache watu wajifariji na kufurahia anachofanya, ili mradi hakugusi wewe moja kwa moja. Wivu ni ugonjwa tafuta dawa kama ukiona unaumia mafanikio ya mwingine.