Masikini
TUJITEGEMEE, wengne miaka yote tumekuwa tukisema adui namba wani wa taifa hili ni CCM lakini kama kenge hamsikii hadi iwatoke masikioni. Ndugu yangu hebu fikiria haya...
Dhalimu mwendakuzimu jiwe alikuwa serikalini kwa miaka karibu ishirini, lakini akijinadi akajifanya hajui tulifikaje tulipo, hajui ilikuwaje nchi ikapinda hadi ikabidi ashushwe kuinyosha!
Pamoja na mapungufu hayo yote bado akasukumiziwa uongozi wa juu kabisa na Chama cha Majizi, chama kilichozeeka na kuchoka, chama chenye shahada ya kuwahadaa wananchi...
Pamoja na sifa zote hizo, chama hicho kikawa ndicho serikali, ndicho mahakama na ndicho Bunge. Genge hilo likataifisha vyombo vya dola kuanzia polisi hadi usalama wa taifa na kuvifanya vitengo vyake.
Magufuli kwa kuijua vilivyo CCM akawa anapiga push-up majukwaani akiwalaghai wananchi kuwa yuko fit huku mashine kifuani ikifanya kazi ya ziada kustahimili mihangaiko na sarakasi zake.
Asante corona kwa kumtembelea huyo dhalimu la sivyo hadi leo tungekuwa bado tuko mikononi mwake. Kuna siku nasi tutadumisha kumbukumbu ya Watanzania waliopotea mikononi kwake.
Bahati mbaya masikini haokoti, akiokota si ajabu akaambiwa kaiba. Tulidhani tumeokota kumbe! Ona sasa tunaambiwa tumekwiba, masikini Watanzania wenzangu, tulikosa nini? Ogopa CCM kama ukoma!