Uongo wa vifurushi vya Intaneti vya Airtel Tanzania

 
Kutokana na matumizi makubwa ya fedha kwenye manunuzi ya vifurushi vya Internet. Tarehe 01/08/2022, nilijiunga na kifurushi cha Tsh.1500 (Mb850) na niliamua kuanza kufuatilia...
Mkuu jaribu kufatilia Simu yako vizuri
 
Airtel bhana Wana Ile sms Yao ya Kila siku asubuhi. "umetumia 100% ya bando lako la internet". hata Kama ujaweka bando mwezi mzima
 
Natumia 0733 hilo haijawahi kutokea kwangu. Ninachofahamu mtandao wao hauna masafa marefu sana kivile WABORESHE.
Basi itakua umejiunga mwezi huu, mwezi wa saba tuu hapo mtandao ulipotea siku tatu, hata kwenye mitandao yao ya kijamii TTCL waliposti kuwa kuna changamoto.
 
Nape uupo tuu anacheza golf bila hofu maana bahasha toka kampuni za simu inaburudisha moyo.
Nimegundua kuwa watoto wa vigogo wa CCM kama Nape, Makamba na Ridhiwani wanafanya kazi bila hofu na kwa mazoea tofauti na vijana kama Hussein Bashe
Nape kule Twitter ukigusia Bado anakwambia leta ushahidi kama unaibiwa
 
Basi itakua umejiunga mwezi huu, mwezi wa saba tuu hapo mtandao ulipotea siku tatu, hata kwenye mitandao yao ya kijamii TTCL waliposti kuwa kuna changamoto.
Nina miezi 8 na ttcl, may be it happened!
 
Airtel wanasikitisha sana japo ndio mtandao wangu pendwa lakini na mpango wa kusajili laini nyingine huwenda wakawa hata na huruma kidogo wakati wananiibia kuliko hawa airtel.
 
Voda hata mimi siwapingi hakuna kitu kizuri kama kutodanganya ndio maana wanakula hela zangu nimejinga bando la wiki Mb 850 nakaribia natimiza siku ya tatu leo.

Nimepima 1.8 za Vida zinadumu kwa muda mwingi kuliko 2.2Gb za Halotel
Voda kwa mbali wana unafuu, nilikuwa natumia kwenye modem nikiset ile speed ndogo hata kama nikiunga cha 500 kwa matumizi yangu madogo madogo ilikuwa inakaa japo nilikuwa natumia kwenye pc lakini ilikuwa inaridhisha. Bahat mbaya nimeipoteza ile laini leo naenda kusajili special namba kabisa niiweke kwenye simu kubwa hii airtel acha ikae kwa kiswaswadu tu
 
Majuzi nimeunga kile cha buku ambacho unapata 400MB, siingii Instagram sikuhizi mimi ni whatsapp na JF tu hata whatsapp yenyewe status siangalii sana zaidi ya picha tu za watu wachache, kama ni video mara nyingi huwa nafanya ku skip tu, sina hata downloads, siingii youtube labda kugugo tu vitu hapa na pale lakini cha ajabu kabla hata ya saa moja usiku napokea sms nshatumia 75% ya data! Hapa saiv nimebaki na madakika kibao hata sijui niyapeleke wapi wayachukue tu na hayo
 
Duh! jamaa wamezidi uhuni ,mimi sasa hivi mfanya kama wewe Jf,gugo na wasap tu hata status kucheki mara chache na Mb800 kwa buku jero Voda lazima kufika siku 3 mara nyingine 4 ingekua Airtel 1 tu
 
Duh! jamaa wamezidi uhuni ,mimi sasa hivi mfanya kama wewe Jf,gugo na wasap tu hata status kucheki mara chache na Mb800 kwa buku jero Voda lazima kufika siku 3 mara nyingine 4 ingekua Airtel 1 tu
Kuna siku nilijiunga kifurushi cha week mara mbili ndani ya siku moja mpaka roho iliniuma aisee. Kifurushi cha week bongo hakina maana kabisa!
 
Exactly uko sahihi airtel ni wahuni, usiku wa kuamkia leo saa sita usiku nilizima simu ikiwa na mb 650 asubuhi nawasha simu nakuta mb 617 ,baada ya kutumia net asubuhi niliweka simu chaji ikiwa na mb 440 lakini baada ya dakika 45 natumiwa sms kwamba kifurushi kimeisha
 
Halote ndo balaaa. Una unga Mb azipiti dk 15 unatumiwa sms ya ume maliza 75% ya kifurushi chako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…