Uongozi mpya CCM waanza rasmi kufanya kazi na wakina Makonda; wadai kundi lake litawasaidia kampeni 2025

Uongozi mpya CCM waanza rasmi kufanya kazi na wakina Makonda; wadai kundi lake litawasaidia kampeni 2025

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Uwajibilaji, uzalendo na uadilifu ni vigezo muhimu kwenye Taifa huru linalotaka kuendelea. Ni nguzo muhimu Kwa chama Cha siasa kinachojali maslahi ya umma na njia pekee yakumfanya mwanadamu amheshimu Mungu na kuamini mamlaka inatoka kwake na siyo Kwa wanadamu.

Chama Cha mapinduzi kimekosa uadilifu Kwa sababu hakuna nafasi unayopewa Kwa uadilifu Bali nafasi unapewa kwa kufanikisha mikakati iliyounganishwa na matakwa ya Watu wachache na familia zao.

Uzalendo eondoka Kwa sababu thamani kubwa ya Uongozi ni fedha, Watu wanatafuta kuiba na kulimbikiza fedha kama ulinzi wa kisiasa kwao na familia zao

Uadilifu unaanza na kusema kweli ukifuatiwa na kusimamia haki. Wana CCM wanavyosema Leo sivyo watavyosema kesho. Fikra za Mwenyekiti ziwe mbovu au nzuri lazima zifauatwe Hadi atakapostaafu ndipo tuseme hapana alikosea na tuliona anakosea ila mkubwa afundishwi.

Kukosekana Kwa sifa hizo hapo juu kumepelekea Kila MTU kuwa na mapungufu na hivyo ukininyooshea kidole nakunyooshea kidole, ukinisema nawatuma kulusema na ukinifix nakufix. This is what is going on kwenye mfumo: na hapa ndipo makundi maovu yanaposamehewa na Watu wachache nakuruhusiwa kuendelea na uovu hata kama wananchi na wanachAma watakataa.

Hivyo tujiandae walewale watesi wetu kesho watakaa na mfalme meza kuu.
 
Makonda akirudi sawa, asiporudi pia ni sawa, jamii inapaswa kujua na wengi mnasema "Mungu kafanya yake" so kila jambo huwa linakuja kwa nafasi yake.

Wengi tuna roho mbaya, uchoyo na nia ovu kwa wengine ili hali mwingine akifanya mnaonekana nyie wasafi, hii inatokana na ile roho ya kwa nini.

Hatuwezi kufikia viwango vya juu vya kufahamu nani anafaa kutuongoza wakati sisi wenyewe tuna makando kando yanatuzunguka.

👉🏾Naendelea kujifunza tabia ya binadamu.
 
Back
Top Bottom