muafi
JF-Expert Member
- Oct 6, 2015
- 2,557
- 6,128
Nimependezwa jana na hotuba ya Jana ya Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya 2022/2023.
Bajeti inekaa vizuri sana. Nampongeza Mh Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha.
Hakika serikali imeonesha nia ya kubana matumizi kwa akili kubwa sana. Jana ndio nilijua hivi kumbe Kuna watu wanalipwa mishahara ambayo hawaifanyii kazi?
Yaani ndani ya halmashauri moja wanaweza kua watu 14 wanalipwa mshahara wa mkurugenzi ilihari sio wakurugenzi eti kisa huko nyuma waliishakua wakurugenzi kisha wakayenguliwa?
Kwahiyo ndani ya wizara moja unaweza kukuta watu zaidi ya 20 wanalipwa mshahara wa katibu mkuu ilihari wako na kazi zingine? Unakuta mhasibu analipwa mshahara wa mkurugenzi?
Nashauri serikali itengue hilo mara moja itasaidia pia mtu kulinda cheo chake kwa kuongeza ufanisi kazini.
Vilevile naafiki swala la kuwakopesha magari watumishi wenye hadhi ya kuwa na magari katika majukumu yao, hii itasaidia kabisa utunzaji wa mali hizo naomba pia hata wale maafisa kilimo watendaji nk hata wao wasipewe pikipiki za serikali isipokua wakopeshwe!
Nawaomba wabunge wote kwa pamoja muipitishe hii bajeti kwa kishindo.
Hongera Rais Samia hongera serikali ya Tanzania