Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi publications za PhD huwa zinahifadhiwa chuoni wa zinakuwa published kwenye international journals? zinahifadhi liblary kama za undergraduatesSiku mbili baada ya shahada za uzamivu (PhD) za viongozi wa kisiasa hasa Mawaziri na Wabunge kuibua mjadala, uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) umezitetea na kueleza namna ya kuondoa shaka juu yake.
Akizungumza na Mwananchi, Makamu Mkuu wa UDOM, Profesa Faustine Bee amesema wenye shaka wanaweza kujiridhisha kwa kutembelea maktaba ya chuo hicho kuona machapisho ya wahitimu wenyewe.
Alisema suala la viongozi wakubwa kuhitimu shahada za uzamivu ni la muhusika mwenyewe anavyojipanga, kupangilia muda wake na majukumu aliyonayo.
“Ni suala la nidhamu ya muda, mtu kupangilia muda wake wa kazi na masomo kwa kuzingatia taratibu na maelekezo ya chuo na wasimamizi. Mimi sioni shida mtu kuhitimu kama anazingatia hayo,” alisema Profesa Bee
Profesa Bee alisema watu wengi wanaosoma shahada ya uzamili na uzamivu wakati wanafanya kazi na wana majukumu mengi, hivyo si sahihi kumhukumu mtu kisa ni mwanasiasa.
Profesa huyo alisema kama mwanafunzi anayesoma anayo nidhamu ya muda, licha ya majukumu yake, lazima atapata wasaa wa kukusanya taarifa.
“Hapa tuna walimu wengi wanasoma uzamivu na wanaendelea na kazi zao za kufundishia wakati nao wanasoma, hivyo suala sio nani, bali vigezo.
Wote hao (mawaziri, wabunge) wamefuata utaratibu wa usimamizi na kuwasilisha mawasilisho ambayo waliyatetea mbele ya jopo la wanataaluma,” alisema Profesa Bee.
Alisema mtu kazi kama si ya kwake, angeshindwa kuitetea, lakini wote walitetea kazi zao vizuri na taarifa na machapisho yao yanapatikana katika chuo hicho na watu wanaweza kuyaona kwa kuwa ni ya umma.
Mjadala huo uliibuliwa juzi na mwanazuoni na mwanasiasa mkongwe, Profesa Mark Mwandosya alipoandika kupitia Twitter: “Nawapongeza wanasiasa mliotunukiwa shahada za uzamivu, udaktari wa falsafa. Nawafahamu mna uwezo mkubwa. Lakini inawezekana kweli ukawa mbunge na waziri, ukapata muda wa utafiti na kuandika tasnifu, hata ya uzamili ni kazi sana. Swali kwa vyuo vikuu, je, vigezo au viwango vimebadilika?” alihoji Profesa Mwandosya.
Mbali ya kuwahi kuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwandosya pia aliwahi kuwa mbunge na waziri katika Serikali za tatu na nne.
Swali hilo limewaalika wanazuoni mbalimbali na mijadala kwenye mitandao ya kijamii, baadhi walimpinga na wengine wakimuunga mkono.
Gazeti la mwananchi la 21/12/2021
Ilipaswa tuwe tumeshatoka huko miaka mingi nyuma, sayansi inaendelea kila siku au labda wana sababu kwanini hayapatikani haya machapisho kirahisi hatuwezi juahatutaki story nyingi,
waweke hayo machapisho yao kwenye web ya chuo tuyapitie wenyewe.
Nadhani zinahifadhiwa kwenye vyuo husika, sina hakika sanaHivi publications za PhD huwa zinahifadhiwa chuoni wa zinakuwa published kwenye international journals? zinahifadhi liblary kama za undergraduates
Zinatakiwa ziwekwe kwenye mtandao, UDOM wana hiyo system lakini hizo za wanasiasa kamwe huto zikuta. Tatizo na waandishi wetu huwa hawana utamaduni wa kuwabana wanaowahoji na maswali ya msingiNadhani zinahifadhiwa kwenye vyuo husika, sina hakika sana
Hili ndio jibu PhD lazima upublishi si chini ya publication mbili ili zipitiwe na wataalamu wengine kwenye Internation Journals. Hapa kwetu wanabebana tu ndio maana hata Prof. M. Mwandosya pia alihoji hili jamboZinatakiwa ziwekwe kwenye mtandao, UDOM wana hiyo system lakini hizo za wanasiasa kamwe huto zikuta. Tatizo na waandishi wetu huwa hawana utamaduni wa kuwabana wanaowahoji na maswali ya msingi
Wanaamini watanzania wote ni mbumbumbu,hatujua kufuatilia mambo.Hizi ni zama za tehama, kwa nini mtu aende mpaka chuoni kupata machapisho ya kazi zao ?
Nini kazi ya UDOM institutional repository ?
Kwa nini kazi za wanafunzi wengine zinawekwa huko lakini hizo za hao wanasiasa haizpatikani mpaka mtu aende mguu kwa mguu ?
View attachment 2053069
Profesa ameongea kisiasa.......Kwa ufupi ni kwamba no publications at all. Graduates wote kuanzia degree ya kwanza hadi ya tatu wanaondoka na leaving certificate.Chuo kikubwa kama UDOM kukosekana kwa haya machapisho kwenye mtandao ni uzamani sana. Au profesa hajaona umuhimu wa hiki kitu, kwa hiyo mtu aliye mfano nje ya nchi akihitaji kupitia haya machapisho afunge safari mpaka Tanzania?
Kama kuna uwalakini wa namna hii sasa si ni vyema zote zisiwekwe?Zinatakiwa ziwekwe kwenye mtandao, UDOM wana hiyo system lakini hizo za wanasiasa kamwe huto zikuta. Tatizo na waandishi wetu huwa hawana utamaduni wa kuwabana wanaowahoji na maswali ya msingi
Wanakwepa aibu tuIlipaswa tuwe tumeshatoka huko miaka mingi nyuma, sayansi inaendelea kila siku au labda wana sababu kwanini hayapatikani haya machapisho kirahisi hatuwezi jua
Wanataka uende direct chuoni Ili utekwe na wasio julikanaHizi ni zama za tehama, kwa nini mtu aende mpaka chuoni kupata machapisho ya kazi zao ?
Nini kazi ya UDOM institutional repository ?
Kwa nini kazi za wanafunzi wengine zinawekwa huko lakini hizo za hao wanasiasa haizpatikani mpaka mtu aende mguu kwa mguu ?
View attachment 2053069
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hizi ni zama za tehama, kwa nini mtu aende mpaka chuoni kupata machapisho ya kazi zao ?
Nini kazi ya UDOM institutional repository ?
Kwa nini kazi za wanafunzi wengine zinawekwa huko lakini hizo za hao wanasiasa haizpatikani mpaka mtu aende mguu kwa mguu ?
View attachment 2053069
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Udom ni chuo cha kisiasa.
Hata wakiwapa PhD wabunge wote ni sawa tu.
Mi naiheshimu PhD ya Mwigullu Nchemba kutoka Makerere tu hao wengine tupa kule!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hiki chuo cha UDom kinazidi kujengewa image mbaya kadri miaka inavyosonga. Kuna interview fulani ya kazi rafiki angu alishinda, wenzake wote walifyekwa kisa tu wamesoma UDom, yeye kasoma kwingne.
Ndiyoo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Chuo kikubwa kama UDOM kukosekana kwa haya machapisho kwenye mtandao ni uzamani sana. Au profesa hajaona umuhimu wa hiki kitu, kwa hiyo mtu aliye mfano nje ya nchi akihitaji kupitia haya machapisho afunge safari mpaka Tanzania?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] tena amejipambanua wazi wazi ktk kutetea uongo huu mubashara, eti watu waende maktaba ya chuo, lol.Dah Prof Faustine K Bee anajishusha.
Wahadhiri wengi kusoma kwao ni rahisi maana wanashinda wanafundisha hivyo vitu,na kuna assignment hutoa kwa wanafunzi zinawasaidia hata wao katika masomo yao.
Sasa mwanasiasa akashinde anazurula bungeni kweli,na wao kirahisi tu wanampa PhD!
Sikutegemea haya kwa msomi na kiongozi wetu mkubwa kama prof.K Bee.