Uongozi UDOM watetea PhD za Mawaziri, na Wabunge

Uongozi UDOM watetea PhD za Mawaziri, na Wabunge

J1 hii Mombasa, meli ilibainika kuwa na mzigo wenye mionzi ya nuclear ukiletwa Bongo.

JF tunajadili kesi ya ....; PhD za .....; Shule ya Uongozi,,, n.k.

Samahani, simaanishi kupanga nini cha kujadili. Namuomba MUNGU AIBARIKI TANZANIA
 
Siku mbili baada ya shahada za uzamivu (PhD) za viongozi wa kisiasa hasa Mawaziri na Wabunge kuibua mjadala, uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) umezitetea na kueleza namna ya kuondoa shaka juu yake.

Akizungumza na Mwananchi, Makamu Mkuu wa UDOM, Profesa Faustine Bee amesema wenye shaka wanaweza kujiridhisha kwa kutembelea maktaba ya chuo hicho kuona machapisho ya wahitimu wenyewe.

Alisema suala la viongozi wakubwa kuhitimu shahada za uzamivu ni la muhusika mwenyewe anavyojipanga, kupangilia muda wake na majukumu aliyonayo.

“Ni suala la nidhamu ya muda, mtu kupangilia muda wake wa kazi na masomo kwa kuzingatia taratibu na maelekezo ya chuo na wasimamizi. Mimi sioni shida mtu kuhitimu kama anazingatia hayo,” alisema Profesa Bee

Profesa Bee alisema watu wengi wanaosoma shahada ya uzamili na uzamivu wakati wanafanya kazi na wana majukumu mengi, hivyo si sahihi kumhukumu mtu kisa ni mwanasiasa.

Profesa huyo alisema kama mwanafunzi anayesoma anayo nidhamu ya muda, licha ya majukumu yake, lazima atapata wasaa wa kukusanya taarifa.

“Hapa tuna walimu wengi wanasoma uzamivu na wanaendelea na kazi zao za kufundishia wakati nao wanasoma, hivyo suala sio nani, bali vigezo.

Wote hao (mawaziri, wabunge) wamefuata utaratibu wa usimamizi na kuwasilisha mawasilisho ambayo waliyatetea mbele ya jopo la wanataaluma,” alisema Profesa Bee.

Alisema mtu kazi kama si ya kwake, angeshindwa kuitetea, lakini wote walitetea kazi zao vizuri na taarifa na machapisho yao yanapatikana katika chuo hicho na watu wanaweza kuyaona kwa kuwa ni ya umma.

Mjadala huo uliibuliwa juzi na mwanazuoni na mwanasiasa mkongwe, Profesa Mark Mwandosya alipoandika kupitia Twitter: “Nawapongeza wanasiasa mliotunukiwa shahada za uzamivu, udaktari wa falsafa. Nawafahamu mna uwezo mkubwa. Lakini inawezekana kweli ukawa mbunge na waziri, ukapata muda wa utafiti na kuandika tasnifu, hata ya uzamili ni kazi sana. Swali kwa vyuo vikuu, je, vigezo au viwango vimebadilika?” alihoji Profesa Mwandosya.

Mbali ya kuwahi kuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwandosya pia aliwahi kuwa mbunge na waziri katika Serikali za tatu na nne.

Swali hilo limewaalika wanazuoni mbalimbali na mijadala kwenye mitandao ya kijamii, baadhi walimpinga na wengine wakimuunga mkono.
Gazeti la mwananchi la 21/12/2021
Hivi publications za PhD huwa zinahifadhiwa chuoni wa zinakuwa published kwenye international journals? zinahifadhi liblary kama za undergraduates
 
Hivi publications za PhD huwa zinahifadhiwa chuoni wa zinakuwa published kwenye international journals? zinahifadhi liblary kama za undergraduates
Nadhani zinahifadhiwa kwenye vyuo husika, sina hakika sana
 
Zinatakiwa ziwekwe kwenye mtandao, UDOM wana hiyo system lakini hizo za wanasiasa kamwe huto zikuta. Tatizo na waandishi wetu huwa hawana utamaduni wa kuwabana wanaowahoji na maswali ya msingi
Hili ndio jibu PhD lazima upublishi si chini ya publication mbili ili zipitiwe na wataalamu wengine kwenye Internation Journals. Hapa kwetu wanabebana tu ndio maana hata Prof. M. Mwandosya pia alihoji hili jambo
 
Hizi ni zama za tehama, kwa nini mtu aende mpaka chuoni kupata machapisho ya kazi zao ?

Nini kazi ya UDOM institutional repository ?

Kwa nini kazi za wanafunzi wengine zinawekwa huko lakini hizo za hao wanasiasa haizpatikani mpaka mtu aende mguu kwa mguu ?

View attachment 2053069
Wanaamini watanzania wote ni mbumbumbu,hatujua kufuatilia mambo.
Hivi inawezekanaje ukute machapisho wa wahitimu wengine ukose la waziri,yeye ni hakua mwanafunzi,why amehitimu?!

Kwa mifumo hii tusitegemee kuwa na Bunge lenye Meno,linaloweza kutafsiri na kutunga sheria zenye malengo ya kuistawisha nchi na wananchi.

Elimu ya bongo,tumepigwaa
 
Chuo kikubwa kama UDOM kukosekana kwa haya machapisho kwenye mtandao ni uzamani sana. Au profesa hajaona umuhimu wa hiki kitu, kwa hiyo mtu aliye mfano nje ya nchi akihitaji kupitia haya machapisho afunge safari mpaka Tanzania?
Profesa ameongea kisiasa.......Kwa ufupi ni kwamba no publications at all. Graduates wote kuanzia degree ya kwanza hadi ya tatu wanaondoka na leaving certificate.
 
Kwa mazingira kama,hayo, kuna uhalakini .... juu ya phD zao ....prof mwandosia hana logic za msimgi sana ila ....wanamjibu kizembe sana,
Then issue ya kusoma thesis ni pana sana kuna vichwa tunavijua vzuri.. kupata u-doctor..
Siyo isue.. nyepesi kiivyo..
Vile vile ili ku- clarify wangeweka Research zao public
 
Hamna kitu hapo.. tulikuwa tu lazima aweke hizo justifications..
Pumbafu zake huyo Pr
 
Zinatakiwa ziwekwe kwenye mtandao, UDOM wana hiyo system lakini hizo za wanasiasa kamwe huto zikuta. Tatizo na waandishi wetu huwa hawana utamaduni wa kuwabana wanaowahoji na maswali ya msingi
Kama kuna uwalakini wa namna hii sasa si ni vyema zote zisiwekwe?

Unaweza nisaidia Cannabis namna ya kuzipata au kuingia katika hiyo system tusome hata hizi zilizopo?
 
Hizi ni zama za tehama, kwa nini mtu aende mpaka chuoni kupata machapisho ya kazi zao ?

Nini kazi ya UDOM institutional repository ?

Kwa nini kazi za wanafunzi wengine zinawekwa huko lakini hizo za hao wanasiasa haizpatikani mpaka mtu aende mguu kwa mguu ?

View attachment 2053069
Wanataka uende direct chuoni Ili utekwe na wasio julikana
 
Hizi ni zama za tehama, kwa nini mtu aende mpaka chuoni kupata machapisho ya kazi zao ?

Nini kazi ya UDOM institutional repository ?

Kwa nini kazi za wanafunzi wengine zinawekwa huko lakini hizo za hao wanasiasa haizpatikani mpaka mtu aende mguu kwa mguu ?

View attachment 2053069
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Udom ni chuo cha kisiasa.

Hata wakiwapa PhD wabunge wote ni sawa tu.

Mi naiheshimu PhD ya Mwigullu Nchemba kutoka Makerere tu hao wengine tupa kule!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hiki chuo cha UDom kinazidi kujengewa image mbaya kadri miaka inavyosonga. Kuna interview fulani ya kazi rafiki angu alishinda, wenzake wote walifyekwa kisa tu wamesoma UDom, yeye kasoma kwingne.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Chuo kikubwa kama UDOM kukosekana kwa haya machapisho kwenye mtandao ni uzamani sana. Au profesa hajaona umuhimu wa hiki kitu, kwa hiyo mtu aliye mfano nje ya nchi akihitaji kupitia haya machapisho afunge safari mpaka Tanzania?
Ndiyoo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dah Prof Faustine K Bee anajishusha.
Wahadhiri wengi kusoma kwao ni rahisi maana wanashinda wanafundisha hivyo vitu,na kuna assignment hutoa kwa wanafunzi zinawasaidia hata wao katika masomo yao.

Sasa mwanasiasa akashinde anazurula bungeni kweli,na wao kirahisi tu wanampa PhD!

Sikutegemea haya kwa msomi na kiongozi wetu mkubwa kama prof.K Bee.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] tena amejipambanua wazi wazi ktk kutetea uongo huu mubashara, eti watu waende maktaba ya chuo, lol.
Aweke mtandaoni ili hata aliye kuwepo Cuba ajionee. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom