DOKEZO Uongozi wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika, unatuvuruga baadhi ya Wanafunzi, wanadai tumelipa fedha “hewa”

DOKEZO Uongozi wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika, unatuvuruga baadhi ya Wanafunzi, wanadai tumelipa fedha “hewa”

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Torra Siabba

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
289
Reaction score
415
SHAHADA YA SAYANSI YA DATA,_page-0001.jpg

SHAHADA YA SAYANSI YA DATA,_page-0002.jpg
Sisi ni wanafunzi wa mwaka wa tatu wa Shahada ya Sayansi ya Data kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika. Tunaomba msaada wa haraka kuhusu changamoto kubwa ya fedha zilizokwisha lipwa na bado tuanendelea kutozwa kila mwaka wa masomo lakini huduma zake hazikutolewa kama inavyotakiwa.

Tumelipa kiasi cha Tsh 100,000 kila mwaka kwa ajili ya field supervision (2022/2023 na 2023/2024), na Tunatakiwa kulipa pia 2024/2025 lakini hatukupata usimamizi wakati wa field training na hata matokeo ya mwaka wa pili alama zake kutokuonekana licha ya kutambulishwa kama somo.

Pia tumelipa Tsh 200,000 kwa kila mwaka (2022/2023, 2023/2024) na tunakiwa kulipa pia kwa mwaka 2024/2025 kwa matumizi ya maabara ya kompyuta, lakini hadi sasa tunatumia vifaa binafsi kwa shughuli za kitaaluma na Chumba hicho cha kopmyuta kutumiwa kama chumba cha kufundishia. Hii inamaanisha kuwa fedha hizi zimekuwa malipo hewa.

Tumechukua hatua mbalimbali zifuatazo:

1. Tumejadili suala hili kwenye Baraza la Wanafunzi (Students’ Baraza) toka mwaka wa kwanza na kuhaidiwa litatafutiwa suluhu bila majibu.
2. Tumeibua hoja madarasani na kwenye vikao mbalimbali vya wanafunzi na kupelekea kuwasilisha malalamiko kwa serikali ya wanafunzi (EASTCSO) bila kupata majibu kutokana na kilicho semwa ni ushirikiano hafifu na kupuuzwa kwa madai hayo na uongozi wa chuo
3. Tumeomba maelezo kutoka kwa uongozi wa chuo kupitia vikao rasmi na barua, lakini hatujapewa majibu yoyote hadi sasa.

Tumeambatanisha ushahidi wa malipo ya hostel, ada, direct cost na malipo mengine ya "Other Fee" ili kuthibitisha madai yetu.

Tunaomba mamlaka husika zitupe msaada kwani asilimia kubwa ya wanafunzi tunaathiriwa na hali hii, hasa wanaotoka katika mazingira magumu.

Baadhi yetu tunazuiwa kufanya mitihani kwa sababu ya kutolipa ada kamili, hali inayotufanya kukatisha masomo yetu.
WhatsApp Image 2025-05-30 at 22.36.44_b4f10f29.jpg
 
Back
Top Bottom