Uongozi wa Shule ya Pugu mmefeli sana kumuweka Mpoki kuwa mgeni rasmi wa mahafali yenu

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Katika mazingira ya elimu, mahafali si sherehe ya kawaida bali ni jukwaa la maono, msukumo na mwelekeo wa maisha ya wahitimu. Ndiyo maana uchaguzi wa mgeni rasmi hubeba uzito mkubwa kuliko inavyodhaniwa, kuna wakati viongozi waandamizi haswa mkuu wa shule pamoja na wasaidizi wake huzungusha barua kuomba mtu fulani awe mtu muhimu kwtika mahafali.
​
Yaani kifupi mgeni rasmi anapaswa kuwa kielelezo cha mafanikio ya kitaaluma, uadilifu, na mchango chanya kwa jamiiβ€”mtu ambaye hadithi yake inaweza kuwasha taa ya matumaini na nidhamu kwa vijana wanaohitimu.

Sasa ni jambo la ajabu na lenye kusikitisha kuona baadhi ya taasisi za elimu zikiyumbisha mizani hii kwa kuweka mbele umaarufu wa burudani badala ya hekima na uzoefu. Wahitimu wanahitaji kusikia sauti ya mtu aliyepitia changamoto za maisha, akajenga misingi imara ya taaluma na uongozi. Vijana wetu wanahitaji mawaidha yanayogusa mustakabali waoβ€”sio tu vichekesho vinavyopita haraka kama upepo.

Nimeshangaa sana kuona Shule kubwa kama Pugu kuweka wazi ya kwamba Mpoki anakwenda kuwa Mgeni ramsi wa Mahafali yao ya 55, serious kabsa. Uongozi wa shule mmefeli pakubwa sana. Tanzania kuna watu wengi sana ambao wanaweza kusimama na kuzungumza na wahitimu mambo ya msingi kuliko vituko na jokes za ajabu.

Kwa historia ya shule ya Pugu nadhani hii ni kali ya mwaka kwa hakika! Na ipo siku kama hii tabia viongozi wataiona kama ni mtindo mzuri..

Ipo siku utasikia Chumvi Nyingi* ni mgeni rasmi kwenye mahafali ya shule ya sekondari Minaki, huku Mama Shea ama Giggy Money amekuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya shule ya wasichana Jangwani.

Kuchagua mgeni rasmi asiyeendana na muktadha wa kitaaluma kunaweza kupotosha vipaumbele vya vijana na kudhoofisha hadhi ya taasisi yenyewe. Kwa hili mmefeli pakubwa sana.
 
Shule km Pugu, ina historia kubwa na nzito, wamepita watu wa maana, wakiwepo Ma Ex Prezidaas, mawaziri etc.
Kwanini wasingechagua hata Kitila Mkumbo kuwa Special Guest.

Huyo Mpoki ataongea nini mbele ya kadamnasi ya wanafunzi kuwa motivate?

Mkuu wa shule ya Pugu awajibishwe, sio kwa fedheha na kejeri hiyo kwa pugu alumnus.
Lol
 
Mgeni rasmi anaweza kuwa mtu yeyote kwa sababu haongezi thamani yoyote kwa wahitimu bali anaweza kutumika katika kutatua kero iliyopo hapo shuleni (fedha) na mara nyingi waajiriwa huwa hawawezi; muhimu kwa wahitimu ni cheti tu.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…