Uongozi wa Shule ya Pugu mmefeli sana kumuweka Mpoki kuwa mgeni rasmi wa mahafali yenu

Uongozi wa Shule ya Pugu mmefeli sana kumuweka Mpoki kuwa mgeni rasmi wa mahafali yenu

Damaso, nimekusoma vizuri sana na hoja zako zina mashiko makubwa, hasa kuhusu umuhimu wa mgeni rasmi kuwa kielelezo cha mafanikio na uadilifu. Ni kweli, tunatamani vijana wetu wapate msukumo wa kitaaluma na maisha kutoka kwa wale waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali.

Lakini pia, nafikiri tunaweza kutoa nafasi kidogo kuona labda Mpoki anaweza kuwa na ujumbe wa kipekee ambao bado utawajengea vijana wetu. Mara nyingi watu maarufu kama yeye huwa na safari ndefu na yenye changamoto walizopitia kabla ya kufikia hapo walipo, na huenda akashiriki uzoefu huo wa maisha na jinsi alivyoitumia elimu yake (kama anayo) kufika hapo alipo. Kumbuka, hata vichekesho vinaweza kubeba hekima kubwa na kuwafikia vijana kwa njia tofauti.

Ni matumaini yangu kwamba uongozi wa Pugu walifanya uamuzi huu kwa kuzingatia jambo fulani ambalo bado hatujaliona wazi, na kwamba Mpoki atatumia jukwaa hili kutoa maneno ya busara na motisha badala ya burudani pekee. Muhimu ni ujumbe utakaotolewa na jinsi utakavyopokelewa na wahitimu wetu. Tuwe na subira kidogo, tusihukumu haraka! Labda tutashangaa.
Hata Gigy money ni maarufu, wangempa yeye hiyo nafasi.
 
Usimfananishe Giggy money na Mpoki mkuu, maana Mpoki hayupo kwenye files za Epstein.
 
Hata Gigy money ni maarufu, wangempa yeye hiyo nafasi.
Hivi kweli Kwenye Mahafali ya Weruweru eti mgeni rasmi awe GIGGY MONEY au Mahafali ya Bwiru Boys mgeni rasmi ni Ngoma Nagwa?
 
Badala ya wahitimu kupewa mbinu za kupambana na soko la ajira, wanaenda kufundishwa jinsi ya kuchekesha watu kwa sauti ya kike.

Niaibu!
 
Bila shaka huyo mkuu wa shule atakuwa amepata ushauri kutoka kwa naibu waziri wa elimu mbalimbali Prof. Dr. Wanu Samuya!
Yaani sure Mkuu! Kwamba amekosa hawa CEO wote wa Mabenki Dar es Salaam hapo? Wale big fish 😔 duuh Pugu imekuwa Pogo
 
Katika mazingira ya elimu, mahafali si sherehe ya kawaida bali ni jukwaa la maono, msukumo na mwelekeo wa maisha ya wahitimu. Ndiyo maana uchaguzi wa mgeni rasmi hubeba uzito mkubwa kuliko inavyodhaniwa, kuna wakati viongozi waandamizi haswa mkuu wa shule pamoja na wasaidizi wake huzungusha barua kuomba mtu fulani awe mtu muhimu kwtika mahafali.
Yaani kifupi mgeni rasmi anapaswa kuwa kielelezo cha mafanikio ya kitaaluma, uadilifu, na mchango chanya kwa jamii—mtu ambaye hadithi yake inaweza kuwasha taa ya matumaini na nidhamu kwa vijana wanaohitimu.
View attachment 3572750
Sasa ni jambo la ajabu na lenye kusikitisha kuona baadhi ya taasisi za elimu zikiyumbisha mizani hii kwa kuweka mbele umaarufu wa burudani badala ya hekima na uzoefu. Wahitimu wanahitaji kusikia sauti ya mtu aliyepitia changamoto za maisha, akajenga misingi imara ya taaluma na uongozi. Vijana wetu wanahitaji mawaidha yanayogusa mustakabali wao—sio tu vichekesho vinavyopita haraka kama upepo.
View attachment 3572751
Nimeshangaa sana kuona Shule kubwa kama Pugu kuweka wazi ya kwamba Mpoki anakwenda kuwa Mgeni ramsi wa Mahafali yao ya 55, serious kabsa. Uongozi wa shule mmefeli pakubwa sana. Tanzania kuna watu wengi sana ambao wanaweza kusimama na kuzungumza na wahitimu mambo ya msingi kuliko vituko na jokes za ajabu.
View attachment 3572752
Kwa historia ya shule ya Pugu nadhani hii ni kali ya mwaka kwa hakika! Na ipo siku kama hii tabia viongozi wataiona kama ni mtindo mzuri..
View attachment 3572754
Ipo siku utasikia Chumvi Nyingi* ni mgeni rasmi kwenye mahafali ya shule ya sekondari Minaki, huku Mama Shea ama Giggy Money amekuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya shule ya wasichana Jangwani.
View attachment 3572753
Kuchagua mgeni rasmi asiyeendana na muktadha wa kitaaluma kunaweza kupotosha vipaumbele vya vijana na kudhoofisha hadhi ya taasisi yenyewe. Kwa hili mmefeli pakubwa sana.
KAMA NI KWELI, BASI HII NI blunder NA LAZIMA SERIKALI itachukua hatua
 
Back
Top Bottom