Katika mazingira ya elimu, mahafali si sherehe ya kawaida bali ni jukwaa la maono, msukumo na mwelekeo wa maisha ya wahitimu. Ndiyo maana uchaguzi wa mgeni rasmi hubeba uzito mkubwa kuliko inavyodhaniwa, kuna wakati viongozi waandamizi haswa mkuu wa shule pamoja na wasaidizi wake huzungusha barua kuomba mtu fulani awe mtu muhimu kwtika mahafali.
Yaani kifupi mgeni rasmi anapaswa kuwa kielelezo cha mafanikio ya kitaaluma, uadilifu, na mchango chanya kwa jamii—mtu ambaye hadithi yake inaweza kuwasha taa ya matumaini na nidhamu kwa vijana wanaohitimu.
View attachment 3572750
Sasa ni jambo la ajabu na lenye kusikitisha kuona baadhi ya taasisi za elimu zikiyumbisha mizani hii kwa kuweka mbele umaarufu wa burudani badala ya hekima na uzoefu. Wahitimu wanahitaji kusikia sauti ya mtu aliyepitia changamoto za maisha, akajenga misingi imara ya taaluma na uongozi. Vijana wetu wanahitaji mawaidha yanayogusa mustakabali wao—sio tu vichekesho vinavyopita haraka kama upepo.
View attachment 3572751
Nimeshangaa sana kuona Shule kubwa kama Pugu kuweka wazi ya kwamba Mpoki anakwenda kuwa Mgeni ramsi wa Mahafali yao ya 55, serious kabsa. Uongozi wa shule mmefeli pakubwa sana. Tanzania kuna watu wengi sana ambao wanaweza kusimama na kuzungumza na wahitimu mambo ya msingi kuliko vituko na jokes za ajabu.
View attachment 3572752
Kwa historia ya shule ya Pugu nadhani hii ni kali ya mwaka kwa hakika! Na ipo siku kama hii tabia viongozi wataiona kama ni mtindo mzuri..
View attachment 3572754
Ipo siku utasikia
Chumvi Nyingi* ni mgeni rasmi kwenye mahafali ya shule ya sekondari Minaki, huku
Mama Shea ama
Giggy Money amekuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya shule ya wasichana Jangwani.
View attachment 3572753
Kuchagua mgeni rasmi asiyeendana na muktadha wa kitaaluma kunaweza kupotosha vipaumbele vya vijana na kudhoofisha hadhi ya taasisi yenyewe. Kwa hili mmefeli pakubwa sana.