Uongozi wa Shule ya Pugu mmefeli sana kumuweka Mpoki kuwa mgeni rasmi wa mahafali yenu

Mtu yeyote anaweza kuwa mgeni rasmi as long as ana akili timamu.
Acha ubaguzi mwalimu mkuu katisha
 
Sasa wakubwa wenyewe wana elim za hapa na pale si Bora hata walio alika mpoki wacheke tu!
 
Labda wamekosa mtu wa maana aliyewahi kusoma hiyo shule awe mgeni rasmi
Wapo kibao! Mpoki anakwenda kuwachekesha vijana wasiwe na presha ya Paper la NECTA
 
Kuchagua mgeni rasmi asiyeendana na muktadha wa kitaaluma kunaweza kupotosha vipaumbele vya vijana na kudhoofisha hadhi ya taasisi yenyewe. Kwa hili mmefeli pakubwa sana.
Mboni mimi sijaona shida hapo asee au nipo na mawazo tofauti kidogo? Ulitaka aende nani Daktari Bingwa Bobezi wa Kutibu Mifupa ya Ubongo kutoka Kizimkazi?
 
sion kama ipo shida kumpa mpoki hiyo nafasi ,elimu sio tu ya kusongoka yani tuamini kwamba ili utoboe maisha ni lazima usome sana uwe na A A B A hapana maisha ni namna utayachukulia,mtu kama mpoki plan B imemtoa pia ni maarufu atakua na cha kuwashauri kwa plan B,shida mnakariri dunia hataki hivyo hata maisha
 
Mkuu unawaonea bure.

Umechanganya maana ya SPECIAL GUEST na GUEST OF HONOR.

Hapo kazi ya mpoki ni kuongeza mvuto wa sherehe tu na sio mgeni rasmi.
Good point ndio maana na mimi nikasema sijaona shida hapo sasa nashangaa mdau ameenda mbali sana au ana jambo lake nyuma ya pazia?
 
Mgeni rasmi anaweza kuwa mtu yeyote kwa sababu haongezi thamani yoyote kwa wahitimu bali anaweza kutumika katika kutatua kero iliyopo hapo shuleni (fedha) na mara nyingi waajiriwa huwa hawawezi; muhimu kwa wahitimu ni cheti tu.​
Mgeni rasmi hapaswi kuwa yoyote bali anapaswa kuwa mtu mwenye mafanikio makubwa katika tasnia fulani au uongozi ambaye atawa inspire wahitimu kwa hatua zitakazofuata za elimu yao au kazi baadaye na inakuwa vizuri zaidi kama alisoma hiyo shule au chuo(alumni).
 
Mpoki wala huwezi kuhesabu ni mmojawapo wa watu ametoboa maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…