SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Uongozi wa Yanga mnataka kutingisha kiberiti ila sidhani kama mmefikiria vya kutosha madhara ya haya mnayofanya.
Kuna matendo mengi ya hovyo mmehusishwa nayo ambayo yalifukiwa kwa sababu za kisiasa. Huku mnapokwenda tutalazimika kuyafukua na hamtabaki salama.
1. Tutafufua udhamini usio halali wa Mfadhili, Mdhamini na anayeonekana kama Mmiliki asiye rasmi wa Klabu ya Yanga kwa vilabu vingine kadhaa vya ligi ya NBC, kampuni ya GSM, na jinsi udhamini huo umeleta viashiria vya upangaji wa matokeo kwa nia ya kuinufaisha Yanga.
2. Tutafufua jinsi mmoja wa wajumbe wa bodi ya wadhamini wa Yanga anavyohusika kuvidhoofisha vilabu vinavyotoa ushindani kwa Yanga kwa kuvinunua na kuvivuruga kwa nia ya kuifaidisha Yanga.
3. Tutafufua mgongano wa maslahi uliopo kati ya Yanga na timu ya Dodoma Jiji na jinsi mgongano huo unavyoinufaisha Yanga.
4. Tutafufua jinsi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, anayejulikana na aliyejitambulisha wazi kuwa ni shabiki kindakindaki wa Yanga alivyojaribu kutumia vibaya madaraka yake ya kisiasa kuingilia masuala ya soka kwa nia ya kuifaidisha Yanga.
5. Tutafufua tuhuma za utumiaji madawa ya kuongeza nguvu zinayowakabili baadhi ya wachezaji wenu.
6. Tutafufua tuhuma za kuwatumia waamuzi kuwapa maamuzi ya kuwapendelea timu ya Yanga bila waamuzi hao kuchukuliwa hatua zozote. Kuanzia magoli ya mikono, penati zinazotokana na faulo za nje ya box, penati za Kibu kwenye derby ya kwanza, nk. Yaani mchezaji anafunga goli la mkono halafu anaenda kuwa Man of the Match, we umesikia waaapi?
7. Tutafufua rushwa iliyotumika kwenye derby ya November 5, 2023 kwa nia ya kuinufaisha Yanga. Msione tulikaa kimya, vithibitisho tunavyo na hamchomoki kwenye hili.
8. Tutafufua jinsi klabu inayomilikiwa na mmoja wa wajumbe wa bodi ya wadhamini wa Yanga ilivyokiuka sheria na taratibu za nchi na ligi kwa kuwapa uraia kiholela wachezaji wa nje kwa nia ya kuinufaisha Yanga.
9. Tutafufua jinsi mabaunsa na watendaji wa Yanga walivyohusika na vitendo vya kihuni, vurugu na jinai dhidi ya mashabiki, waandishi wa habari za michezo na viongozi wa timu nyingine bila wahusika kuchukuliwa hatua zozote za kinidhamu wala kisheria.
10. Tutafufua matendo yanayojirudia mara kwa mara yenye viashiria vya imani za kishirikina yanayoendelea kufanywa na klabu ya Yanga bila mamlaka husika kutoa adhabu kali zaidi kukomesha vitendo hivyo na mara nyingine mamlaka hizo kuonekana kubariki vitendo hivyo.
Usipopewa heshima yako kwa hiari unalazimika kuidai kwa nguvu.