Upande wa pili wa usalama wa Taifa ukoje?

Tatizo ni pale ambapo idara hii wanachukuana makada wa CCM, bila kujali u-smart kichwani ,uzalendo n.k.
Kazi yao kubwa ni kuvaa masuti meusi,kulinda viongozi na kuteka ama kuua wapinzani wa serikali.
Hii sio sawa.
Naililia NCHI yangu Tanzania.
 
Idara ya Usalama wa Taifa iweke wazi Ofisi zake zilipo na iajiri kwa wazi kama CIA wanavyofanya. Sio mambo yote ya kufanyia gizani
Ofisi zilipo kaka Yoda ? Hawawezi na hawatoweza tizama hata sehemu zinazosemwa ndizo ila ukweli sizo.
 
Idara ya Usalama wa Taifa iweke wazi Ofisi zake zilipo na iajiri kwa wazi kama CIA wanavyofanya. Sio mambo yote ya kufanyia gizani
Hawa usalama wa taifa wana shida sana aisee na wanakera sana wana shida mbili iko hivi wao wanajiona ndo wao wakati kiuhalisia ni watoto wadogo sana,

Iko hivi kuna siku nilikuwa Kigoma kikazi sasa siku iyo kulikuwa kuna vijana wa JKT walikuwa wanafanya usafi kwenye holi moja wapo ambalo waziri mkuu alitakiwa aje pale.

Sasa mm nilikuwa kama msimamizi wa wale vijana wa JKT natoa code tuu sijali wala nn [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Hii ni true story aisee.


Sasa bhana katika kufanya usafi wale madogo hawa usalama wa taifa si wakaja bhana sasa kama mnavyojua sisi wazee wa kitenge hakuna kitu tuna heshimu kama bendera na katiba yani bendera tunaheshimu vibaya mno..


Ww ukitaka zinguana na sisi basi mess up katika hivyo vitu viwili bendera na katiba,[emoji41][emoji41] mana sisi tupo kwa ajiri ya kusave hivyo vitu viwili tu bendera na katiba basi na si kingine tuna viheshimu sana

Sasa bana siku iyo ilikuwa saa kumi na mbili jioni mzee madogo wakawa wanashusha bendera sasa ujue bana kama nilivyosema sisi wa kwetu kwetu huwa tunaheshimu bendera vibaya mno bendera ikishushwa lazima tuheshimu.

Bwana wee yule dogo wakati anashusha bendera aisee kuna uyo usalama wa taifa anajifanya eti anakagua kagua mazingira na wakati filimbi imepigwa watu tumesimama yy anajikuta anatembea tembea na kukagua kagua mazingira tulimuacha mpaka bendera ilivyoshushwa.


Sasa baada ya kushushwa bendera tukamfata tukamwambia ww ni mzarendo gani usiheshimu bendera akawa mjuaji anaoongea shit aloo tulichukua fimbo tukanza mchapa aisee chapa sana akajifanya kutoa eti kipisto chake akapiga juu..


Tukamwambia ww ni mpuuzi eeh yani unatutishia sisi pisto na wakati sisi tunacheza na silaa ambazo ww tokea uzaliwe ujawai ziona hata tulimzingua likawa bonge moja la vagi mpaka wakuu wakaja.


Wakuu walikuwa wakuu wao na wakuu wetu mana ugomvi ulikuwa mkubwa sana ishu ikasoviwa pale frsh


Sasa bhana kesho yake tulivyoshusha bendera wote wakawa wamesimama wakaheshimu,hivyo basi usalama wa taifa inatakiwa uwe na weledi kama ilivyo usalama wa jeshini IO..usalama wa sikuhivi si wazalendo hawana siri ni wana mambo ya hovyo sana...
 
Shida ni kuwa wako overrated hivyo wanajioverrate pia japo smart wapo japo wengi ni vituko changanya na maisha magumu basi ni vichekesho tu
 
Oooh mwanangu amefeli fomu Foo, naomba mumchoke angalau huko!! Ha ha ha haa
 
Huwa najizuia kuandika juu ya Usalama wa Taifa ,lakini ukweli ni kwamba kati ya taasisi zilizofeli kuleta matundavtarajiwa ni hii.Labda Mimi sielewi,inawezekanaje watu serikalini wanapanga michongo ya kuiba pesa ndefu bila wao kushitukiwa na kuzuiliwa?Je si kazi ya idara ya Usalama wa Taifa kuzuia uhalifu mkubwa unaoleta madhara kwa Taifa?Vipi kuhusu NGO zinazopromote ushoga na kuharibu maadili ya nchi?Wanawezaje kuendesha mambo Yao huku Usalama wa Taifa wako kimya?Hiyo ni mifano michache tu ya jinsi ambayo naona wanafeli kulinda Taifa letu.
 
Hebu ona mfumo huu.

Source ya vyombo vyote vya usalama ni jeshini..


Je tunapataje hao wanajeshi .?

Kwa kutangaza ajira na sifa kama ulifeli form four ndiyo unapewa kipaumbele na siyo mtoto wa masikini ila kwa wenye vyeo na kuhonga ndipo utapata ajira...later on.

-Jeshi na polisi lina mashoga.
-Polisi ni wala rushwa (kama kongo).

-Usalama wa taifa,jeshi,polisi wanatumia nguvu kuwaza na siyo akili muulize (Nape,Roma na lisu)

-Kwanini wanatumia nguvu na siyo akili,-Sababu wanaowalinda yaani raia wana akili kuwazidi na wanapowaambia ukweli wanaona wanawadharau, kulithibitisha hilo jaribu kuongea na askali yeyote na ujaribu kumshusha kama hajakutishia kukulaza sero.

-CCM ili kuendelea kulinda maslahi hao form four failures wanaongezewa kidanganya macho (posho).

-Afrika tutaendelea pale tu,tutakapo ondoa waliofeli kwenye mifumo yote (Ulinzi,Elimu,Afya,Uongozi(serikalini)) ..

Tangu lini aliyefeli akamuongoza ,akamlinda,akamtibu,akamfundisha aliyefaulu πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
......mfumo ubadilidilishwe
Sawa sisi wananchi tumekusikia.

Sasa unataka Mfumo ubadilishweje? Toa mapendekezo ya namna ya kubadili mfumo!? Sisi wananchi, Hatutaki malalamiko ya kero tu tunataka utuandikie mapendekezo ya namna ya kuondoa kero hizo.
 
Sidhani kama hayo ya kuzuia wizi ndio majukumu ya msingi ya hiyo idara ya usalama. Labda kuna sehemu hatuelewi au tunachanganya mambo. Ninavyofahamu kila taasisi ya serikali huwa na kitengo cha Ukaguzi wa ndani (internal audit) ambacho ndio kina jukumu la kukagua na kubaini kama kuna vitu haviko sawa na kuripoti kwa menejimenti. Kama ni lawama basi ziende kwa kitengo hiki ndio jukumu lao la kila siku
 
Hujui ulitendalo. Jua jpm ndo aliharibu nchi hii na kuirudisha kwenye mstari itachukuwa ten years. Hakupenda transparency hivyo watu wakawa wanajipigia tu ndo mana ttcl imejiendesh kwa hasara na Bado wakawa wanalipa gawio the same to Atcl na trc. Angekuwepo jpm tusingesikia haya madudu. Amini nakwambia jpm alikuwa zaidi ya lucifer
 
Hili ndilo neno maana form four failures ndiyo wanaolinda maslahi ya nchi...

Ugumu ni kwamba..
Hao form four failures ndiyo wamejaa jeshini,polisi na kwenye vitengo vinavyotumia silaha kwahiyo mapinduzi ni ngumu kiasi
 
Hili ndilo neno maana form four failures ndiyo wanaolinda maslahi ya nchi...

Ugumu ni kwamba..
Hao form four failures ndiyo wamejaa jeshini,polisi na kwenye vitengo vinavyotumia silaha kwahiyo mapinduzi ni ngumu kiasi

Kwa taarifa yako hao wadogo wala hawapo huko, bali viongozi wao maana ndio wafaidika wa mfumo uliopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…