Konseli Mkuu Andrew
JF-Expert Member
- May 10, 2013
- 749
- 875
Tupo imara kuilinda katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tupo imara kuilinda katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hizi nazo ni taarifa za kutolewa na jeshi wanashindwaje kuwamaliza hao matapeli kimya kimya kama alivyokuwa anafanya Mwendazake nn Maana ya kusajili simu kwa vidoleSalaam Wakuu,
Leo Jeshi la Wananchi Tanzania, linafanya Mkutano na Waandishi wa habari. Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ) kutoa Tamko Maalumu 30 Novemba, 2021
Nipo Nimefika kwenye Ukumbi huu kuwajuza kila kitakachojiri.
=====
UPDATES: 1022hrs
======
View attachment 2027879
Waandishi wameshafika eneo la tukio
1034 hrs: Mkurugenzi wa Habari wa JWTZ, Luteni Kanali Gervas Ilonda
View attachment 2027914
Wengi tumekutana hapa kujua ni nini hasa tunataka kuzungumza. Siji kutoa tamko bali nimekuja kutoa ufafanuzi wa mambo ambayo jeshi limeona yanaendelea. Hatuwezi kuyafumbia macho.
Naomba nitoe ufafanuzi kwa Vijana wanaojiandikisha kujiunga na Jeshi.
Hapo nyuma Viongozi wamekuwa wakitembelea Miradi ya Kimkakati. Wakiwa kule, wamekuwa wakilizishwa na Vija wa kujenga taifa wanavyojituma na kuwa Wazalendo.
Viongozi baada ya kuona uzalendo na umahili wa hali ya Juu wamekuwa wakiwaahidi kwamba nafasi za jeshi zikitka watapata.
Hivi karibu zimetoka nafasi kwa vijana wa Makambi ya JKT sio wote. Zimetoka chache lakini si haba.
Nimelazimika kuongea na vyombo vya habari ili tufahamishe umma kwamba kwa sasa kumeanza kuibuka kwa vitendo cya baadhi ya watu kutumia hizi nafasi za hawa vijana kujinufaisha. Vitendo vya Rushwa na Udanganyifu katika nafasi hizi. Matapeli hao wamekwenda mbali zaidi kwa kusingizia viongozi kwamba wametumwa wamewe hela ili vijana waandikishwe. Wanadai Mkuu wa majeshi ndo amewatuma. Jambo hilo sio kweli. Hatiwezi kulifumbia macho kuona viongozi wetu wanasumbuliwa. Mbaya zaidi wanachukua nyumba za kulala wageni wanaingiza vijana na kuwaambia subiri tunaenda kuwatafutia kazi, matokeo yake wanaanza kuwafuata wakuu wa Majeshi kudai nafasi zao. Kupitia kwenu nawaomba muwapuuze na msidanganyike kutoa fesha kwa nafasi za kuingia jeshini.
Natoa rai kwa wanaofanya Vitendo hivyo kwamba sio vya busara wala kiungwana. Waache mara moja.
Baadhi ya Wazazi wameanza kuwafuata viongozi waliopo Jishini kwenye ngazi mbalimbali kuwaomba wawasaidie kuwaingiza vijana wao Jeshini. Jeshi la Tanzania, lina taratibu na kanuni za kuingiza Vijana Jeshini sio kwa fedha wala kuoneana huruma.
Kijana anatakiwa awe
1). Raia wa Tanzania wa kuzaliwa
2). Umri awe na miaka 18 hadi 28
3) Awe na afya njema ya mwili na akili
4). Lazima awe mwenye tabia njema na nidhamu nzuri, asiwe amepatikana na hatia ya kijinai
5) Awe na cheti halisi cha kuzaliwa, vya shule na chuo.
Kwa Upande wa Madaktari
Awe amemaliza mafunzo kwa vitendo na pamoja na kusaidiwa na bodi ya madaktari.
Hizi ndizo sifa zitatumika kuwachuja vijana Walioandikishwa kuingia Jeshi la wananchi wa Tanzania. Sio wote walioandikishwa watapita.
Kazi ya jeshi ni kazi ngumu, ukiingia kwa hela bila kuwa na utimu wa akili na mwili atapoteza uhai au atakuwa mlemavu
Kazi anayojiandikisha kufanya, wengi wanasema ni ajira. Hakuna mwanajeshi mwenye ajira. Wote wameandikishwa. Mwanajeshi halipwi Mshahara bali malipo. Huwezi kuajiriwa kutoa uhai wako bali unajiandikisha. Unatoa uhai kwa kulinda nchi. Ndo maana hatutoi ajira kwa upendeleo wala Rushwa.
Watanzania tuungane kupinga vitendo hivi viovu vya rushwa, udanganyifu Wizi, halafu akishakuibia analala mbele.
Nawaomba watanzania wote kwa moyo mmoja mkunjufu, tuungane kufichua vitendo hivi. Mkisikia mtu anataka apewe hela, toeni taarifa, jeshini, Polisi na TAKUKURU.
Watanzania tuendelee kuliunga mkono jeshi letu lililo imara. Tupo imara kuilinda katiba ya jamhuru ya Muungano wa Tanzania.
Asanteni sana
Great! Nimekutumia vocha ya 5000.Watanzania na Haswa Muhimili usio Rasmi yaani waandishi wa Habari/vyombo vya Habari vya Tanzania vinapaswa viwe na Uzalendo wa kuweka masilahi ya nchi yao Kwanza.
NCHI KWANZA........huo ndio uzalendo wa kweli.
Mimi ndo wale tunakomaa mpk.mwishoKwani wewe hujahamia burundi, au ulidharau tamko la mchumi mkuu daraja la kwanza.....
Hiyo 4:00 ifanye Iwe pmKitendo tu cha kusema 4:00 wataanza na sasa ni 4:32 kinanipa nafasi ya nini kinaenda kuzungumzwa
Uko mbali maroon walivyopigwa fimbo na kinga'iUkiona heshi linakusanya korosho ujue tumepigwa
Media ilisaidia Kenya kumwaga damu 2008, pia Rwanda na Burundi. Ndiyo maana West huwezi kuwa Journo hadi uwe na taaluma nyingine kwanza ili uandike news za taaluma yako tuuuuu kwasababu huko kuna check and balance toka kwa wanataaluma wenzako ambao ni nguli.Watanzania na Haswa Muhimili usio Rasmi yaani waandishi wa Habari/vyombo vya Habari vya Tanzania vinapaswa viwe na Uzalendo wa kuweka masilahi ya nchi yao Kwanza.
NCHI KWANZA........huo ndio uzalendo wa kweli.
NakaziaHamna jipya hapo
Ndugu yangu aliyeitisha Kikao ni mabeyo ama msemaji wa jeshi?haya mambo si yalipaswa yasemwe na wizara ya ulinzi na is jeshi lenyewe? huko nyuma yalikuwa yanasemwa na waziri wa ulinzi au ye yote kwa niaba yake, huyu mabeyo ameamua kufanya hivi kwa kuwa rais na waziri wa ulinzi ni wanawake?
Heri mimi sijasema.Jeshi linalalamika
Jeshi haliogopi tapeli yeyote ila inafanya hivi kwa faida ya vijana na wazazi wao wanaotaka kuandikishwa jeshi maana wanateseka sana na nafasi hizo na wengi hawafanikiwiJeshi limechanganyikiwa [emoji12][emoji12][emoji12] yaani jeshi letu kuu na mkwara wote ule kumbe linaogopa matapeli, hakika inasikitisha.
Bado naweza kuwa "mwaipaya" hata nikiwa na peni yangu mkononi.Wewe ndio hutaki kuwa "Mwaipaya" hahahaha Divide and rule!
Kwani Mtwara Kuna Nini?Nikajua wataongelea ishu za Mtwara huko.
Soma vizuri nilichoandika. nimeanza kwa kuangalia historia na mwenenndo wa jeshi huko nyuma. usiniletee mihemuko h=yako ya kumpenda mabeyoNdugu yangu aliyeitisha Kikao ni mabeyo ama msemaji wa jeshi?
Jeshi Lina msemaji wake na ndio huyo hapo kaitisha Kikao, hivi kati u wa wizara na msemaji wa jeshi yupi kauli yake ni rasmi zaidi kwenye kutoa maelezo ya kijeshi