Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Watanzania kama sio kukosa exposure basi ujinga unatutesa sana na kuna siku utakuja kutugharimu sana
Wiki iliyopita nilikuwa Dodoma nimeangalia namna ya Jiji la Dodoma lilivyopangwa na kusema kweli nimesikitika sana.
Hii nchi kuna siku yatatukuta ya Haiti wahuni wanaingia kwenye makazi ya Rais kufanya umafia na kutokomea bila hata kukamatwa alafu ndo tunakuja kuunda tume kujua tatizo kumbe hatushughulishi akili zetu kwa wakati sahihi.
Nani aliyesema Chamwino kwenye Ikulu pazungukwe na Makazi ya watu binafsi? Waliopendekeza hili hawakuona hatari yake?
Nani alipendekeza Mji wa Serikali ujengwe Mtumba na sio Chamwino?
Kwa sehemu nyingi duniani makazi ya Rais yanazungukwa na Ofisi Kuu za Serikali na hata makazi ya viongozi wa Kiserikali na sio watu binafsi. Kujenga mji wa Serikali sehemu tofauti alafu kuweka ikulu kwenye makazi ya watu hawakuona hili linaweza kuleta matatizo siku moja?
Kiuhalisia Mji wa Serikali na Makazi ya Viongozi wa Serikali vyote vilitakiwa kuwepo Chamwino na kuzungukwe na kambi za Jeshi ila kwa Dodoma haya hayajafanyika
La kunichekesha zaidi ni Jengo la Bunge. Hili Jengo lipo sehemu ya ajabu kabisa. Nje kuna vibanda vya chips na makazi holela. Inafika hadi wabunge wanakosa sehemu za kupaki magari na mwishowe kusababisha msongamano mkubwa sana kipindi cha Bunge.
Kusema kweli kwa watu wasio na akili wataifurahia Dodoma ila kwa wenye akili na wanaoona mbali Dodoma itakuja kuligharimu sana Taifa siku za mbeleni mbeleni!