Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,351
- 9,838
- Thread starter
- #61
Kwamba ukiwa na hisa ndogo, ukapata tenda kubwa huwezi kukopa ukadeliver?Inaelekea hujui hata unachotetea .
Hoja ni ukiukwaji wa utaratibu wa kutoa vibali vya uagizwaji wa sukari nje pindi kunapokuwa na uhaba wa sukari viwanda vinapositisha uzalishaji wa sukari.
Utaratibu huo upo na waziri bashe aliukiuka na hilo alikiri bungeni kwamba alilazimika kutokufuata utaratibu huo ili kuwaokoa wananchi baada ya sukari kuadimika.
Mpina ndio akaibuka na hoja zake kwamba waziri kadanganya na amekituka taratibu na kuboronga kabisa hadi kuzipa vibali kampuni za kijanja ambazo hazikuwa na sifa wala vigezo vya kuagiza sukari nje.
Hizo kampuni ambazo nyaraka zake brela zinaonyesha zina hisa ndogo zimetoa wapi fedha za kuagiza sukari za kiasi kikubwa hivyo kama sio hapo tayari kuna suala la utakatishaji wa fedha na ukwepaji wa kodi mkubwa sana umefanyika?
Yani mtu mwenye mtaji mdogo hapaswi kukua?