TUMESHINDWA KUMLINDA, WAMEMUUA BINTI YETU ASIMWE, WAMECHUKUA BAADHI YA VIUNGO VYAKE💔
Baada ya kupotea kwa siku kadhaa asijulikane alipo. Hatimae siku ya jana mwili wa binti huyo mdogo mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) kwa jina la Asimwe ulikutwa kichakani umeviringishwa kwenye fuko huku baadhi ya viungo vyake vya mwili vikiwa vimetolewa.
Wanadamu tumekosa utu, tusamehe binti yetu mzuri tumeshindwa kukulinda, tamaa ya madaraka, mafanikio ya haraka, imani potofu, vimeondoa uhai wako. Hatujui ulijiteteaje wakati wanakutoa uhai, ulikuwa unawatazama au walikufunga macho💔. Imeharibika dunia.