Updated List: Haya ndio makabila yenye wasomi zaidi Tanzania

Updated List: Haya ndio makabila yenye wasomi zaidi Tanzania

Endelea kucomment kwa adabu jf ukitegemea humu utapata connection [emoji1787][emoji1787]pana watu wazito BumbaaaaaaV!
Japo sina adabu connection kubwa kuliko zote kwenye maisha yangu nmepata humu humu jf , na bado naendelea kuchangia bila adabu .
 
Manyuzi yanajirudia inaonekana sasa hatuna jipya.
 
Kuna wasukuma 20m!?..
Je wana akili ya kulete maendeleo? Angalia mazingira yao wanayoishi vijijini, bahati mbaya nilipita Usukumani mwaka 1970 Dec nilipita karibu mkoa wote mpaka mkoa wa Musoma nikaishia Isbania na kurudi APRIL 1971. Maendeleo yalikua zero
 
Mkuu serious wanyakyusa wana uwezo kawaida???


Sijajua ila katika soma zangu sijawai kutana na Mnyakyusa mzembe darasani

Me mwenyewe sio utani isingekuwa kubebana chuo flan nilikuwa naondoka na best student 😃
 
Je wana akili ya kulete maendeleo? Angalia mazingira yao wanayoishi vijijini, bahati mbaya nilipita Usukumani mwaka 1970 Dec nilipita karibu mkoa wote mpaka mkoa wa Musoma nikaishia Isbania na kurudi APRIL 1971. Maendeleo yalikua zero
Kuzungumzia maendeleo ya jamii za kitanzania ya mwaka 1970 kulinganisha na 2024 lazima dish liwe limeyumba.
 
Mkuu usijizime data, nakukumbusha tu kwamba mkoa wa Kilimanjaro pamoja na eneo lake dogo ndio mkoa unaoongoza kwa shule nyingi zaidi nchini, na wanaofaulu kwenda vyuoni ni wengi pia,
Mkoa wa Kilimanjaro una shule nyingi za sekondari tu lakini hauna idadi kubwa ya wanafunzi. Kwa mfano mkoa wa Kagera unapeleka wanafunzi wengi Form six kuliko kilimanjaro alafu kilimanjaro wanasoma wanafunzi wengi kutoka mikoa(makabila) mengine hivo uwepo wa sekondari nyingi sio kigezo cha wachagga kwenda shule
 
Je wana akili ya kulete maendeleo? Angalia mazingira yao wanayoishi vijijini, bahati mbaya nilipita Usukumani mwaka 1970 Dec nilipita karibu mkoa wote mpaka mkoa wa Musoma nikaishia Isbania na kurudi APRIL 1971. Maendeleo yalikua zero
Wewe kwanza ahapo ulipo nakupa pole sana! Jamii zimeshachange sana tu! Njoo saizi utajionea mabadiliko ya kutosha kuanzia Shinyanga ,Kaham,Katoro, Mwanza ,Lamadi na maeneo mbali mba;li!

Miaka hiyo najua hata shule zilikuwepo chache na zilikuwa mjini tu! Kama unazungumzia maendeleo haya yaliyopo na maeneo mengine mbona hata Kanda ya ziwa yapo na hakuna tofauti!
 
Sahihi kabisa
Wanyakyusa tuko vizuri kielimu .....huku mbeya mtoto ukikataa shule .... wazazi wanakutimua nyumbani [emoji23][emoji23]

Pia Kwa vyuo vikuu na vile vyakati mbeya vinafika Hadi 20..

But Kwa wachaga na wahaya Kwa elimu hawa watu wanaheshima yao
 
Umesahau
Tabora,
Katavi,
Rukwa,
Morogoro,
Mbeya


Wamesambaa karibu kila kona ya nchi leta hiyo taarifa yako ya sensa.

Wasukuma ndio kabila kubwa Tanzania.

Hawafiki milioni ishirini. Kusambaa hata wachaga, waha, Masai wamesambaa sana.
 
Nasikitika makabila yenye akili elimu ilichelewa kwao lakini, elimu imewahi kwa makabila yenye vilaza wengi ndiyo maana hadi leo hatuna gunduzi za kitanzania zinazo eleweka zaidi ya ubinafsi na majigambo. Nchi inaimaskini wa kunuka.
 
1. Wachaga - Kama kawaida yao sio watu wa kujisifia iwe ni biashara, maendeleo ya vijini kwao, n.k. Kiufupi hawa suala la elimu wapo Mbali tangu enzi za ukoloni, Mkoa wa Kilimanjaro ni mdogo ila ndio unaongoza kwa shule nyingi hasa maeneo ya uchagani, Kitu cha ziada ambacho wengi hawakijui ni kwamba wana mwamko wa shule za kimataifa na hata miji wanayoishi ya Moshi na Arusha kuna shule hizi nyingi kama St Constatine, Braeburn, INternational school of Moshi, Kennedy house, n.k. Kwenye shule hizi watoto utaowakuta kutoka Tz ni wachache ila majority huwa ni wachaga, sio suala la mzazi kuwa na pesa pekee bali na mwamko wa kuwapa watoto elimu ya kimataifa, na hata zile nafasi za udhamini watanzania kusoma bure huwa ni watoto wa kichaga. Ikumbukwe shule hizi ni tofauti kabisa na hizi za Necta, huku ukisoma kuna guarantee kubwa kusoma vyuo bora duniani, Luhgha za wazungu walimu ni wazungu, connections nzito za watoto wa wazito, n.k.

2. Wahaya - Yes, Ni nani asiewajua watu hawa waliowekewa kizuizi na Nyerere kwa alama za kufaulu darasa la saba ? Hawa watu wanaipenda shule jamani, Shida ni kwamba kuna changamoto za kiuchumi mkoani Kagera, wapo wengi wanaotamanigi kuendelea na shule na uwezo upo ila inawalazimu waendelee na maisha mengine, halafu pia wao na makabila mengine wana mwamko mdogo sana na International schools, Mhaya mwenye pesa za kutosha atapeleka mtoto wake Kaizarage ya Bukoba ama saint Francis huko Mbeya yani hana mwamko kabisa kujua kwamba kuna shule International.

3. Wanyakyusa - Ughonile, Nimeishi nao so nawajua vizuri hawa kina Mwakyusa, Mwakatobe, Mwakyembe, Bukuku, n.k., wazazi wa kinyakyusa hasa wamama wanaasa sana watoto wasome, wapo tayari kujinyima kwa lolote mtoto asome shule nzuri, Nakumbuka nikiwa Mbeya mtu anaweza kuresit form 4 hata mara 3 kutafuta credit, hawana jambo dogo kwenye elimu !! kuhusu uwezo darasani wanao wa kawaida ila wapo wachache nishawai kutana nao ni ma genius, Kwa sasa Mbeya ndio mkoa inaoongoza kwa vyuo ukiitoa Dsm, Kuba shule za kiingereza 4 za serikali za msingi, Shule za Sekondari zipo nyingi

4. Wasukuma - wasukuma wapo wengi sana hii nchi ila tatizo maeneo yao mengi hawaipi elimu kipaumbele, mikoa waliyojazana wasukuma kama Simiyu, Geita, Shinyanga, n.k elimu haipewi uzito na shule ni chache, Mwanza ndio inawabeba.... Laiti wasukuma wangejiongeza kielimu lingekuwa ni tishio kubwa sana hapa nchini maana katika kila watanzania sita kuna msukuma moja, Huenda mkoloni hakupeleka elimu usukumani alishaona watadominate sana, na pia licha ya Mwanza kuwa jiji la pili kwa ukubwa Tz hawana chuo kikuu.

5. Wakerewe - wakerewe wapo katika kisiwa kidogo cha Ukerewe, kwa mipaka ya ramani kipo mkoa wa Mwanza lakini kiuhalisia kipo mkoa wa Mara, wakerewe ndio wanaongoza nchi nzima kwa kuwa na maprofesa wengi zaidi wenye phd za kutafuta darasani, Sababu ya kuwa namba tano ni idadi yao (population) kuwa ndogo.

Bonus....

Watu wa Mara - sijajua ni kabila lipi kati ya wajita, wakurya, wajaluo au wazanaki lakini nimesoma vyanzo mbali mbali kwamba mkoa huu ni kinara wa kutoa wasomi wengi, Majimbo kama Musoma vijijini ule mchujo tu wa kupata mbunge wa kupitishwa ni phd tupu.


Makabila mengine ni Wapare, wamasai wa Meru, Wamatengo wa Ruvuma, n.k.
Ni uchambuzi wenye ukweli mkubwa sana ila usisahau kuwa Morogoro ina vyuo vikuu vingi na vikubwa; SUA, Mzumbe, Jordan, Muslim University, etc, Pengine K’Njaro inafuatia.

Pia ujue hakuna watu waliominywa kwenye elimu enzi za Nyerere kama Wachagga. Hawakuachwa wafaulu waende shule za serikali ila walijiongeza na kuwa na shule nyingi za mashirika ya dini na hata kwenda Kenya kusoma pindi Nyerere alipowadhibiti.

Mwisho wa siku walishinda siasa za kimaskini za Nyerere na Nyerere aliwaogopa mno!
 
Mkoa wa Kilimanjaro una shule nyingi za sekondari tu lakini hauna idadi kubwa ya wanafunzi. Kwa mfano mkoa wa Kagera unapeleka wanafunzi wengi Form six kuliko kilimanjaro alafu kilimanjaro wanasoma wanafunzi wengi kutoka mikoa(makabila) mengine hivo uwepo wa sekondari nyingi sio kigezo cha wachagga kwenda shule
Ni kweli flani; zaidi ya 80% ya wachagga wapo nje ya K’Njaro na watoto wengi wa huko husoma nje ya mkoa.

Vijana wengi sana K’Njaro wameenda shule ndio maana siku hizi kupata vibarua au wafanyakazi Moshi ni ngumu sana na huagizwa mikoa mingine.

Lazima kitu kifanyike kurudisha population kule K’Njaro la sivyo mkoa utakufa!
 
Wandengereko, wazaramo na the like wapo busy kukata mauno na kushikana uchawi

Hatuna stress watu wa Pwani. Nyie ibeni halafu tupeni sisi hizo hela zenu za Wizi tuwajengee Mahekalu yenu. Sie tukiwa tuna Kuku 10 Bandani wewe una Ng’ombe 10 zizini tunakuona fala tu. Ndio maana mmekuja mjini tumewauzia nyumba zetu za Magomeni, Kariakoo, Ilala halafu sisi haoo Mbagala na Chanika. Tukisoma sote nani atamtuma mwenzie?
 
Na wewe labda pia hukuinielewa vizuri. Hizo sources za data nilizotoa ndiyo statistical representation nzuri ya distribution ya wasomi; siyo kuwa wasomi wote wanafanya kazi hizo, wengine huenda wana digrii zao lakini wanafanya shughuli zisizohusiana kabsa na digrii zao kwa mfano wanauza madini au ni wakulima au wqana maduka yao, lakini distribution nzuri ya wasomi itaonyeshwa na presense yao katika fields hizo nilzosema.

Idadi ya shule za sekondari Kilimanjaro ilikuwa kipimo kizuri zamani lakini siyo siku hizi. Angalia jinsi nchi nzima ilivyo na shule za sekodari, kanda ya ziwa siku hizi ina shule nyingi sana leo.

View attachment 2860576
Nimekuelewa vizuri. Sasa, uwe objectively verifiable. Nilidhani kusudio lako la kumpinga,usingedhani tena kama yeye, ungeweka data kwa kutumia cluster groups ulizotaja. Ukija na data unanishawishi. Niambie kwa kutumia statistcs za Wizara ya Elimu,ni Mkoa gani hapa nchini unaongoza kwa kuwa na shule nyingi za sekondari?
 
Back
Top Bottom