UPDATES: Madhara ya mvua iliyonyesha jijini Dar - Desemba 17, 2019

Hahaha niliwahi kusikia, serikali awamu ya tano ilimaliza hizi kero, kumbe bado kama enzi za Nyerere tu a.k.a awamu ya kwanza.
 
me mwenyewe nimoja Kati ya wahanga wa hii mvua aisee yaani imeshanirudisha nyuma kwanamna moja ama nyingine
 
Nawaza kwa sauti kama Mkoloni angeendelea kututawala basi pale jangwani angeshajenga daraja, ila serikali ya ccm tangu imeingia madarakani wanapatazama tu pale hawachukui hatua sijui wanatuchukuliaje watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukienda Mwanza kipindi cha mvua hautamaliza wiki unapakimbia. Kule radi zinaua, zinatoboa mabati na kupasua miti. Radi ikipita mahali utafikiri jogoo kaparua.
Hiyo itakuwa ni Mwanza ya Malawi ila Mwanza ya Tz haiko hivyo ulivyoielezea, ki ujumla ukanda wa ziwa Victoria radi ni jambo la kawaida, mara nyingi radi ina strike eneo la ziwa sio kwenye makazi ya watu ikitokea hivyo ni nadra sana labda tuseme mara moja baada ya muongo, na sehemu inayoongoza kwa radi ukanda huu ni Kampala ila huku Mwanza radi ni za kawaida sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…