Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Nimechukia kuona amepata kura hata hizo 5200. Huyu alistahili kupata kura 15 tuu kutoka familia yake, hii inaonyesha bado kuna watu hawaelewi nini kinaendelea hapa nchini.

kabisa!
 
Asanteni kwa kutuondolea pumba moja! Nakumbuka siku alijaribu kutaka kubishana na Lissu bungeni! Wakora wana Nkenge.👍👍👌
 
Yuko na Mwapachu. Mzee Kingunge of course atakuwa na watu wake. Lakini si unajua mambo ya masila eventually kila mtu ataangalia ana-benefit wapi?
Msema kweli Oct 25th, 2015
 
Kama kuna watu alikuwa anawategemea sana Lowasa katika mikakati yake basi ni pamoja na huyu Hussein Bashe. Bashe ni miongoni mwa makada wa CCM ambao walitajwa kuhamia CHADEMA kumfuata bosi wao Lowasa. Pia alikuwepo Mussa Zungu, Kangi Lugola, Christopher Ole Sendeka nk. Ushindi wa makada hawa hakika ni pigo kubwa sana kwa Lowasa. Sidhani kama kuna dalili za yale Mafuriko ya makada wa CCM kukimbilia CHADEMA. Mpaka sasa, katika watu wake wa karibu, ni mkewe tu ndiye aliyeenda CHADEMA.

Na bado

Lowasa ana hela lakini watu hana.Nilishangaa MBowe aliposema eti lowasa atawaleta wanaCCM mamilioni kuhamia CHADEMA.Lowasa ana watu CCM kawatoa wapi? Akina mbowe jiandaeni hao hao mlionao ndio atakaowatumia yeye kaja mweupe hana wafuasi huyo ana wapenzi tu wa muda kutegemea na hela alizowamwagia.Mtu mwenye watu CHADEMA ni SLAA SIO MBOWE na CUF ni SEIF sio Lipumba.

Lowasa mliyemchukua CHADEMA mmechukua mtu asiyekuwa na watu huyo alikuwa anategemea wana CCM wenye watu wampe na wamsaidie kampeni.Mbowe sababu hana watu hawezi mbeba Lowasa.Ni wajanja wawili wasio na watu wanaoviziana Mbowe akidhani Lowasa ana watu na Lowasa akivizia na kudhani mbowe ana watu.Wamekutana wajanja wa mjini wawili wasiokuwa na watu.CHADEMA itagaragazwa safari hii uchaguzi mkuu hadi basi.Matokeo ya safari yatakuwa ya aibu kwa CHADEMA mark my words.
 
Huyo mmama amegawa sana hela..Mtaani jana ilikuwa ni sherehe

Ni kweli, nimesikia kwa mmoja wa Katibu wa CCM tawi, anasema habari za pesa na tena kuna mama alikuwa anamsikitia kwa kukosa nafasi ijapokuwa aligawa pesa nyingi sana.

Zaidi, huyu Katibu wa tawi anasema huyo Mama aliyependekezwa na CCM ameapa kutokumwacha kwakuwa alimfanyia kazi kubwa ya kupata ushindi.....hawa CCM ni hatari for they use alot of money to secure posts.

Makongoro ameshindwa kwasababu walimchoka na dharau zake but pesa naye kamwaga sana.

Nikitoka huku ndani nitaongea na huyo Mama (Katibu) and, I know, she will explain everything to me what happened yesterday.

Ofisi za tawi CCM zipo nyumbani kwetu lkn mimi sikuwepo jana wakati wanafanya uchaguzi.
 
...yaani ccm tumewazidi maarifa mpaka aibu, shangilieni baadae mtatuelewa...
 
Ningekuwa mwana ccm ningepatwa na hofu sana wafuasi kindakindaki wa EL kubaki ccm na kuwa kwenye vyombo nyeti vya maamuzi.

Mfano Nchimbi, Kimbisa et al. Kama unajua siasa utakuwa umenielewa

Furahia Bashe kushinda kura za maoni kwa sasa

Mkuu umenena coz huwezi kujua nn kitafuata baada ya matokeo hayo.Ninaamini kuna jambo litakuja na litawaacha wengi midomo wazi.
 
WANAOONGOZA KURA ZA MAONI MAJIMBONI MPAKA SASA:
1. Mwigulu - Iramba
2. Nape - Mtama
3. Mwakasaka - Tabora Mjini
4. Mama Sitta - Urambo
5. Kadutu - Ulyankulu
6. Bashe - Nzega
7. Ngeleja - Sengerema
8. Seif - Igunga ktk jimbo jipya.
9. Masaburi - Ubungo
10. Patel - Ukonga
11. Prof Kamala - Nkenge, Misenyi
12. Kagasheki -
13. Lukuvi - Isimani
14. January - Bumbuli
15. Muhongo - Musoma vijijini
16. Ndugai - Kongwa
17. Chumi - Mafinga
18. Kigola - Mufindi kusini
19. Mgimwa - Mufindi kaskazini
20. Filikunjombe - Ludewa
21. Mgimwa - Kalenga...
22. Lusinde - Mtera
23. Imani Moshi - Kaliua bado kata 2

Ni lini alipata uprof na instituion gani ilimpa u prof?
 
Ningekuwa mwana ccm ningepatwa na hofu sana wafuasi kindakindaki wa EL kubaki ccm na kuwa kwenye vyombo nyeti vya maamuzi.

Mfano Nchimbi, Kimbisa et al. Kama unajua siasa utakuwa umenielewa

Furahia Bashe kushinda kura za maoni kwa sasa

Kama babayao mamvi alikuwepo na bado watu wakafanya maamuzi sahihi huku wakimuangalia usoni, hawa viroboto hawawezi wataishia kumzidishia pressure tu huyu mzee wa watu
 
Lowasa ana hela lakini watu hana.Nilishangaa MBowe aliposema eti lowasa atawaleta wanaCCM mamilioni kuhamia CHADEMA.Lowasa ana watu CCM kawatoa wapi? Akina mbowe jiandaeni hao hao mlionao ndio atakaowatumia yeye kaja mweupe hana wafuasi huyo ana wapenzi tu wa muda kutegemea na hela alizowamwagia.Mtu mwenye watu CHADEMA ni SLAA SIO MBOWE na CUF ni SEIF sio Lipumba.

Lowasa mliyemchukua CHADEMA mmechukua mtu asiyekuwa na watu huyo alikuwa anategemea wana CCM wenye watu wampe na wamsaidie kampeni.Mbowe sababu hana watu hawezi mbeba Lowasa.Ni wajanja wawili wasio na watu wanaoviziana Mbowe akidhani Lowasa ana watu na Lowasa akivizia na kudhani mbowe ana watu.Wamekutana wajanja wa mjini wawili wasiokuwa na watu.CHADEMA itagaragazwa safari hii uchaguzi mkuu hadi basi.Matokeo ya safari yatakuwa ya aibu kwa CHADEMA mark my words.

Yaani wewe unahangaika na EL ..au alikuwa bwanako zamani sasa kakuacha ?
 
Ole Sendeka wala hakuwa swahiba wake. Juzi nusura wampige kwenye kampeni baadaya kusema Lowassa didimia.
 
Back
Top Bottom