Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

The best thing CCM has to do ni kumrushia Lowassa hayo makopo yake aende nayo ili asiwasumbue baadae.
 

Hujui siasa..... Wala hujui mipango iliyopo, ni vyema ukae kimya....

Na ni tokea lini Ole Sendeka alikuwa kambi ya Lowassa?
 
Hizi ni habari njema, yale mafisadi ktk mfumo yabaki huko huko!
 
Ningekuwa mwana ccm ningepatwa na hofu sana wafuasi kindakindaki wa EL kubaki ccm na kuwa kwenye vyombo nyeti vya maamuzi.

Mfano Nchimbi, Kimbisa et al. Kama unajua siasa utakuwa umenielewa

Furahia Bashe kushinda kura za maoni kwa sasa

Huyu Hot Lady hajui siasa kabisa...... Kwa taarifa yake hii ni vita ya ndani na nje..... Huwezi kuangusha dola kwa vita ya nje tu.....
 
Duh mtoa uzi ww siasa haujiui ni bora utulie tu topic ya kitoto sana
 
Wadau nimejaribu kufuatilia uchaguzi za CCM uliofanyika jana. Kila kona kila sehemu kumukuwa na malalamiko ya uchakachuaji wa kura. Kwa mfano wagombea wengine wamekuwa wakigawa rushwa, kuwa na card feki za kupigia kura au kuwa na karatasi ambazo tayari zinaalama ya ndio kwa mgombea. Nimejiuliza maswali mengi sana kama CCM wenyewe kwa wenyewe wanataka kufungana na bao la mkono..? Je uchaguzi wa rais utakuwaje..? Hapo naona bila ubishi bao la mkono limeshafungwa..! Au wadau mnaonaje..?
Mfano eneo la Tabata, kuna mgombea anaonyesha kushinda kwa zaidi ya idadi ya watu waliopiga kura katika kata moja. Nasikia alikuwa na card za kumwaga anagawia watu na sh 10,000 ukampigie kura. Mtu unaitwa John unatumia card imeandikwa Salehe na unapiga kura bila kugundulika. Nasikia huyu Diwani aliyekuwa anatetea kiti chake alisashukua card za kumwaga miaka ya nyuma akaziweka kabatini kuisubiri siku ya jana.Inasikisha sanaaaaaaaa isee..!
Hivi kweli CCM haijui jinsi ya kuweka rekodi za wanachama wake ktk kila kata..? Hii inadhihirisha system mbovu. Au wadau mnaoaje...?
Pia kama kuna mdau mwenye matokeo ya Wasira na Ndungai atulushie..
 
hizi idadi za wapiga kura za maoni CCM hazina uhalisia wowote
 

Umeongea kishabiki mnooo mi ni mzaliwa wa nzega power ya ukawa sasa naitambua wala hilo halitishi ilibidi mshtuke nyie magamba kwann mshirika wa karibu wa lowassa kabaki huko anania gani kumbuka mlimfanyia umafia2010 je sasa anafikiria nini???? Unasema lowasaa hana watu kwahyo wale wa monduli, 4umovement, friends of lowassa, wale wa musoma waliogoma kujiandikisha kisa lowassa we huwaoni??? Nikupe taarifa makao makuu ya chadema kadi za uanachama zimeisha coz wiki hii wamepokea wanachama wengi mnoo je hao wamefata nini???? Ninawasiwasi nawe unaposema lipumba hana watu we unaendeshwa na mahaba ya magamba ongea ukweli ndugu
 

hizo idadi ya kura za maoni CCM hazina uhalisia
 
WanaCCM wanajifariji sana, wameumia sana Lowassa kuhamia CHADEMA walidhani hawezi kufanya hivyo, jamaa akafanya maamuzi magumu.
Vibaraka wa Lowassa waliopo CCM ni hatari zaidi kwa CCM kuendelea kuwakumbatia maana watasumbua tu ndani ya CCM.
Huo ni mchuzi wa samaki tu, samaki mwenyewe yuko UKAWA, kama CCM hawataki shombo ya Samaki, basi na mchuzi waumwage basi.
 
Wale watuhumiwa 4 wa escrow Chenge, Muhongo, Ngeleja na Tibaijuka wameshinda kwa kishindo kura za maoni kule CCM. Wanaccm waliopiga kura za maoni wamedharau adhabu walizopewa wagombea hao na uongozi wa juu wa chama. Lakini ukweli unabaki palepale hawa ni WATUHUMIWA tu kama alivyo Nape pale Takukuru Lindi!
 

Lowasa ataendelea kuwa hatari kwa CCM daima.Tena hao waliobaki CCM ndo hatari zaidi.Jamaa atakuwa na mtandao ndani na nje ya CCM na CDM
 
Mpaka muda huu sijapata matokeo ya Kura za maoni juu ya mama Anna Tibaijuka ila nasikia anapumulia mashine ,mwenzake Prof muhongo amepita kwa kishindo na bila shaka atarudi bungeni please please itakuwa ni matusi kama atarudi kwa kupitia jimbo,
 
Wataopiga kura ni milioni 6 ya wote waliojiandikisha, wengine walitaka vitambulisho tuu, pia kuna kura za kuharibika hapo! Hivyo kama wana milioni 3 tayari do the maths!
 
KURA ZA MAONI CCM
1. Mwigulu - Iramba

2. Nape - Mtama

3. Mwakasaka - Tabora Mjini

4. Mama Sitta - Urambo

5. Kadutu - Ulyankulu

6. Bashe - Nzega

7. Ngeleja - Sengerema

8. Seif - Igunga ktk jimbo jipya.

9. Masaburi - Ubungo

10. Patel - Ukonga

11. Prof Kamala - Nkenge, Misenyi

12. Kagasheki - Bukoba mjini

13. Lukuvi - Isimani

14. January - Bumbuli

15. Muhongo - Musoma vijijini

16. Ndugai - Kongwa

17. Chumi - Mafinga

18. Kigola - Mufindi kusini

19. Mgimwa - Mufindi kaskazini

20. Filikunjombe - Ludewa

21. Mgimwa - Kalenga...

22. Lusinde - Mtera

23. Imani Moshi - Kaliua

24.Mwakasaka -Tabora mjini

25.Fenala Mkangara -Kibamba

26.Mapunda-Mbinga mjini

27.Masele -Kahama

28.Antony Mavunde-Dodoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…