Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

CCM Kiteto kimenuka mdogo wake Nangoro anusurika kuuawa ofisini aokolewa na viongozi wa CCM, ni baada ya kuingia ndani ya ofisi za CCM wanachama wahofu kuwa aliyenda kutoa rushwa
Katibu CCM alonga adai alitumwa na kaka yake Mbunge Nagoro kuja kuchukuwa matokeo
Wanachama wadai mpaka kieleweke..polisi watanda na silaha kali za moto
 
CCM ukiwa na mkwanja lazima ushinde hata kama unawatukana wapiga kura wako, watakupa tu sababu ya njaa, huku waligawa kadi za chama bure kwa kila mtu alafu wanakupa hela ili uende kupiga kura.
 
Cdm wajihadhari wasipokee kila mtu. Huyu na Makongoro Mahanga sina imani nao

Mkuu unaongea ukweli ila hawa wakija CDM wanakuwa wanachama kama mm ma wewe tuu, so hawana effect, cha kuzingatia wacpewe nafasi za juu kama watabahatika.
 
Matokeo Jimbo Tabora Kaskazini 1.ALMAS A. MAIGE 9000+,2.SHAFF SUMA 6000+,3.JOSEPH KIDAHA 5000+ jumla ya wagombea ilikuwa 10
 
Huyu mzee ni wa kwetu kabisaaaa sema roho wa upako bado haja mkolea vyema ila Mungu anafanya makusudi tumpate..akija najua kwa yale maneno yake akiwa kampeni shughuli ya ccm itakuwa pevu saaana
 
Cdm wajihadhari wasipokee kila mtu. Huyu na Makongoro Mahanga sina imani nao
Hivi huyo Makongoro Mahanga si ndiye yeye kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alimfunga Fred Mpendazoe wa Chadema 'goli' la mkono kwa kukimbia na masanduku ya kura baada ya kugundua amieshindwa uchaguzi huo?

Itabidi Chadema sasa wawe makini sana na watu wa design kama ya Makongoro ambao wanataka kuja Chadema baada ya kupigwa chini kwenye kura ya maoni kwenye chama chao cha magamba.

Watu wa design hiyo kama kweli watakuwa na mapenzi ya kweli na Chadema basi wakubali kupokelewa lakini siyo kwa wao kutoa masharti ya kuingia CDM kwa kupewa fursa ya kugombea Ubunge, bali waanze kwanza kuwa wanachama wa kawaida.
 
Cdm wajihadhari wasipokee kila mtu. Huyu na Makongoro Mahanga sina imani nao

Makongoro mahanga alichuja siku nyingi na aliwahi iba kura za mpendazoe. Leo ni zamu take yeye aingie tu kuwa mwanachama wa kawaida asitegemee ubunge kupitia CDM. Kama ni kugombea ubunge aende TLP
 
Matokeo mbinga mjini bado kizungumkuti. source moja ya diwani aliyeshinda kura za maoni.
 
Hivi huyo Makongoro Mahanga si ndiye yeye kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alimfunga Fred Mpendazoe wa Chadema 'goli' la mkono kwa kukimbia na masanduku ya kura baada ya kugundua amieshindwa uchaguzi huo?

Itabidi Chadema sasa wawe makini sana na watu wa design kama ya Makongoro ambao wanataka kuja Chadema baada ya kupigwa chini kwenye kura ya maoni kwenye chama chao cha magamba.

Watu wa design hiyo kama kweli watakuwa na mapenzi ya kweli na Chadema basi wakubali kupokelewa lakini siyo kwa wao kutoa masharti ya kuingia CDM kwa kupewa fursa ya kugombea Ubunge, bali waanze kwanza kuwa wanachama wa kawaida.

Nakubaliana na wewe sana kiongozi. Na ndo maana Dr.Slaa haonekani yeye pamoja na wataalam wenzake watakuwa wamejichimbia mahali fulani wakiwa na darubini zao wakichunguza kila mmoja anayejiunga na chama. Wanafanya veting ya siri kwa kila anayejiunga. Wanaanda kambi ya wakimbizi
 
sam_4512.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Monaban ya jijini Arusha, Philemon Mollel ambaye pia ni Mgombea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM akimwaga sera zake.​
 
Back
Top Bottom