Hivi huyo Makongoro Mahanga si ndiye yeye kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alimfunga Fred Mpendazoe wa Chadema 'goli' la mkono kwa kukimbia na masanduku ya kura baada ya kugundua amieshindwa uchaguzi huo?
Itabidi Chadema sasa wawe makini sana na watu wa design kama ya Makongoro ambao wanataka kuja Chadema baada ya kupigwa chini kwenye kura ya maoni kwenye chama chao cha magamba.
Watu wa design hiyo kama kweli watakuwa na mapenzi ya kweli na Chadema basi wakubali kupokelewa lakini siyo kwa wao kutoa masharti ya kuingia CDM kwa kupewa fursa ya kugombea Ubunge, bali waanze kwanza kuwa wanachama wa kawaida.