UPDATES: Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva | Mlimani City | 10.07.2026

UPDATES: Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva | Mlimani City | 10.07.2026

Saida
Amezeeka
Hakati Tena Yale mauno yake
 

Attachments

  • PXL_20260710_215900992.PORTRAIT.jpg
    PXL_20260710_215900992.PORTRAIT.jpg
    1 MB · Views: 12
  • PXL_20260710_215855857.PORTRAIT.jpg
    PXL_20260710_215855857.PORTRAIT.jpg
    984.9 KB · Views: 12
Natamani hata kulia oyaa maisha ni nyakati zikipita baaasiii
Acha tu Mzee. Kila kinachotokea kwenye maisha yetu kinabaki kua historia hakuna kinachojirudia Mzee. Inaumiza ila ndo ukweli tunatakiwa kuukubali. Enzi hizo tunasoma hatuna majukumu tunafrahia tu maisha huenda nyakati za huzuni na mahangaiko zilikua chache kuliko zile za fraha kwasababu kila angle kulikua na watu wanaturahisishia baadhi ya mambo, wazazi na ndugu wengine. Leo hii wengi tuna majukumu binafsi na ya familia, lakini pia tumepoteza wenzetu wengi sana ambao labda tulipaswa kushare nao moments tofauti tofauti za nyakati hizi kama hii show ya leo, hawapo Mzee. Tumshukuru Mungu kwa kila jambo na tuendelee kuamini kila kitu kitapita tu. Frahia nyakati za uhai wako Mzee ipo siku nasi tutakumbukwa kama wengine. Mimi leo naangalia hii show kupitia YouTube channel sipo Dar, sipo Tz niko mbali na nyumbani ila fresh nafrahia na kukumbuka nyakati zang, that's life Men... let's enjoy!!!
 
Back
Top Bottom