UPDATES: Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva | Mlimani City | 10.07.2026

Hadi sasa wasanii wazima wa sauti ni
Banana Zorro
Joslin
Kassim Mganga
Mwana FA
AY
Gk


Wengine wote Chali..sauti hakuna.
Hamna msanii ameimba vibaya kama Tundaman.. yaani tunda jamani kaimba hovyo kuliko wengine wote.
Tumuongeze Domokaya
Stara kidogo japo anahema sana
Hafsa
 
Kweli mzee tumshukuru mungu
 
Watu wengi wanawalaumu wasanii sijui sauti sijui pumzi,..wazee hawa wasanii wetu wa zamani sio kama wa mbele. Mbele wasanii wa zamani bado wanaendelea kua kwenye industry ya sanaa maisha yao yote na mifumo inawabeba kwa kiasi kikubwa wananufaika na kile walifanya zamani. Kwetu ni tofauti sana. Mifumo haikua vizuri so walipata hela enzi hizo na zilipokata tu walizopata walipokua kwenye peak zao basii waliondoka kwenye industry mazima. Wengine waliingia kwenye maisha mengine kabsa. So leo ukiwaleta hapa usotegemee watakua na nguvu na uwezo kama zamani. Lakini pia % kubwa umri na majukumu pia. Tuwashukuru kwa hiki walichotupa leo na tuwaombee kwa Mungu wawe na afya njema na shughuli wanazofanya kwa sasa ziwape kipato cha kuwasaidia kumudu maisha yao. Kadri umri unavyozidi kusogea nguvu, uwezo na maarifa ya utafutaji inapungua. Hata Mimi kuna muda naona kabsa ile thinking capacity ya miaka 10 ilopita sio sawa na leo na kazi yangu sio manual ni ya kufikiria tu na ku-act&react, translating mindset into real& tangible results
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…