Upendo Nkone: Mayai ya kisasa yanaongeza matiti kwa wanaume

Tatizo sio vita shida inakuja huyo upendo kasema hivyo akiwa kama nani kwenye sekta ya afya ,kwa sababu zipo sababu nyingine za matiti nyingine ni changamoto kubwa kabisa za kiafya , hauoni akisema ni mayai tu ni uposhaji mkubwa?
Kasema kama mdau wa afya, hata mimi nikishauri kuhusu jambo la kiafya kuna shida?
 
Pia mara nyingi na akiri zao zinakua na mfanano kabisaaa na makuku wakisasa.

NB: Eti sigara pia zinasababisha uotaji wa ndevu mapema, kwa wanaotumia chini ya umri wakuota ndevu.
 
Mavyakula na mavinywaji karibu yote tu siku hizi ni sumu.
Kwanini yeye kaamua kuchagua mayai ya kisasa?
 
Haya mayai huwa tunayatandika sana kwenye sherehe zetu, labda sie tumekomaa hatuwezi kuota matiti ukubwani
 
Aliyaona wapi hayo manyonyo ya watoto wa kiume waliokula mayai ya kisasa?
 
Kasema kama mdau wa afya, hata mimi nikishauri kuhusu jambo la kiafya kuna shida?
Ipo shida hasa kwa jamii inayofuata mkumbo tu kama ya kwetu, kuna mdau mmoja alishakuja yeye alikua mjamzito , shida yake ilikua kubwa ilihitaji upasuaji akadai haiwezekani kisa kuna nabii mmoja mkubwa kamwambia mara hii hata jifungua kwa operation, mwisho wa siku tulimpoteza mama mtu.

Ndio maana mimi napinga , eti upendo mkono wa nyimbo za injili🚮
 
Basi wazungu wote wangekuwa na matiti km matikiti maana wao toka kuzaliwa hadi kuufa ni mwendo wa mayai ya kisasa tu.
 
Mbona jambo alilolisema hata halihusiani kabisa na injili mkuu ni jambo la kawaida sana kwenye maisha.
 
Ana taaluma yoyote kuhusu masuala ya afya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…