Upendo Nkone: Mayai ya kisasa yanaongeza matiti kwa wanaume

Upendo Nkone: Mayai ya kisasa yanaongeza matiti kwa wanaume

Muimbaji wa nyimbo za Injili, Upendo Nkone, ametoa angalizo kwa wazazi kuhusu ulaji wa mayai ya kuku wa kisasa kwa kudai kuwa yanaongeza ukuaji wa matiti kwa watoto wa kiume.

Muimbaji huyo aliandika ujumbe huo kupitia akaunti yake ya Instagram akisema..''Jamani wazazi natoa ushauri tuu kwamba, tusiruhusu watoto wa kiume kula mayai ya kisasa, yanaleta manyonyo kwa wanaume. Hayo madawa nadhani yanayotumika, kama ni chips kula kavu au ule tuu mayai ya kienyejii, wanaume hili ni la muhimu sana"

Alimalizia kwa kusema "ila mnisamehe kama nitakuwa nimekosea au nimewaudhii️. Waachieni wanawake wale japo kwa kiasi pia. Nashindwa namna ya kuliwasilisha vizuri hilii ila mnisamehe wanaume''

Chanzo: Gazeti la Pambazuko.
Mkorogo kaacha? Au haijapata madhara bado?
 
Yani yeye kuimba nyimbo za injili amethibitisha vipi kila mtu akila mayai ya kisasa ataota matiti na sio sababu nyingine tu
Kwa alilolisema lipo na tunaona athari ya ulaji wa hayo mayai mkuu japo inaweza isiwe hivyo kwa kila mlaji ila yana athari.
 
Hata mwanaume kula chips mi huwa naona sio sawa,hua naona chips ni chakula cha wanawake
 
Kwa alilolisema lipo na tunaona athari ya ulaji wa hayo mayai mkuu japo inaweza isiwe hivyo kwa kila mlaji ila yana athari.
Kushauri mambo nyeti kama hayo tena kama wewe ni mtu maarufu na sio mtaalamu wa hayo mambo inaweza leta madhara makubwa hasa kwa jamii zetu ambazo kwao kufuatilia jambo ni ngumu.

Inawezekana ukakuta mtu anatumia dawa za saratani au anatatizo kubwa jingine lililopelekea hivyo ila yeye akafikiri ni mayai kutoka kwa mtaalamu wake upendo mkono.
 
Mkuu unatumia hayo mayai ya kisasa?

Kama jibu ni ndiyo basi pokea huu ushauri wa mhubiri wa Injili kwa njia ya uimbaji na uufanyie kazi kwa faida yako na wanao wa kiume
kwanini wanawake huwa mnadanganyika kirahisi sana na hao mnaowaita wahubiri, wachungaji, manabii n.k?

Ndio maana sisi wengine huwa hatuwashirikishi wake zetu kwenye ufanyaji wa maamuzi muhimu ya kifamilia. Tunaishia kuambiwa ni madikteta hatuheshimu wanawake ila sababu ni kwamba huwa mnaendeshwa na miemko tu bila kufanya utafiti wala kutumia logic

Screenshot_20250331_131304_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom