Pre GE2025 Upepo wa kisiasa unavuma upinzani, je hii ni ishara njema kwa chama tawala kuelekea 2025?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,158
Reaction score
7,787
Ukweli ni kwamba kwa sasa upepo wa siasa unavuma CHADEMA, macho na masikio ya wengi yameelekea huko.

Chama tawala ni kama wamesahaulika kwa muda, je hii ni ishara njema kwao kuelekea 2025?

Nini sababu ya chama tawala kupoteza ushawishi katika kipindi hiki kifupi? Je ni mbinu hafifu za kisiasa ambazo zinatekelezwa na viongozi wao?

Nadhani baadhi yao tayari wamepata maono kwamba hali ikiendelea kuwa hivi 2025 wataumia vibaya, endapo CHADEMA wakipata uongozi mpya hali itakuwa mbaya zaidi kwa upande wao.

Suluhisho la haya ni lipi? Je watafute mgombea/mwenyekiti mwingine kuokoa jahazi au waendelee kuwafunga midomo wapinzani kwa mbinu zao za kutumia land cruiser hard top?
 
Hali ilivyo
 
Attachments

  • downloadfile-3.jpg
    downloadfile-3.jpg
    56.7 KB · Views: 1
Ngoja niendelee kunywa kahawa huku nikiendelea kuperuzi kurasa za thread hii. Nimsikiliza Lisu vizuri sana leo pale nyumbani kwake akihojiwa na Masoud na Fety kutoka Clouds. Nawasihi sana Wanachadema mpeni huyu ndugu uwenyekiti wa Chama chenu. Naamini Wapo wengi huko kwenye Kijani na Njano wanaowaunga mkono kimyakimya, kwa nia njema kabisa.
 
TAL ni alimasi inayopaswa kutunzwa, wenye akili timamu wanafahamu hilo na haijalishi wapo upande gani wa kisiasa.
 
Ukweli ni kwamba kwa sasa upepo wa siasa unavuma CHADEMA, macho na masikio ya wengi yameelekea huko.

Chama tawala ni kama wamesahaulika kwa muda, je hii ni ishara njema kwao kuelekea 2025?

Nini sababu ya chama tawala kupoteza ushawishi katika kipindi hiki kifupi? Je ni mbinu hafifu za kisiasa ambazo zinatekelezwa na viongozi wao?

Nadhani baadhi yao tayari wamepata maono kwamba hali ikiendelea kuwa hivi 2025 wataumia vibaya, endapo CHADEMA wakipata uongozi mpya hali itakuwa mbaya zaidi kwa upande wao.

Suluhisho la haya ni lipi? Je watafute mgombea/mwenyekiti mwingine kuokoa jahazi au waendelee kuwafunga midomo wapinzani kwa mbinu zao za kutumia land cruiser hard top?

Tatizo ni viongozi fake tumeona huko Arusha sasa watu wanapelekwa kwenye matope. Yaani Mkuu wa Mkoa naye analalamika!
 
TAL ni alimasi inayopaswa kutunzwa, wenye akili timamu wanafahamu hilo na haijalishi wapo upande gani wa kisiasa.
Ni kweli kabisa. Ndiyo maana kelele zimekuwa nyingi sana za kumpinga na kwa bahati mbaya kelele nyingine zinatoka upande wa chama chake. Angekuwa mgombea wa kawaida wala kusingesikika makelele yote haya. Wahenga walisema, siku zote mti wenye matunda ndiyo hurushiwa mawe. Kila la heri Chadema. Endeleeni kuonyesha ukomavu wenu katika hili pia. Mmepitia magumu mengi, na kushinda. Msiruhusu hili la Lisu kutia nia kugombea hiyo nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema taifa liwasambaratishe.
 
Swala la Kusambaratika au kuimarika kwa chama lipo mikononi mwa wanachama, wanapaswa kuelewa hiki ni kipindi cha kawaida wala sio vita.

Ni haki yao kuwafanyia kampeni wagombea wanao wataka, muhimu wasivuke mipaka na kusahau yapo maisha baada ya chaguzi.
 
Hakuna magwiji wa siasa Tanzania hii kama CCM ,Siasa kama siasa wanazifahamu haswa ,upinzani wa kweli utatokana na CCM yenyewe either kwa nguvu ya Umma au ya wanachama wake wenyewe..
 
Chama kinachotumia polisi na wizi wa kura ni ishara ya wazi kimeishiwa mbinu na ushawishi. CCM kwa sasa siyo tena chama cha siasa bali ni chama dola na chama cha namna hii siku kikiondoka madarakani ndiyo kinakufa kabisa.
 
Back
Top Bottom