Upi ni umri sahihi wa mtoto kuacha kuingia chumbani kwa wazazi wake?

Upi ni umri sahihi wa mtoto kuacha kuingia chumbani kwa wazazi wake?

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,469
Reaction score
12,391
Kwa sisi makabila ya kusini mara tu mtoto (wa kike na kiume) anapopitia jando na unyago,hua ndio tiketi ya kuacha kuingia chumbani kwa wazazi wetu, ulingana na mafundisho tunayopewa kule,

Haijalishi una umri gani yani hata uingie jando na miaka 8 Ni MARUFUKU KABISA na kamwe hautakaa uingie chumbani kwa baba na mama yako labda iwe ni kwa dharula kubwa mnooo ambayo hakuna mbadala wa mtu mwingine kuingia huko.

(Marufuku hii huwa haiapply kwa wajukuu kuingia chumbani kwa bibi na babu zao.)

Je, huko kwenu ni umri gani ni sahihi kwa mtoto kuacha kuingia chumbani kwa wazazi wake?
 
Kwangu sina kizingiti kabisa. Ila tu mtoto akishaanza kujitegemea hutegemei awe tena nashughuli ya kuingia chumbani. Ni Busara kwangu asubuhi watoto walikuwa wanagonga kutujulia hali nikisema karibu wanafungua mlango. Nisiposema karibu Nikamjibu Tu wanajua kuwa hawatakiwi kuongia. Ndiyo nilivyofundisha. Na muda mwingine nilikuwa natuma chumbani kuniletea kitu. Na kuna mambo Fulani ya kifamilia chumbani kwangu watoto walijua kabati au droo yenye vitu Fulani muhimu. Na kwenye safe kuna list ya vitu vilivyopo na combination keys vimehifadhiwa na watoto walijua vilipohifadhiwa. Hata kwa sasa wanajua maana wote wanajitegemea. Ni muhimu mno kushirikisha watoto wajue arrangement ya chumba chako na chumba kile unachohifadhia vitu muhimu. Narudia ni muhimu mno. Ila angalizo ukiona watoto kitabia siyo poa basi kuna mmoja au wawili washirikishe. Walipokuwa wadogo kabisa walikuwa wanajingiza tu kwa Fujo kama mbuzi🤣🤣🤣 na walikuwa wanaomba zamu za Kulala chumbani mpaka walipofika say 5 yes. Last born alilala Sana chumbani kwetu mpaka nilipomtoa ilikuwa mbinde Sana kusinzia chumbani kwake. Tuna bond kubwa Sana na huyu kuliko wengine japo nao Kwa kweli family bond ni kubwa mno. Ninamshukuru Sana Mungu.
 
Ukikuta dingi yako kaganda kifuani kwa maza ako anasukuma moja moja utajiskiaje? (samahani kwa mfano mbaya)
Kwahiyo (kulingana na maandishi yako)watoto wadogo ndio wanafaa kushuhudia? Hii sio hoja, otherwise familia iwe na watu wasio na utashi.
 
Ukikuta dingi yako kaganda kifuani kwa maza ako anasukuma moja moja utajiskiaje? (samahani kwa mfano mbaya)
Wazazi wetu walitufundisha kupiga hodi kabla ya kuingia chumbani.

Hawakuishia hapo,walitufundisha pia kuingia endapo utaruhusiwa kuingia.

Hivyo mfano wewe wazazi wako wanapigana miti alafu ikaingia bila hodi basi ni halali yako kuwakuta hivyo.

Ila mtoto muungwana atapiga hodi,wazazi kama wanapigana miti hawatomruhusu mtoto aingie na hivyo haiwezekani mtoto kuwafuma wazazi wake katika tendo.

Kwa mantiki hiyo adabu ya hodi inazingatiwa kabla ya kuingia chumbani kwa wazazi.

Lakini pia katika hali nyingi watoto tunaingia chumbani ikiwa tumetumwa na wazazi wetu kwamba safuher kanichukulie kitu fulani chumbani kwangu,so kama mzqzi kakutuma ndani na yeye yupo nje sio rahisi kuwafuma wazazi wako wakiwa faragha.

Kiufupi mkuu ukizingatia kitu "hodi" huweI kuweka hoja kama hiyo uliyoiweka
 
وَإِذَا بَلَغَ ٱلۡأَطۡفَٰلُ مِنكُمُ ٱلۡحُلُمَ فَلۡيَسۡتَـٔۡذِنُواْ كَمَا ٱسۡتَـٔۡذَنَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمۡ ءَايَٰتِهِۦۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ

(Dr. Mustafa Khattab)
And when your children reach the age of puberty, let them seek permission ˹to come in˺, as their seniors do. This is how Allah makes His revelations clear to you, for Allah is All-Knowing, All-Wise.

(Ali Muhsin Al-Barwani)
Na watoto wanapo fikilia umri wa kubaalighi basi nawatake ruhusa, kama walivyo taka ruhusa wa kabla yao. Hivyo ndivyo anavyo kubainishieni Mwenyezi Mungu Aya zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima.

-Surah An-Nur, Ayah 59

Quran inatufundisha hivyo
 
Watoto wangu huwa wanaingia kwa kupiga hodi, bahati nzuri mama yao alishawapa hayo maadili, kuna wakati nikitoka safari wanakuwa wananiganda muda wote chumbani ninapoenda kulala. Ila mi nafurahi tu, kwa sababu ndio furaha yao
 
Kama ni mwanamke mpaka akiolewa bado anaruhusiwa.
 
Wazazi wetu walitufundisha kupiga hodi kabla ya kuingia chumbani.

Hawakuishia hapo,walitufundisha pia kuingia endapo utaruhusiwa kuingia.

Hivyo mfano wewe wazazi wako wanapigana miti alafu ikaingia bila hodi basi ni halali yako kuwakuta hivyo.

Ila mtoto muungwana atapiga hodi,wazazi kama wanapigana miti hawatomruhusu mtoto aingie na hivyo haiwezekani mtoto kuwafuma wazazi wake katika tendo.

Kwa mantiki hiyo adabu ya hodi inazingatiwa kabla ya kuingia chumbani kwa wazazi.

Lakini pia katika hali nyingi watoto tunaingia chumbani ikiwa tumetumwa na wazazi wetu kwamba safuher kanichukulie kitu fulani chumbani kwangu,so kama mzqzi kakutuma ndani na yeye yupo nje sio rahisi kuwafuma wazazi wako wakiwa faragha.

Kiufupi mkuu ukizingatia kitu "hodi" huweI kuweka hoja kama hiyo uliyoiweka
Unapiga hodi, chumba Cha wazazi unataka kwenda kufanya Nini?
Kuna mahitaji gani muhimu unahitaji kwenye chumba Cha wazazi?
Chumba Ni faragha jamani, hebu kuweni serious!
 
  • Thanks
Reactions: THT
Back
Top Bottom