Kwa sasa sio muda sahihi kusema mchezaji gani ni bora kati ya Razak wa Yanga na Chikwende wa Simba. Kuna kuzoea mazingira, mifumo ya uchezaji, vyakula, lugha, kuzoeana na wachezaji wenzake, uhitaji wa timu iliyomsajili, benchi la ufundi, n.k. Mpira ni mchezo unaochezwa hadharani tusubiri tuwaone tusiwe wapiga ramli kwani miguu yao itaongea. Mpira ni mchezo wa ajabu sana kwani mchezaji anaweza kuwa bora kwenye timu A lakini akaenda kuwa kichekesho kwenye timu B. Na mifano ipo mingi sana duniani Mateja Kezman, Shevechenko, Hazad, Donald Ngoma, na wengineo