Pole ndugu yangu, tatizo hayo mambo huleta roho chafu zinakuvaa na kutake control of ur life ndo mana huwa ngumu kuacha.
Cha kukushauri tu kama wewe ni Mkristo hebu omba tena omba hasa, anza na toba. Uzinzi wa aina yoyote ile unamuaibisha Mungu kumbuka mwili ni hekalu la Bwana, sasa dhambi hii huwa inampa shetani kibali cha kuku control kupitia huo mlango ulimuachia wazi, Mpaka utakapoufunga huo mlango ndipo shetani ataacha kukutesa.
Na Mungu ni wa Rehema ndo mana hata anakupa Neema ya kutambua kwamba unakosea na unataka kutubu ili uache kabisa huo uovu. Kumbuka tukitubu kwa moyo wa kumaanisha yeye hutusafisha kabisa na kututenga mbali na dhambi ''kama mashariki ilivyo mbali na magharibi hivyo ndivyo ataweka dhambi zetu mbali nasi''.
Mwambie Mungu nakuja mbele zako naomba toba na msamaha kwa kukuabisha pale nilipozini kinyume na mpango wako, Mungu nakiri kuwa nimekutenda dhambi naomba Unisamehe, unioshe kabisa uovu wangu, unitakase dhambi zangu, mana nimejua mimi makosa yangu na dhambi yangu i mbele yangu daima, unifutie hatia zangu zote,
Bwana neno lako likae ndani yangu nisije kukutenda dhambi, Yesu wewe hukuja kuwaita wenye haki bali wenye dhambi kama mimi, katika jina la Yesu navunja connection zote za kiroho kati yangu na masturbation, navunja mamlaka niliyompa shetani pale nilipotoa mwili wangu kwake, Navunja soul tie zooote na nguvu zote za giza zilizoingia kwangu kupitia masturbation, naweka msalaba wa Yesu kati yangu na kitendo hiki na naagiza nafsi, roho na mwili kusahau kabisa, najiwekea ukuta wa damu ya Yesu. Asante Yesu kwa kunisamehe, kunikomboa na kunisafisha. Amen
Hii iwe sala yako usiku na mchana, na ukumbuke kufanya mazoezi au kujiweka busy ili usipate nafasi ya kuyawaza mambo yatakayofanya mwili upate udhaifu wa kuwaza ngono.