Mimi ninachokushauri ni hiki, kwanza tambua ya kuwa wewe ni wa mhimu sana mbele za Mungu.
Punyeto au utazamaji wa porn ni chukizo kubwa sana mbele za Mungu, kwani unapotazama picha za ngono au kupiga punyeto unakuwa unampa utukufu shetani,na mtu yeyote anayekuwa akitenda dhambi huwa anakuwa mtumwa wa dhambi hiyo, hivyo hawezi kuwa huru hata siku moja.
Picha zote za ngono, majarida au habari za ngono hizo hazipo kwa ajiri ya kukupa burudani, huo ni mtego uliowekwa na mawakala wa shetani ili kuwanasa watu wa Mungu wapate kuanguka. Wacheza sinema za ngono hao huwa wanalaana tangu awali ,kwani wapo tayari kufanya lolote na wakati wowote,ndo mana waweza kuwaona wengine wanafanya ngono,mtu mmoja kwa watu watano au zaidi. Na wengine utawakuta wanafanya ngono na mbwa au na mnyama yeyote, hiyo ni laana.
Kutazama au kupiga punyeto, kunakaribisha pepo wachafu kuweza kumuingia mtu,ndo mana unakuwa na kiu ya kutazama, huwezi kumaliza siku mbili au tatu bila kutazama, mwanamke au mwanaume akinaswa na hizo picha yupo tayari kulala na dada yake au kaka yake. pindi unapotazama picha hizo chafu usizani ya kuwa upo peke ako, hapo unakuwa na pepo wachafu wakikutazama na kushuhudia udhaifu wako.kuna watu unawaona kwenye hizo video clips ,wanawake wazuri na warembo hasa, sio wote ni binadamu, kuna wengine ni pepo wachafu wakiwa wamevaa maumbo ya kibinadamu, wapo tayari kumuangamiza yeyote anae kuja mbele yao.
Na tambua ya kuwa sisi sote tu viumbe vya Mungu na hivyo twatakiwa kuwa safi wakati wote, kiroho na kimwili. Sasa pindi utazamapo picha za ngono au kupiga punyeto roho wa Mungu huwa anaondoka na kukuacha peke yako mana hawezi kuishi katika mwili utendao maovu, kama tunavyojua ya kuwa mwili ni hekalu la roho mtakatifu aliye msaada wetu wakati waote,
Sasa tunapokuwa mbali na roho mtakatifu uwepo wetu umekuwa bure, maana yeye ndio msaada wetu kwa kila jambo,atuepusha kwa ajari, atupatia neema na baraka na ndio mwombezi wetu .
Ushauri wangu, jikane nafsi yako tangu sasa na uamue kuacha mara moja huo mchezo mchafu, jiulize tangu umekuwa ukifanya hayo umefaidika na nini sasa???
Kama sio kupoteza mda, kujitia hatia, kusononesha roho yako, kupata hasara ya bando zako kwenda bure kutokana na kupakua vitu viovu na kuvifuta tena na tena, kuwa chukizo mbele za Mungu.
Kweli Mungu huchukizwa na dhambi, sasa unapenda wewe akuchukie na kukuona wa ovyo ulie kubali kushindwa na mambo ya kidunia?.
Au hujui ya kuwa imeandikwa, "msiifate dunia wala vilivyomo ndani yake,mana dunia imejaa tamaa ya macho, tamaa ya mwili na kiburi cha uzima"
Tena imeandikwa ikimbieni zinaa, tena tumeambiwa tuvitunze viungo vyetu na tuvifanye viwe safi,na tuifanye miili yetu kuwa safi na tayari kwa kumtolea bwana.
Mungu huchukizwa na dhambi. muombe Mungu wa rehema akurehemu,akusamehe na uaachane na uovu huo usio na faida, kwa Mungu yote yawezekana maana yeye ndo muweza wa yote. Ubarikiwe katika kristu bwana