Upigaji Uyui: Waziri Mkuu ashangazwa kibanda cha Mlinzi VETA kujengwa kwa Tsh. milioni 11, aagiza waliyosimamia ujenzi kukamatwa

Sasa hao mnaoita Wakuu wa Wilaya sijui Mikoa na Takukuru wenyewe huwa wanafanya Kazi gani Sasa kama vitu kama Hivi hata waje viongozi wa Kitaifa?

Kwani wanapoenda kukagua huwa unakagua nini sasa ikiwa huwezi fanya break through ya items husika?

Mpaka hapo wengine watakuwa wamestuliwa so wataingiza gharama kwenye items zingine..

Yaani sekretarieti za Mikoa zina wahandisi sasa Kazi zao huwa ni zipi hasa?
 
Itakuwa ni kweli.
Mimi nyumbani kwangu nimejenga choo na bafu ukubwa huo juu nimemwaga slab ya zege cement kali siyo hizo bati za Kiboko za kupauka tofali 6inch tena za kulala na imenigharimu 3,725,000/=.

Na ni Dar siyo huko porini huko wanatumia tofali za kuchoma moja Tsh 100,watu wanakula kwa urefu wa kamba zao usitetee ujinga
 
Boss upo kwenye chain hiyo nini?
 
Hivi TAKUKURU hadi waagizwe,wao hawaoni?wasipoagizwa hawafanyi kazi au wanachagua kazi za kufanya?
Hiyo wilaya ina mkuu wa wilaya,kamanda wa TAKUKURU,mkuu wa Usalama wa wilaya wote hawaoni hadi Waziri mkuu aagize?
 
Huyu PM anadharauliwa sana, amri zake huwa zinaishia magazetini. Hata kamati zake za kuchunguza huwa ni funika kombe
 
Waziri mkuu ni zaidi ya MANDONGA. Ameshaunda kamati nyingi sana za kufuatilia ubadhirifu lakini hakujawahi kuwa na mlejesho wowote ule.

CCM kwenye ubadhilifu huwa hawashugulikiani zaidi ya kulindana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…