Upigaji Uyui: Waziri Mkuu ashangazwa kibanda cha Mlinzi VETA kujengwa kwa Tsh. milioni 11, aagiza waliyosimamia ujenzi kukamatwa

Upigaji Uyui: Waziri Mkuu ashangazwa kibanda cha Mlinzi VETA kujengwa kwa Tsh. milioni 11, aagiza waliyosimamia ujenzi kukamatwa

Hao wamekula pesa ndogo ya kula tu. Mbona wale wa ripoti ya CAG mwaka wa fedha mbona wao wameachwa? Tuache double standard. Mkiamua watu wale acheni wote
 
Ni sawa tu, kwasababu mbao na mabati na materials mengine tumenunua Ukraine, sasa masuala ya logistics ili utoe mzigo wako Ukraine ni lazima upitie Urusi ambapo Kuna gharama za kulipa; jumla vyote kutoka Ukraine mpaka Tanzania.

1. Usafiri na manunuzi milioni 6.
2. Mkandarasi kutoka China milioni 3
3. Posho ya viongozi wa Mwenge milioni 1
4. Mchango wa matibabu ya mke wa Mkurugenzi milioni 1
 
Hilo la kudhulumiwa liko sana. Wanakukopa wanachelewa kukulipa miaka kadhaa wakijua umefilisika na kampuni haiko wanakuja wanakuambia wanataka kukulipa ulete leseni ya sasa na address ya ofisi wakati wanajua fika hunavyo.. Serikali inanjia nyingi za kudhulumu basi tu.
Hizi tunaitaga serikali ya kijambazi,yaani ikikuona una hela basi baadhi ya viongozi wasio waaminifu watakutengenezea mazingira ya kukudhulumu mali zako kwa mgongo wa serikali
 
Huyo RC enzi za Jiwe mpaka sasa tungekuwa tumeshaletewa waraka wa utenguzi kutoka kwa Mjomba Msigwa!
Inamaana TISS na TAKUKURU walikuwa hawajui au ni vita ya nyongeza ya mashahara Kati ya Watumishi wa serikali na serikali imeanza rasmi🤣🤣🤣
 
Lakini hizi pesa hadi kumfikia mkandarasi si huwa kuna mlolongo kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya umma? Consultant alikuwa wapi?
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Tabora kuchunguza gharama za ujenzi wa kibanda hicho.

Majaliwa amesema hajaridhishwa na gharama za ujenzi wa kibanda hicho kilichopo katika chuo cha VETA cha Uyui na hivyo TAKUKURU iwahoji wote waliohusika akiwemo Mkandarasi.
 
Kitakuwa kimesheheni furniture.. recliner matata na office table za mbele huko.
 
“Sitamvumilia yeyote atakayemuhujumu Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, watafutwe na wachukuliwe

Hakuna kitu hapo,kuwa mkali kwa kusema “atakaeihujumu serikali maana serikali ni wananchi" hizo blah blah blahs sijui muhushimiwa sijui kitu gani nikujipendekeza kwanza hao anaowatisha wameshajua huyo aliye-mention hapo hana cha kuwafanya na kweli cha kuwafanya hana.
 
Lakini hizi pesa hadi kumfikia mkandarasi si huwa kuna mlolongo kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya umma? Consultant alikuwa wapi?
Hao wote ni mchwa!

Sheria ya manunuzi inafanya kazi ngazi ya wajumbe wa mitaa na wafanyabiashara na wanunuzi mitaani tu inapokuja habari ya tenda kubwa za serikali hizo sheria zinawekwa kapuni watu wanapiga.
 
Kwa ujenzi wa kiserikali hiyo bei ni sahihi.
Kuna physibility study ya jengo kikao.
Kuna kunununa eneo kikao.
Kuna kupima udongo wa kiwanja kikao.
Kuna kumtafuta mkandarasi mshauri kikao.
Kuna kutangaza zabuni kikao.
Kuna kumchagua mzabuni kikao.

Vikao vyote vina posho.

Ikijumlisha na ujenzi imara wa hiyo ofisi hiyo gharama ni halari kabisa.
 
Hizi komedy .

Kwani wakati wanakijenga mpaka kina kamilika walikua wapi??

Au ndio mpaka aje kiongozi wa siasa aseme jambo ndio lifanyike.

Watu wameajiriwa na wanalipwa mishahara ya tozo ila kazi ndio mpaka wasukumwe kama mapunda.
 
Back
Top Bottom