Upigaji wa honi za Magari wakati wa kuingia Majumbani

Habari Wakuu!

Kuna hii tabia ya Watu wanaoishi katika Nyumba zenye mageti, pindi wanapokuwa wanarudi majumbani mwao kuanza kupiga honi (wakati mwingine mfululizo) ili wafunguliwe mageti, hasa hizi nyumba ambazo mageti yake hufunguliwa na Mmojawapo wa mwanafamilia na sio Mlinzi.

Hivi kuna ulazima huo kama humo ndani unapotaka kuingia ni kwako na karibia watu wote wa humo ndani una namba zao za simu? Kuna tatizo lolote ukimpgia simu mmojawao ukiwa nje umesimama au umekaribia kabisa getini kuwa akufungulie?

Ki usalama pia hii nadhani haijakaa vizuri, watu wanaweza kujua umerudi au bado kwa kusikilizia honi zako tu, mana mlio wa honi unaenda mbali kidogo.

Pia ni usumbufu hata kwa majirani hasa nyakati za usiku, kwa maoni yangu upigaji wa simu ni bora zaidi Kuliko ufunguliwe geti kwa kupiga honi.

Naomba kuwakilisha.
Gari unalo wewe
 
Kwa hiyo unataka ukifika uruke ukuta uzame ndani

Ova
 
Mimi hua sipigi honi nashuka mwenyewe kwenda kufungua geti japo hii inaubaya wake mtu anaweza ingia kwa gari akaondoka nalo...nawaza Tu. Anyways nachukia horn Sana. Mi hua sipigagi honi kishamba. Dah watu washajua nna gari, hizi mada zingine bhana inabidi tukae kimya. Sema hamjajua Nina gar Aina gani mhaya mie, maana si kila gari ni gari
Ninayo Vogue afu iko full tank ol da time
 
Habari Wakuu!

Kuna hii tabia ya Watu wanaoishi katika Nyumba zenye mageti, pindi wanapokuwa wanarudi majumbani mwao kuanza kupiga honi (wakati mwingine mfululizo) ili wafunguliwe mageti, hasa hizi nyumba ambazo mageti yake hufunguliwa na Mmojawapo wa mwanafamilia na sio Mlinzi.

Hivi kuna ulazima huo kama humo ndani unapotaka kuingia ni kwako na karibia watu wote wa humo ndani una namba zao za simu? Kuna tatizo lolote ukimpgia simu mmojawao ukiwa nje umesimama au umekaribia kabisa getini kuwa akufungulie?

Ki usalama pia hii nadhani haijakaa vizuri, watu wanaweza kujua umerudi au bado kwa kusikilizia honi zako tu, mana mlio wa honi unaenda mbali kidogo.

Pia ni usumbufu hata kwa majirani hasa nyakati za usiku, kwa maoni yangu upigaji wa simu ni bora zaidi Kuliko ufunguliwe geti kwa kupiga honi.

Naomba kuwakilisha.
Asante Sana. Kuna point kubwa Sana hapa nimejifunza.
 
Na kuna lazima gani ya kupiga simu wakati honi ya gari ipo??
 
Serikali yetu tulivu na sikivu soon wataleta tozo ya honi

Bora honi sasa wale wanaoishi kwenye mageti simu wanazo lakini kutwa kugongeana kwa fujo
 
Hii kitu huwa inaboa sana. Unakuta mtu anapiga honi utadhani anakimbizwa alipotoka.

Huwa najiuliza why asipige simu mita chache kabla ya kufika home ili waliopo ndani waanze kutoka na kumfungulia geti on time.
 
Hii nayo kero nyingine...mtu anaokota kipande cha jiwe anaanza kugonga...hivi vile vikengele vya nje ya mageti vya kubonyeza vilipotelea wapi? Au vipi sehemu maalum!
 
Yaani mimi nilivyo mvivu kupiga simu na nikipiga ikaita mara tano isipokelewe naikata harafu nifike home nianze kuhangaika na simu ili nifunguliwe[emoji3][emoji3]no no no
Sema uzuri nikikunja tu kona kuingia nyumbani namulika dirishani moja kwa moja wife anajua tu jamaa kafika Jr anakuja speed anafungua kabla hata sijapiga mbii mbiii!
 
Hii kitu huwa inaboa sana. Unakuta mtu anapiga honi utadhani anakimbizwa alipotoka.

Huwa najiuliza why asipige simu mita chache kabla ya kufika home ili waliopo ndani waanze kutoka na kumfungulia geti on time.
Ugumu sijui huwa uko wapi, labda wapigaji wa honi wanaweza kutueleza sababu za msingi hadi kusumbua wengine hata nyakati za usiku.
 
Back
Top Bottom