Upigaji wa honi za Magari wakati wa kuingia Majumbani

Upigaji wa honi za Magari wakati wa kuingia Majumbani

Yaani mimi nilivyo mvivu kupiga simu na nikipiga ikaita mara tano isipokelewe naikata harafu nifike home nianze kuhangaika na simu ili nifunguliwe[emoji3][emoji3]no no no
Sema uzuri nikikunja tu kona kuingia nyumbani namulika dirishani moja kwa moja wife anajua tu jamaa kafika Jr anakuja speed anafungua kabla hata sijapiga mbii mbiii!
Nyumba yako ina chumba kimoja hicho hicho jikoni, sebule, chooni so Mama Jr lazima awepo tu humo ama ni dirisha hilo moja tu nyumba nzima Mkuu Baba Jr.
 
Dirisha la chumbani mkuu na nyumba nzima imeface barabarani,kutokana na ratba za maisha yangu mara nyingi naingia home night wote wamo ndani,napiga full light kisha napunguza mwanga kama sign kisha natulia watakuja tu kufungua.
 
Mkuu ulitaka wafanyeje? Kuna mambo huwezi yaepuka. Utaumia tu. Unayafanya maisha yako yawe magumu. Kama honi tu inataka kukutoa roho, makubwa je?
Hahaha nimecheka eti feni inataka kukutoa roho. Binadamu tuna makariko sana jameni mtusamehe
 
Ukiwa jirani na watu wa NISSAN PATROL, VX, nk, ni raha tupu. Wanaingia kimyakimya kwa kuteleza. Kabla hata hajasimama,geti lishafunguka.
Daa, kwenye vijigari vyetu vya mikopo, asalalaa!! Mawazo yote yako kwenye salary slip!!
 
Mimi hua sipigi honi nashuka mwenyewe kwenda kufungua geti japo hii inaubaya wake mtu anaweza ingia kwa gari akaondoka nalo...nawaza Tu. Anyways nachukia horn Sana. Mi hua sipigagi honi kishamba. Dah watu washajua nna gari, hizi mada zingine bhana inabidi tukae kimya. Sema hamjajua Nina gar Aina gani mhaya mie, maana si kila gari ni gari
Una gari aina gani?
 
Utakuwa na Passo
 
yani kwa hela hizi za tozo na mikodi kibao upige simu wakati uko getini, nadhani haujakaa sawa wewe jamaa, uko kwako getini tena upoteze hela ya kupiga simu , si bora hata ungeshauri mtu ashuke agonge geti ungeweza ukawa na hoja
 
Mimi huwa nina namba za simu za watu wa mtaa mzima, nikiwa naja nawapigia wote simu kuwa sasa naja na nitapiga honi nikifika getini kwangu...

Naachaje kulibofya bofya hili jihoni lenye mlio maridhawa wa honi ya Harrier
 
Lakini kwa nini magari yanao ongoza kupiga honi hata ukiwa babarani ni, IST specio Nissan trail, probox raum duet nk kuna siri kwenye wamiliki wa hizo gari?
Kwa sababu ndiyo mengi. Halafu wewe siyo dereva kwa hiyo hujui undani na umuhimu wa honi. Kuna watumiaji wa barabara wanaudhi sana. Honi hutumika pia kuelimisha wengine kuhusu Usalama. Hilo ndilo la msingi sana. Yaani honi ni moja ya kisemeo cha dereva. Kisemeo kingine ni taa.

Kama gari haina honi ni kosa kisheria
 
Lakini kwa nini magari yanao ongoza kupiga honi hata ukiwa babarani ni, IST specio Nissan trail, probox raum duet nk kuna siri kwenye wamiliki wa hizo gari?
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom