Upigaji wa honi za Magari wakati wa kuingia Majumbani

Upigaji wa honi za Magari wakati wa kuingia Majumbani

Tatizo sio kama mtu ana gari au hana...mimi nazungumzia huo utaratibu wa wengi ulivyo, binafsi sipigi honi nikiwa nje ya geti, siwezi kuleta usumbufu kwa majirani sababu naingia kwangu.
Dawa yao wapiga honi ni katiba MPYA tu
 
Habari Wakuu!

Kuna hii tabia ya Watu wanaoishi katika Nyumba zenye mageti, pindi wanapokuwa wanarudi majumbani mwao kuanza kupiga honi (wakati mwingine mfululizo) ili wafunguliwe mageti, hasa hizi nyumba ambazo mageti yake hufunguliwa na Mmojawapo wa mwanafamilia na sio Mlinzi.

Hivi kuna ulazima huo kama humo ndani unapotaka kuingia ni kwako na karibia watu wote wa humo ndani una namba zao za simu? Kuna tatizo lolote ukimpgia simu mmojawao ukiwa nje umesimama au umekaribia kabisa getini kuwa akufungulie?

Ki usalama pia hii nadhani haijakaa vizuri, watu wanaweza kujua umerudi au bado kwa kusikilizia honi zako tu, mana mlio wa honi unaenda mbali kidogo.

Pia ni usumbufu hata kwa majirani hasa nyakati za usiku, kwa maoni yangu upigaji wa simu ni bora zaidi Kuliko ufunguliwe geti kwa kupiga honi.

Naomba kuwakilisha.
😅😅😅 Tafuta pesa mkuu
 
Ningechangia mada lakin staki watu wajue nina miliki gari Marcedes-benz 4matic
Ngoja tu ninyamaze nisitaje na bei watu wanao miliki vigari vya 80M wasije kuona naringa
 
Waanze kutumia mifumo ya kisasa ya kufungua mageti wakiwa ndani ya magari yao.
 
Mimi hufanya yote hayo kutegemea na situation. Wakati mwingine nalitest kama halijalockiwa nalifungua.

Ki msingi mimi si mpenzi wa kupiga honi, wife alikuwa anapenda kutumia honi lakini mdogomdogo ameanza kuniiga. Watoto wengine ninaowapa kuyatumia hawapigi honi kabisa.

Ila fundi sasa akiwa analirudisha baada ya service ,anapiga honi hizo utadhani kuna majambazi yanamkimbza.
 
Huu ujinga wa honi hadi kwenye foleni.Sielewi kabisa busara ya kupigia honi gari liliopo mbele yako.
 
Ukiwa jirani na watu wa NISSAN PATROL, VX, nk, ni raha tupu. Wanaingia kimyakimya kwa kuteleza. Kabla hata hajasimama,geti lishafunguka.
Daa, kwenye vijigari vyetu vya mikopo, asalalaa!! Mawazo yote yako kwenye salary slip!!
Nissan Patrol 4.2, Discovery tdi hizo hazihitaji hata honi,Engine zake tu Ni honi Tisha.Likisimama getini unaenda kufungua mwenyewe.
 
Mkuu ukiishi India utapata tabu sana, wanasema hakuna watu wanaopenda kupiga honi kama wahindi......imagine jiji kama bombay kila mtu apige honi ndani ya gari lake, si vibe la kitoto...
 
Mkuu ukiishi India utapata tabu sana, wanasema hakuna watu wanaopenda kupiga honi kama wahindi......imagine jiji kama bombay kila mtu apige honi ndani ya gari lake, si vibe la kitoto...
Huu ndio uthibitisho kuwa honi kuna wakati ni karaha..bora za barabarani sio hizi za kufunguliwa geti Mkuu.
 
Ningechangia mada lakin staki watu wajue nina miliki gari Marcedes-benz 4matic
Ngoja tu ninyamaze nisitaje na bei watu wanao miliki vigari vya 80M wasije kuona naringa
Ndio tushajua Mkuu, hongera!
 
Je wenye muziki mnene wa gari wanapoingia Nyumbani huku volume inasome 30 wanasemaje?
 
Habari Wakuu!

Kuna hii tabia ya Watu wanaoishi katika Nyumba zenye mageti, pindi wanapokuwa wanarudi majumbani mwao kuanza kupiga honi (wakati mwingine mfululizo) ili wafunguliwe mageti, hasa hizi nyumba ambazo mageti yake hufunguliwa na Mmojawapo wa mwanafamilia na sio Mlinzi.

Hivi kuna ulazima huo kama humo ndani unapotaka kuingia ni kwako na karibia watu wote wa humo ndani una namba zao za simu? Kuna tatizo lolote ukimpgia simu mmojawao ukiwa nje umesimama au umekaribia kabisa getini kuwa akufungulie?

Ki usalama pia hii nadhani haijakaa vizuri, watu wanaweza kujua umerudi au bado kwa kusikilizia honi zako tu, mana mlio wa honi unaenda mbali kidogo.

Pia ni usumbufu hata kwa majirani hasa nyakati za usiku, kwa maoni yangu upigaji wa simu ni bora zaidi Kuliko ufunguliwe geti kwa kupiga honi.

Naomba kuwakilisha.
Account full what for ???
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]maisha magumu
Una mind hadi horn[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom