Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa Afrika ubadhilifu na uchotaji wa rasilimali za umma au chama ni vitu vinavyotokea.
Lakini hata huko Ulaya na marekani kwenye vyama vya siasa upo wizi wa kughushi na kujipatia viposho kwa njia za udanganyifu.
NdioWewe bogus naukumbuka ule uzi wako wa kutaka jiwe awe Rais wa maisha, hujielewi.
Kuna anchi fulani ya Ulaya leo mtu kaamua kuingia kanisani na kuchinja watu.Angalia ujinga ulioandika hapa! Hebu twambie huko Ulaya ni Nchi gani inafanya maovu ya kutisha kama maccm halafu inakaa madarakani miaka 59? Tafakari kwa kina kabla ya KUKURUPUKA na kuandika upuuzi.
Kuna anchi fulani ya Ulaya leo mtu kaamua kuingia kanisani na kuchinja watu.
Ni kutokana na yeye kuamini kwamba kuna ukandamizaji wa aina fulani kwa watu wa aina fulani.
Hilo jiji si lilikuwa chini ya upinzani au?Total fucken shit indeed...mvua imenyesha kidogo tu kila mahali ni bwawa,...
Siasa ni sayansi.Don’t change the subject please! What happened in France does not justify what is going in our country . Stop this stupidity please!
Hilo jiji si lilikuwa chini ya upinzani au?
Dawa ya wanaccm ni kuanza kuwapoteza mmoja mmojaKwa Afrika ubadhilifu na uchotaji wa rasilimali za umma au chama ni vitu vinavyotokea.
Lakini hata huko Ulaya na marekani kwenye vyama vya siasa upo wizi wa kughushi na kujipatia viposho kwa njia za udanganyifu.
Usikimbie ukweli kuwa halmashauri ya jiji iliyotawaliwa na upinzani haikufanya lolote kuboresha miundombinu kwa miaka mitano. Sasa yamewakuta.Kwa hio umeprove Rais na serikali yako aliposema msipomchagua fulani (CCM) maendeleo hayaji jimboni kwenu na wewe unaona ni sawa?
Siasa ni sayansi.
Mimi nigekuwa Tundu Lissu tangu alipopitishwa kuwa mgombea wa CCM angejipanga kukabiliana na sera zote za CCM na ilani yake ya Uchaguzi.
Kisha ningetafuta makosa na udhaifu wote wa CCM na serikali yake.
Halafu hapo unapata wapi pa kuanzia strategically.
Lakini si njia ambayo Tundu Lissu amepitia tangu achaguliwe kuwa mgombea wa Chadema.
Amekosea sana kimkakati na kuieledi.
Yaani ni afadhali na uchaguzi wa 2010 a 2015 ambapo Dr Sla na Edward Lowasa waliweka hekaheka.
''Sasa kibaya zaidi ni kitendo cha kuwashirikisha wageni kutaka kuvuruga amani ya nchi yetu na hata kufikia baadhi yao wageni hao khasa bwana Robert Amsterdam kuandika barua za vitisho na dhihaka kwa kiongozi wa Tanzania akidhani yeye ndie mahakama ya dunia!''Ni kama nilivyowahi kusema na ntaendelea kusema kwamba upinzani nchini Tanzania ni kiinimacho na upo kwa ajili ya kula ruzuku.
Mimi ni mmoja wa watu ambao bila kutetereka nimemuunga mkono raisi John Magufuli na serikali yake kwa miaka mitano ilopita na ntaendelea kumuunga mkono kwa yale yote mema anayoyatendea nchi hii.
Tuwe wakweli hata wewe ukiwa na mipango yako wataka uifanye na waona kabisa kuna "obstacles" au vipingamizi ambavyo vipo kwa ajili ya kukukatisha tamaa na kuvuruga ni hatua zipi utachukua?
Ndio, hii yaitwa "obstacles to progress" yaani mtu kwa makusudi kabisa apingaaa kila kitu!!
Upinzani watakiwa kuwa objective yaani uwe wapinga lakini hapohapo kwenye masuala ya kuhusu maslahi ya taifa waonekana waunga mkono asilimia 100.
Nchi zote zilizoendelea na zinazoendela wanafanya hivyo na tumeziona hata katika suala la COVID-19 wapinzani wameunga mkono jitihada za serikali na penye kupinga wamepinga na kutaka ufafanuzi.
Lengo lao la kupinga ni kuitaka serikali ifanye marekebisho ya sheria zake kuhusiana na ugonjwa huo na mengine yanayobaki kama kuunga mkono "lockdown" wameunga mkono serikali zao.
Lakini upinzani wa Tanzania ni kupinga kila lililo jema na kibaya zaidi kuzungumzia upingaji huo mitandaoni kwa kukejeli na kukashifu vitendo ambavyo wananchi wameona na wamesikitishwa sana.
Kutohudhuria vikao vya bunge na kuendelea kulipwa fedha za vikao mmeliingizia hasara Bunge na taifa kwa ujumla maana fedha hizo ni bora zingeenda kushughulikia maendeleo ya huko vijijini na huduma zingine muhimu kwa nchi yetu.
Pia kutohudhuria vikao vya bunge mmewanyima wananchi haki yao ya kufikishiwa shida zao bungeni na badala yake mkampa kazi raisi Magufuli kuzunguka nchi nzima akishughulikia matatizo ya wananchi papo kwa hapo.
Matatizo ya wananchi kama kukosa huduma ya vyoo ni jukumu ya mbunge na jimbo jimbo lake kuhakikisha kuna vyoo vya umma katika maeneo kama masoko na vituo vya mabasi.
Sasa kibaya zaidi ni kitendo cha kuwashirikisha wageni kutaka kuvuruga amani ya nchi yetu na hata kufikia baadhi yao wageni hao khasa bwana Robert Amsterdam kuandika barua za vitisho na dhihaka kwa kiongozi wa Tanzania akidhani yeye ndie mahakama ya dunia!
Wananchi wa Tanzania si wajinga ni watu waelewa sana na wapinzani wasidharau kauli hii.
Nilisema pia humu kuwa wananchi hawa walojitokeza kwenye mikutano yenu hawakufanya hivyo bila sababu, walitaka kusikia mnachosema majukwaani.
Mlichofanya mkaishia kumzungumzia raisi Magufuli na serikali yake badala ya kunadi sera zenu na ilani za vyama vyenu.
Niliwakumbusha hapa ndani kabisa ya kampeni baada ya kuona mnapotea lakini hamkusikia mkazidisha kuchukua picha za nyomi la watu na kutupa mtandaoni.
Wapinzani leteni sera mbadala zidi ya serikali zenye tija ili kumkomboa mtanzania
Nimekua nikifuatilia mijadala ya bunge Hili la bajeti 2016 /17.Michango mbali mbali inatolewa na wabunge wa pande zote mbili, yaani wa chama tawala na wapinzani.Nataka nijikite kwa wabunge wa upinzani kwa kuwapa ushauri ambao si sheria na kama si sheria basi hawalazimishwi kuufuata. Rais...www.jamiiforums.com
Sasa hivi wanawachapa bakora khasa na kuwakumbusha kuwa upinzani ni kuwa objective unampinga mtu na hapohapo waonyesha unamsaidia katika baadhi ya mambo ambayo ni positive.
Kiukweli mnahitaji kujipanga uzuri na kuja kivingine mkipinga yanayostahiki na kuisaidia serikali kufanya shughuli zake bungeni na majimboni kwa ufanisi na huko ndiko kula na kipofu.
Sasa hata yule anefahamu kula na kipofu anawashindaaa!!
Hiyo ni kwasababu upinzani kuja kutawala nchi hii itachukua miaka mingi sana na sababu ni haohao wananchi mnaowadharau kwa kuwaita wajinga.
Lakini ni kheri mjinga asiefahamu na anaengojea kuelimishwa kuhusu sera mbadala, kuliko yule mpumbafu anaejiona afahamu kila kitu na hata kutumia mabeberu kutaka kuiuza nchi yake.
Tuendelee kushuhudia kichapo kutoka kwa wananchi na poleni wapinzani, poleni sana.