Upinzani mkubali ukweli, Wananchi wamewachapa bakora kwa kutokukaa bungeni na kupinga kila kitu

Contents za uzi zinahusu uchaguzi mkuu wa 2020.
Na hapa ndio ulitakiwa uweke hizo mbinu mbadala acha ngonjera za 2006.
Mimi kabla ya 2015 nilikuwa mpinzani khasa tena wa aina ya Dr Slaa.

Tuliongoea sana humu na tukawa twamponda weee JK wa watu.

Chadema ilitakiwa kimyakimya inaanda majimbo hivyo kwanza kutafuta watu ambao watakuwa wagombea wao wa maana wa ubunge.

Pili, wabunge wa Chadema walipaswa kushiriki shughuli za maendeleo na sio kwenda majimboni wakati wa kampeni kama alivyofanya bwana Mbowe na alichokutana nacho nafikiri ulikisikia.

Hivyo ni kama nnavyosisitiza, kuwa kimkakati zaidi yaani strategic na kuwa objective.

Ukifanya hivyo hata siku ukiomba mdahalo utaonena unafaa kufanya mdahalo.

Ukiwa mshari sahau kila kitu.

Siasa ni sayansi.

Ndo maana CCM walikuwa wakiwaangalia mlipokuwa mkijimwambafwai majukwani na ukimsikiliza Polepole utaona namna anavyojibu hoja kisayansi na wananchi wanasikiliza na kuelewa.

Hata Bashiru nae taratibu akawaita mabalozi kuwaambia ukweli kwamba watulie na wakamwelewa.

Watanzania si wajinga ila hawapendi shari na vurugu.

Hata ile siku mabomu yalipolipuka kule Mtoni nilishuhudia jinsi watiu walivyoacha majumbani vitoto vichanga na vibibi kizee na kukimbilia kusikojulikana.

Ilikuwa ni baada ya utulivu ndipo watu walianza kuchungulia na kujitokeza uwanja wa Taifa kutafuta ndugu zao.

Narudia, siasa ni sayansi.
 
Kwa kukomesha kabisa Magu atateia viongozi wa upinzani kibao[emoji23][emoji23][emoji23] ili kuwatia hasira zaidi
Teeth watawashawishi baadhi ya wabunge walioangushwa wajiunge na ccm ili wapate vyeo ,achana na mayalla(njaa),hatutoamini yatakayokuja kutokea.
 
Tutakavyoanza kuisoma namba watakuwa wanaangalia ulikuwa unashabikia chama gani au wote tutaisoma namba
Kama mtu una shughuli yako inayokuingizia kipato halali kwanini uwe na wasiwasi?
 
Malawi ni chama kikuu ndicho kimerudi madarakani hivyo si kazi sana kurudi kwani kilihitaji kuongeza idadi wa wabunge.

Seychelles bwana Ramkalawan amejaribu chaguzi sita! ndo amekuja kushinda uchaguzi huu.

Na raisi aliekuwepo na huyu raisi mpya wanapishana mwaka mmoja kiumri raisi mpya akiwa na mkubwa hivyo hii yaweza kuwa ni moja ya sababu wananchi wanapima sera.

Isitoshe babu yake raisi mpya ni mhamiaji mwenye asili ya India katika jimbo la Bihar, hivyo mkono wa India katika uchaguzi huo hauwezi kukwepeka.

Kuna mvutano baina ya mataifa ya India China na Marekani katika kisiwa hicho hivyo kutolewa taarifa mbalimbali kutoka katika serikali za nch hizo pia si jambo la kushangaza.

Hivyo si jambo la kushangaza wananchi wameamua kubadilisha upepo.
 
Acha ujinga wewe sasa chama kilichopo madarakani kingetaka kutengeneza mazingira kama ya hapa unadhani hao wangeshindwa?
Mbona una ufinyu wa akili kiasi hicho? Kwa hiyo kwa UFINYU wa akili yako Chadema ijaribu chaguzi ngapi ndiyo ishinde hata kama Watanzania walio wengi wamewachoka maccm?

 
Acha ujinga wewe sasa chama kilichopo madarakani kingetaka kutengeneza mazingira kama ya hapa unadhani hao wangeshindwa?
Mbona una ufinyu wa akili kiasi hicho?
Hujanielewa.

Itakuwa ni ngumu sana kuelewana kwani wewe tayari ulikwishaamini Chadema itashinda uchaguzi wa mwaka huu.
 
Sasa hapa ndio umeongea mkuu.
Hoja imeshiba vizuri. Tuko pamoja.

Ila licha ya madhaifu ya upinzani bado haiondoi ukweli kuwa ccm wameiba sana huu uchaguzi hilo liko wazi labda kama umetekwa na ukada wa ccm.
 
Leo 29/10/2020 ilikua siku ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad Swallalaah Alayh Wassallam..
Utaratibu kila mwaka kunakua na baraza la maulid kitaifa na bakwata ndio waandaaji.

Vipi mbona kama sikusikia chochote? Au bakwata ndio hivo tena walikua busy na uchaguzi, maulid yakawekwa pembeni?
Miaka iliyopita 👇👇👇
BAKWATA: Maadhimisho ya Maulid kufanyika Novemba 09, Mwaka huu
Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limetangaza kuwa mnamo Novemba 09, 2019 yatafanyika maadhimisho ya Kitaifa ya Maulid katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza Aidha, Baraza hilo limesema kuwa Baraza la Maulid litafanyika Kitaifa mnamo Novemba 10, 2019 katika Ukumbi wa Benki Kuu...
www.jamiiforums.com www.jamiiforums.com

Baraza la Maulid Tanga lampongeza Rais Magufuli. Mufti Mkuu akemea masuala ya ushoga
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi ametumia Baraza la Maulid kuwataka Masheikh wa mikoa nchini kukemea vitendo vya ushoga ambavyo vinaharibu sifa ya Uislamu. Mufti amesema hayo leo Jumanne Novemba 20, 2018 alipokuwa akiwahutubia wananchi katika kumbukizi hiyo ya kuzaliwa Mtume Muhammad...
www.jamiiforums.com www.jamiiforums.com
 
Hawakosi visingizio. Wananchi wamewachapa kabora kweli kweli. Mwingine huyu hapa anawachapa 👇:

 
Sasa hapa ndio umeongea mkuu.
Hoja imeshiba vizuri. Tuko pamoja.

Ila licha ya madhaifu ya upinzani bado haiondoi ukweli kuwa ccm wameiba sana huu uchaguzi hilo liko wazi labda kama umetekwa na ukada wa ccm.
Hii ya CCM imeiba kura ni imani na madai yenu ambayo yataka kuondoa ukweli kwamba mmeshindwa uchgyzi huu kwa kishindo.
 
Shetani wewe unakula kod zetu
 
Hii ya CCM imeiba kura ni imani na madai yenu ambayo yataka kuondoa ukweli kwamba mmeshindwa uchgyzi huu kwa kishindo.
Mkuu nimegundua wewe sio objective ni subjective. Haihitaji rocket science kujua hili suala hata layman wa mtaan huku wanafahamu.
Haya endelea na mada yako, mimi niishie hapa.
 
Maadui Wa Nchi Yetu Ni:-

Umasikini

Ujinga

Maradhi

Halafu Na Hiki..........M

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…