Upinzani mmezimishwa sio kama hamtaki kusema

Hahahahahaaa
 
Acha wee! Tunajua janja yenu. Buku saba zimekata.
 
Ningependa kutoa ushauri kwa watanzania wote, tusijaribu kusherehekea siasa kama ushindani wa mpira. Kuwepo kwa political balance kwenye vyombo vya kutunga sheria ni suala muhimu kwa afya ya taifa lolote. Nadhani hii ndio motivation ya mataifa wahisani kutusukuma kwenye demokrasia wakiamini bila yake hatuwezi kufika.

Kuna haja ya kutafakari ni kwanini political balance imekosekana. Tukishafahamu tatizo lilopelekea hapo tulipo, ndio tujaribu kutoa suluhisho. Ninachokusudia kusema hata kama bunge la sasa lingekuwa na +90% ya CHADEMA/CUF/ACT bado kwa aliemakini hatopendelea hali hio. Na sio hapendelei kwasababu yeye ni CCM/NCCR bali imekosekana balance ambayo ni muhimu kwa afya ya taifa.

Unapokuja kusema kwamba serekali ya sasa imekamilika na haina makosa. Nadhani wengine hatukufuhamu, ikiwa serekali hata za nchi zilizoendelea bado kuna mambo mengi ya kutafakari na kuboresha. Wakati wao wako mbele na wametuzidi kwa miaka mingi katika maendeleo, ulitaka tukufuhamu vipi ?

Maeneo haya naweza yatolea mfano ambapo nina uhakika kuna mambo mengi yanahitaji uboreshaji:
  1. Elimu haizalishi majembe/vichwa
  2. Afya
  3. Haki za binadamu na utawala bora / uhuru wa kujielezea
  4. Ajira
  5. Sheria nyingi chakavu na zina upungufu mkubwa wa kukabailiana na hali halisi
  6. n.k
Maasalaam
 
Wakikaa kimya unateseka sana? Nawewe kaa kimya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…