GE2025 Upinzani ndani ya CCM: Kinachompoza Samia ni kuwa mwanamke?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Kusini pride

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2022
Posts
1,762
Reaction score
4,079
Upinzani wa Ndani CCM, Kinachomponza Samia Ujanajike Wake

Katika siku za hivi karibuni, tumeona kuibuka kwa baadhi ya wanasiasa waliowahi kuwa ndani ya mfumo wa utawala wa awamu ya tano—wakijaribu kuvaa joho la uanaharakati na kuunyooshea kidole utawala wa sasa. Alianza Job Ndugai kwa kauli zenye miguno ya malalamiko. Akafuata Askofu Josephat Gwajima kwa maneno ya kejeli yenye ladha ya chuki ya kisiasa. Sasa ni Humphrey Polepole, akijaribu kuandika upya historia kana kwamba yeye hakuwa sehemu ya kinacholalamikiwa leo.

Lakini historia haijisahau.

Watu hawa si wapya katika siasa za Tanzania. Si wageni wa mfumo wanaoupinga sasa. Wamekuwa sehemu ya mfumo ambao leo wanaunyooshea kidole. Tofauti ni kwamba, wakati mfumo ulipowapa nafasi kubwakubwa, walinyamaza. Walitumia mamlaka yao kufunika maovu, kuhalalisha unyanyasaji, na kuwakemea wale waliothubutu kuhoji.

Serikali ya Magufuli: Hali Halisi Waliyonyamazia

Wakati wa utawala wa Hayati John Magufuli, Tanzania ilishuhudia ongezeko la matukio ya kukamatwa kwa wanaharakati, wanasiasa wa upinzani, na hata watu wa kawaida waliokuwa na maoni tofauti. Matukio ya kutekwa, kubambikiziwa kesi, kufungwa kiholela, na kuporwa kwa ushindi wa chaguzi yaligeuka kuwa kawaida.

Na bado, Ndugai akiwa Spika wa Bunge, Gwajima akiwa mbunge, na Polepole akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM—hawakusema chochote. Walikuwa mstari wa mbele kuhalalisha, kutetea na hata kushambulia wale waliokemea.

Leo wanarudi kama watetezi wa haki? Kama mashujaa waliochelewa? Hapana. Historia itawahukumu kwa ukimya wao wa wakati ule na unafiki wao wa sasa.

Tatizo ni Mfumo Dume, si Samia

Msingi wa malalamiko yao hauko katika uovu wa serikali, bali katika kuvunjika kwa ndoto ya mfumo dume wanaouhusudu. Hawa walikuwa na mgombea wao, walichokuwa wanasubiri Magufuli amalize hatamu yake. Magufuli alipofariki ghafla, walihamaki. Inasemekana, kulikuwepo na mpango wa kumfanya Samia Suluhu Hassan awe Rais wa mpito tu, kisha taifa liende kwenye uchaguzi mpya ili kurudisha mtu wao.

Hawakuwahi kumkubali Samia. Si kwa sababu ya sera, bali kwa sababu ya jinsia na asili ya uongozi wake. Alipovunja mnyororo wa utegemezi na kuanzisha mwelekeo wake—wakati mwingine kwa makosa yake—ndipo wakageuka na kuanza kupiga kelele kama vile walikuwa wapinzani wa kudumu.

Tuwe Makini: Historia si ya Kuandika Upya

Watanzania hawawezi kusahaulishwa yaliyotendeka. Sauti za sasa za malalamiko haziwezi kufuta ushiriki wa watu hawa katika misingi ile ile wanayoikemea leo. Siasa za Tanzania hazihitaji mashujaa wanafiki—wanaotokea tu pale wanapopoteza fursa au madaraka.

Tunapaswa kupima hoja zao si kwa ukubwa wa sauti, bali kwa ukweli wa historia zao. Je, walikuwa wapi wakati watu wakipotea? Wakati chaguzi zikiibwa na kunajisiwa? Wakati upinzani ukizimwa kwa nguvu za dola? Wakati mikutano ya hadhara imepigwa marufuku, Polepole si alikuwa Katibu Mwenezi wa CCM?

Wasitufanye wajinga. Ukimya wao wa jana ni ushahidi wa unafiki wao wa leo.

Hitimisho: Tusiingie Mtegoni

Mabadiliko ya kweli huanzia kwenye ukweli na uwazi wa dhamira. Tanzania haitajengwa kwa kurudi nyuma kwenye mitandao ya zamani ya kifisadi na kikatili, bali kwa kuangalia mbele na kujifunza kutoka makosa ya wote—wa jana na wa leo.

Polepole, Gwajima, na Ndugai hawapaswi kuwa sauti ya haki katika taifa walilolinyamazisha kwa muda mrefu. Sauti za kweli ni zile ambazo hazikuwahi kunyamaza hata pale maumivu yalipokuwa makali. Na hizo ndizo sauti tunazopaswa kuzisikiliza sasa.

Wao wakitaka kusikilizwa, waanze kwanza kukiri ushiriki wao na kumkalia kimya Magufuli. Waombe msamaha kwa hilo, kisha ndio waungane na sisi katika mapambano. Kinyume na hivyo ni unafiki na mapambano hayataki unafiki.
 
Nashangaa kuona Leo chadema wanawashabikia akina Mpina, Gwajima, polepole, ndugai inamana wameshasahau.
Nadhani ndo maana chadema waliitwa manyumbu
 
Mtatoa kila aina ya milio mwaka huu kudadadeq
 
Nashindwa kuelewa una mlengo gani na shida ipo wapi?

Unawahoji hao uliowataja kwasababu kwasasa wanayekinzana nae yupo sahihi au hauyupo sahihi?

Wanayoyahoji ni hoja binafsi au za kitaifa na ni maswali ya wanainchi?

Wamuombe msamaha nani kwa makosa gani?
 
Plus kuwa Mzanzibar mengine yote ni visingizio.

Waulize kina Slow Slow kama tunachagua Rais Kwa kuangalia delivery,ni yupi kati ya waliopita anaweza msogepea Samia Kwa utekelezaji?
 
Sio issue ya jinsia wala dini yake. Shida ni utawala wake haupo kufuata katiba. Kiongozi aliyeapa kuitetea na kuilinda katiba ya nchi leo anatoka hadharani na kusema katiba is just a paper!! . Huyu si layman wa utawala na anajua nguvu na umuhimu wa katiba katika maendeleo ya nchi.
 
Plus kuwa Mzanzibar mengine yote ni visingizio.

Waulize kina Slow Slow kama tunachagua Rais Kwa kuangalia delivery,ni yupi kati ya waliopita anaweza msogepea Samia Kwa utekelezaji?
Hapa ndipo mnapoanza kukera nyie fans wa ⌚💯, utekeleza au utelekezaji?

Kwann mnakuwa waongo wa mchana kweupe,wewe umepita hii barabara ya uhuru, umepita barabara zote zilizofumuliwa,kuna hata moja iliyokamilika tokea kipindi cha magufuri?

Utekelezaji wa eneo gani?

Magufuri alikuwa mkorofi ila kiutendaji alikuwa makini na alikuwa ana deliver kwa wakati hicho ndicho kinamfanya magufuri kuwa "Bitter sweet leader" kwa watanzania. Miradi aliyoitekeleza inampa utofauti na hata viongozi waliomtangulia kiheshima.
 
Upinzani wa Ndani CCM, Kinachomponza Samia Ujanajike Wake

Katika siku za hivi karibuni, tumeona kuibuka kwa baadhi ya wanasiasa waliowahi kuwa ndani ya mfumo wa utawala wa awamu ya tano—wakijaribu kuvaa joho la uanaharakati na kuunyooshea kidole utawala wa sasa. Alianza Job Ndugai kwa kauli zenye miguno ya malalamiko. Akafuata Askofu Josephat Gwajima kwa maneno ya kejeli yenye ladha ya chuki ya kisiasa. Sasa ni Humphrey Polepole, akijaribu kuandika upya historia kana kwamba yeye hakuwa sehemu ya kinacholalamikiwa leo.

Lakini historia haijisahau.

Watu hawa si wapya katika siasa za Tanzania. Si wageni wa mfumo wanaoupinga sasa. Wamekuwa sehemu ya mfumo ambao leo wanaunyooshea kidole. Tofauti ni kwamba, wakati mfumo ulipowapa nafasi kubwakubwa, walinyamaza. Walitumia mamlaka yao kufunika maovu, kuhalalisha unyanyasaji, na kuwakemea wale waliothubutu kuhoji.

Serikali ya Magufuli: Hali Halisi Waliyonyamazia

Wakati wa utawala wa Hayati John Magufuli, Tanzania ilishuhudia ongezeko la matukio ya kukamatwa kwa wanaharakati, wanasiasa wa upinzani, na hata watu wa kawaida waliokuwa na maoni tofauti. Matukio ya kutekwa, kubambikiziwa kesi, kufungwa kiholela, na kuporwa kwa ushindi wa chaguzi yaligeuka kuwa kawaida.

Na bado, Ndugai akiwa Spika wa Bunge, Gwajima akiwa mbunge, na Polepole akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM—hawakusema chochote. Walikuwa mstari wa mbele kuhalalisha, kutetea na hata kushambulia wale waliokemea.

Leo wanarudi kama watetezi wa haki? Kama mashujaa waliochelewa? Hapana. Historia itawahukumu kwa ukimya wao wa wakati ule na unafiki wao wa sasa.

Tatizo ni Mfumo Dume, si Samia

Msingi wa malalamiko yao hauko katika uovu wa serikali, bali katika kuvunjika kwa ndoto ya mfumo dume wanaouhusudu. Hawa walikuwa na mgombea wao, walichokuwa wanasubiri Magufuli amalize hatamu yake. Magufuli alipofariki ghafla, walihamaki. Inasemekana, kulikuwepo na mpango wa kumfanya Samia Suluhu Hassan awe Rais wa mpito tu, kisha taifa liende kwenye uchaguzi mpya ili kurudisha mtu wao.

Hawakuwahi kumkubali Samia. Si kwa sababu ya sera, bali kwa sababu ya jinsia na asili ya uongozi wake. Alipovunja mnyororo wa utegemezi na kuanzisha mwelekeo wake—wakati mwingine kwa makosa yake—ndipo wakageuka na kuanza kupiga kelele kama vile walikuwa wapinzani wa kudumu.

Tuwe Makini: Historia si ya Kuandika Upya

Watanzania hawawezi kusahaulishwa yaliyotendeka. Sauti za sasa za malalamiko haziwezi kufuta ushiriki wa watu hawa katika misingi ile ile wanayoikemea leo. Siasa za Tanzania hazihitaji mashujaa wanafiki—wanaotokea tu pale wanapopoteza fursa au madaraka.

Tunapaswa kupima hoja zao si kwa ukubwa wa sauti, bali kwa ukweli wa historia zao. Je, walikuwa wapi wakati watu wakipotea? Wakati chaguzi zikiibwa na kunajisiwa? Wakati upinzani ukizimwa kwa nguvu za dola? Wakati mikutano ya hadhara imepigwa marufuku, Polepole si alikuwa Katibu Mwenezi wa CCM?

Wasitufanye wajinga. Ukimya wao wa jana ni ushahidi wa unafiki wao wa leo.

Hitimisho: Tusiingie Mtegoni

Mabadiliko ya kweli huanzia kwenye ukweli na uwazi wa dhamira. Tanzania haitajengwa kwa kurudi nyuma kwenye mitandao ya zamani ya kifisadi na kikatili, bali kwa kuangalia mbele na kujifunza kutoka makosa ya wote—wa jana na wa leo.

Polepole, Gwajima, na Ndugai hawapaswi kuwa sauti ya haki katika taifa walilolinyamazisha kwa muda mrefu. Sauti za kweli ni zile ambazo hazikuwahi kunyamaza hata pale maumivu yalipokuwa makali. Na hizo ndizo sauti tunazopaswa kuzisikiliza sasa.

Wao wakitaka kusikilizwa, waanze kwanza kukiri ushiriki wao na kumkalia kimya Magufuli. Waombe msamaha kwa hilo, kisha ndio waungane na sisi katika mapambano. Kinyume na hivyo ni unafiki na mapambano hayataki unafiki.
Ungekuwa na point kama Samia angekuwa hajafanya anayoshutumiwa kufanya.

Sasa kama mtu kaiba, watu wakasema kaiba, utamtetea vipi kwa kusema hugu anasakamwa kwa sababu ni mwanamke bila kujibu kashfa kwamba kaiba?

Two wrongs do not make a right. Two seemingly opposite things can both be right. Watu kukaa kimya kwa Magufuli haimaanishi ni lazima wakae kimya kwa Samia pia. After all, what is important is the truth, not who is saying the truth.

Why are you addressing negatively who is saying the truth instead of what is the truth?

That is ad hominem fallacy.
 
Upinzani wa Ndani CCM, Kinachomponza Samia Ujanajike Wake

Katika siku za hivi karibuni, tumeona kuibuka kwa baadhi ya wanasiasa waliowahi kuwa ndani ya mfumo wa utawala wa awamu ya tano—wakijaribu kuvaa joho la uanaharakati na kuunyooshea kidole utawala wa sasa. Alianza Job Ndugai kwa kauli zenye miguno ya malalamiko. Akafuata Askofu Josephat Gwajima kwa maneno ya kejeli yenye ladha ya chuki ya kisiasa. Sasa ni Humphrey Polepole, akijaribu kuandika upya historia kana kwamba yeye hakuwa sehemu ya kinacholalamikiwa leo.

Lakini historia haijisahau.

Watu hawa si wapya katika siasa za Tanzania. Si wageni wa mfumo wanaoupinga sasa. Wamekuwa sehemu ya mfumo ambao leo wanaunyooshea kidole. Tofauti ni kwamba, wakati mfumo ulipowapa nafasi kubwakubwa, walinyamaza. Walitumia mamlaka yao kufunika maovu, kuhalalisha unyanyasaji, na kuwakemea wale waliothubutu kuhoji.

Serikali ya Magufuli: Hali Halisi Waliyonyamazia

Wakati wa utawala wa Hayati John Magufuli, Tanzania ilishuhudia ongezeko la matukio ya kukamatwa kwa wanaharakati, wanasiasa wa upinzani, na hata watu wa kawaida waliokuwa na maoni tofauti. Matukio ya kutekwa, kubambikiziwa kesi, kufungwa kiholela, na kuporwa kwa ushindi wa chaguzi yaligeuka kuwa kawaida.

Na bado, Ndugai akiwa Spika wa Bunge, Gwajima akiwa mbunge, na Polepole akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM—hawakusema chochote. Walikuwa mstari wa mbele kuhalalisha, kutetea na hata kushambulia wale waliokemea.

Leo wanarudi kama watetezi wa haki? Kama mashujaa waliochelewa? Hapana. Historia itawahukumu kwa ukimya wao wa wakati ule na unafiki wao wa sasa.

Tatizo ni Mfumo Dume, si Samia

Msingi wa malalamiko yao hauko katika uovu wa serikali, bali katika kuvunjika kwa ndoto ya mfumo dume wanaouhusudu. Hawa walikuwa na mgombea wao, walichokuwa wanasubiri Magufuli amalize hatamu yake. Magufuli alipofariki ghafla, walihamaki. Inasemekana, kulikuwepo na mpango wa kumfanya Samia Suluhu Hassan awe Rais wa mpito tu, kisha taifa liende kwenye uchaguzi mpya ili kurudisha mtu wao.

Hawakuwahi kumkubali Samia. Si kwa sababu ya sera, bali kwa sababu ya jinsia na asili ya uongozi wake. Alipovunja mnyororo wa utegemezi na kuanzisha mwelekeo wake—wakati mwingine kwa makosa yake—ndipo wakageuka na kuanza kupiga kelele kama vile walikuwa wapinzani wa kudumu.

Tuwe Makini: Historia si ya Kuandika Upya

Watanzania hawawezi kusahaulishwa yaliyotendeka. Sauti za sasa za malalamiko haziwezi kufuta
Huyu Mama uwezo wake ni mdogo sana katika kuiongoza hii Nchi, hakubariki ndani wala nje ya Chama, Kuna Watu wachache ambao wananufaika na uwezo wake mdogo wa kuongoza ndiyo wanaaminisha Watu kuwa anafaa.

Leo hii yakifanyika mabadiliko ndani ya Tume ya Uchaguzi na kuwa huru, halafu Tundu Lissu agombee Urais, huyu Mana hawezi mshinda Tundu Lissu.

Ukweli ni kwamba huyu hakubariki kwa Wananchi wa hali ya chini ambao ndiyo wengi, wanaomkubali ni wale ambao wananufaika kupitia udhaifu wake wakiwemo Mafisadi.
 
Back
Top Bottom