GE2025 Upinzani ndani ya CCM: Kinachompoza Samia ni kuwa mwanamke?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Nashangaa kuona Leo chadema wanawashabikia akina Mpina, Gwajima, polepole, ndugai inamana wameshasahau.
Nadhani ndo maana chadema waliitwa manyumbu
Ulitaka Chadema wawashabikie nyinyi wahalifu mnaowateka na kuwaua makada wao, nyinyi wahalifu mnaotumia vibaya madaraka yenu kuwafunga viongozi wao magerezani kwa kesi za mchongo, nyinyi mnaowatumia majaji wa mchongo na msajili wenu wa vyama kuwafanyia Chadema zengwe la kutofanya shughuli zao za siasa kupitia kesi za kipuuzi!!

Aisee utakuwa una matatizo kichwani! Siyo bure. Haiwezekani mtu na akili yako timamu, uje na hoja dhaifu kama hii.
 
Sisi furaha yetu ni nyie mzidi kuparurana kazi yetu ni kukoleza moto ili muuane kabisa, wapuuzi wakubwa nyie.
 
Ulitaka Chadema wawashabikie nyinyi wahalifu mnaowateka na kuwaua makada wao, nyinyi wahalifu mnaotumia vibaya madaraka yenu kuwafunga viongozi wao magerezani kwa kesi za mchongo, nyinyi mnaowatumia majaji wa mchongo na msajili wenu wa vyama kuwafanyia Chadema zengwe la kutofanya shughuli zao za siasa kupitia kesi za kipuuzi!!

Aisee utakuwa una matatizo kichwani! Siyo bure. Haiwezekani mtu na akili yako timamu, uje na hoja dhaifu kama hii.
Haya ma essay Soma mwenyewe
 
Mtaandika sana lkn ukweli ni kwamba hasafishiki na hakubaliki, nje na ndani...
Umeandika kweli, lakini pia haya yanakolezwa na anakotoka pamoja na imani yake. Kuna wanaodai eti watu kama yeye wasiongoze JMT wakasahau kwamba, kama sio watu kama yeye hiyo JMT isingekuwepo leo hii.

Mitazamo yao ni kwamba watu hawa na kila kilicho chao, tuwadhibiti kwasababu eti ni hatari kwa usalama na ustawi wa mkono wa pili. Lakini sisi Waswahili huwa tunasema "ukipenda boga upende na mti wake". Mi niseme tu kwamba sisi tupo na tutabanana hapahapa. Vinginevyo tugawane mbao.
 
Mkuu uwezo wa huyu mama ni dhahiri machoni pa watu wengi kuwa uko chini ya kiwango! hayo ya imani na mengineyo ni kichaka tu cha kufichia incompetence yake ya wazi...laiti angeweza kudeliver ipasavyo nadhani hivyo vichaka visingetajwa!
 
Upinzani wa Ndani CCM, Kinachomponza Samia Ujanajike Wake

Katika siku za hivi karibuni, tumeona kuibuka kwa baadhi ya wanasiasa waliowahi kuwa ndani ya mfumo wa utawala wa awamu ya tano—wakijaribu kuvaa joho la uanaharakati na kuunyooshea kidole utawala wa sasa. Alianza Job Ndugai kwa kauli zenye miguno ya malalamiko. Akafuata Askofu Josephat Gwajima kwa maneno ya kejeli yenye ladha ya chuki ya kisiasa. Sasa ni Humphrey Polepole, akijaribu kuandika upya historia kana kwamba yeye hakuwa sehemu ya kinacholalamikiwa leo.

Lakini historia haijisahau.

Watu hawa si wapya katika siasa za Tanzania. Si wageni wa mfumo wanaoupinga sasa. Wamekuwa sehemu ya mfumo ambao leo wanaunyooshea kidole. Tofauti ni kwamba, wakati mfumo ulipowapa nafasi kubwakubwa, walinyamaza. Walitumia mamlaka yao kufunika maovu, kuhalalisha unyanyasaji, na kuwakemea wale waliothubutu kuhoji.

Serikali ya Magufuli: Hali Halisi Waliyonyamazia

Wakati wa utawala wa Hayati John Magufuli, Tanzania ilishuhudia ongezeko la matukio ya kukamatwa kwa wanaharakati, wanasiasa wa upinzani, na hata watu wa kawaida waliokuwa na maoni tofauti. Matukio ya kutekwa, kubambikiziwa kesi, kufungwa kiholela, na kuporwa kwa ushindi wa chaguzi yaligeuka kuwa kawaida.

Na bado, Ndugai akiwa Spika wa Bunge, Gwajima akiwa mbunge, na Polepole akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM—hawakusema chochote. Walikuwa mstari wa mbele kuhalalisha, kutetea na hata kushambulia wale waliokemea.

Leo wanarudi kama watetezi wa haki? Kama mashujaa waliochelewa? Hapana. Historia itawahukumu kwa ukimya wao wa wakati ule na unafiki wao wa sasa.

Tatizo ni Mfumo Dume, si Samia

Msingi wa malalamiko yao hauko katika uovu wa serikali, bali katika kuvunjika kwa ndoto ya mfumo dume wanaouhusudu. Hawa walikuwa na mgombea wao, walichokuwa wanasubiri Magufuli amalize hatamu yake. Magufuli alipofariki ghafla, walihamaki. Inasemekana, kulikuwepo na mpango wa kumfanya Samia Suluhu Hassan awe Rais wa mpito tu, kisha taifa liende kwenye uchaguzi mpya ili kurudisha mtu wao.

Hawakuwahi kumkubali Samia. Si kwa sababu ya sera, bali kwa sababu ya jinsia na asili ya uongozi wake. Alipovunja mnyororo wa utegemezi na kuanzisha mwelekeo wake—wakati mwingine kwa makosa yake—ndipo wakageuka na kuanza kupiga kelele kama vile walikuwa wapinzani wa kudumu.

Tuwe Makini: Historia si ya Kuandika Upya

Watanzania hawawezi kusahaulishwa yaliyotendeka. Sauti za sasa za malalamiko haziwezi kufuta ushiriki wa watu hawa katika misingi ile ile wanayoikemea leo. Siasa za Tanzania hazihitaji mashujaa wanafiki—wanaotokea tu pale wanapopoteza fursa au madaraka.

Tunapaswa kupima hoja zao si kwa ukubwa wa sauti, bali kwa ukweli wa historia zao. Je, walikuwa wapi wakati watu wakipotea? Wakati chaguzi zikiibwa na kunajisiwa? Wakati upinzani ukizimwa kwa nguvu za dola? Wakati mikutano ya hadhara imepigwa marufuku, Polepole si alikuwa Katibu Mwenezi wa CCM?

Wasitufanye wajinga. Ukimya wao wa jana ni ushahidi wa unafiki wao wa leo.

Hitimisho: Tusiingie Mtegoni

Mabadiliko ya kweli huanzia kwenye ukweli na uwazi wa dhamira. Tanzania haitajengwa kwa kurudi nyuma kwenye mitandao ya zamani ya kifisadi na kikatili, bali kwa kuangalia mbele na kujifunza kutoka makosa ya wote—wa jana na wa leo.

Polepole, Gwajima, na Ndugai hawapaswi kuwa sauti ya haki katika taifa walilolinyamazisha kwa muda mrefu. Sauti za kweli ni zile ambazo hazikuwahi kunyamaza hata pale maumivu yalipokuwa makali. Na hizo ndizo sauti tunazopaswa kuzisikiliza sasa.

Wao wakitaka kusikilizwa, waanze kwanza kukiri ushiriki wao na kumkalia kimya Magufuli. Waombe msamaha kwa hilo, kisha ndio waungane na sisi katika mapambano. Kinyume na hivyo ni unafiki na mapambano hayataki unafiki.
Ujanajike ni lugha ya wapi!!!???
Jifunzeni lugha vijana
Turudi kwenye mada: Shida ni UWEZO
 
Wameongoza Wazanzibar na Waislam wengi nchi hii hawakukutana na upinzani huu anaokutana nao [emoji355]️[emoji817]
Shida siyo Jinsia, Dini wala Asili
 
Hoja haina ukweli,ukweli japo mngeubaini kwa kukubali japo kuyaelewa kwa uchache malalamiko ya Slow slow,ya Watanzani na ya Wazalendo ya taifa hili mlishakataa kuyasikiliza na mkayapuuza,hida yote ipo hapa acha visingizio vya kitoto.!
 
Nikifikiri unajibu hoja zake kuwa mgombea wenu alipitishwa kinyume na maelekezo ya Katiba yenu! Kumbe we unekuja na mengine mapya!
 
Back
Top Bottom