GE2025 Upinzani ndani ya CCM: Kinachompoza Samia ni kuwa mwanamke?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wamekwambia wanamkosoa sababu ya ujike wake au utendaji mbaya na kuvunja utaratibu wa chama.
 
Plus kuwa Mzanzibar mengine yote ni visingizio.

Waulize kina Slow Slow kama tunachagua Rais Kwa kuangalia delivery,ni yupi kati ya waliopita anaweza msogepea Samia Kwa utekelezaji?
Uongo mkubwa
Wala SI jinsia,dini yake...
Dini inaeleweka viongozi wanapokezana SS inaingiaje hapa? Acheni kutafuta visingizio bwana,....ht mi Kwa mara ya kwanza jana nimejua vitu vingi polepole alivyofafanua kwenye katiba yenu hiyoo
Fuateni katiba acheni uhuni
 
Kuna Katiba ambayo SSH amevunja so far?
 
Tukiwaambia upinzani sio chama ni ideology inayotoka kwa mtu tu , mnakaza mafuvu🚮
Sasa polepole ni mpinzani au ni tapeli? Kipindi chake mikutano ya siasa ilikuwepo? Ruzuku mlikuwa mnapokea?
Ndo maana mnaitwa manyumbu
 
Uongo mtupu,

Uliona wapi kiongozi azuie na kubaka katiba ya chama chake Ili ajipitiahe bila ushinda I, bila mchujo,

Ameenda mbali kukutoa pia CDM Ili abaki pekeake!

Huyo hafai kuwa kiongozi, ni mwovu KUPITA wote.
 
Uinga tu wa kuwazankwa kutumia tundu
 
Sasa polepole ni mpinzani au ni tapeli? Kipindi chake mikutano ya siasa ilikuwepo? Ruzuku mlikuwa mnapokea?
Ndo maana mnaitwa manyumbu
Toeni madudu yenu yote 😅😅😅 asee
 
Unaleta story gani wewe! Watu tumekaa pembeni tukiwasubiri mraruane, na ikibidi muuane kabisa! Kwani hiyo ccm ina tija gani kwenye hii nchi, zaidi tu ya kutumiwa na wajanja wachache kujineemesha kiuchumi?
 
Kwa sababu yalishawahi kufanyika huko nyuma nasi twapasa kuvumilia tena sasa ndio Great Thinking yako?
Braying of a jackass.
 
Uanajike? Mama yangu na bibi zangu nao ni wanawake lakini hawamkubali raisi aliyeko madarakani na si kwasababu eti ni mwanamke.

Hivi inaingiaje akilinj raisi mzima kabisa anaamka anataja mbele ya Taifa na watu anaowaongoza kwamba "bosi" wake ni Kikwete? Yaani kidemokrasia na hata kikatiba anayepaswa kuwa bosi wa Samia ni nani, Kikwete ama wananchi? Sasa hili kosa maana yake haijuhi katiba vizuri, anaidharau katiba ama anawadharau wananchi?

Masuala kama bandari ya Bagamoyo kiusalama ilishasemwa mkataba wake si sawa bado unaruhusu mambo ya namna ile hivi kweli wewe unaweza kusema uko tayari kuilinda nchi na mipaka yake kwa mjibu wa katiba ama ndo yale yale mnajikuta ndo maana hata wahuni wanateka jeshi lote la polisi kwa kuhack akaunti yao .. hapo kuna nini tena?

Hivi haya maisha yalivyo mtaani leo magumu kama jiwe wakati huo rasilimali za Taifa zimewekwa nyara watu wanakwapua mnataka kuharalisha huu udhaifu wa kiuongozi kwa ajiri ya nani, ni nini maana ya mali za nchi na hawa wananchi wanakuja kuneemekaje na mali zao?

Kama nyie mnamwogopa kumwambia ukweli acheni wanaoweza na wauseme ukweli, si kwa jinsia yake lakini ni kwasababu ya kupungukiwa na uwezo wa kuilinda nchi na kutokujua ukubwa wa kitabu alichohapa kuilinda (katiba). Haelewi maana ya katiba ya nchi na ukuu wake kama raisi pengine anajua ana huo ukuu pale anapoona anaweza kuamlisha matumizi ya nguvu dhidi ya wananchi na si mengineyo... katiba si kuamlisha maumivu dhidi ya unaowatawala, katiba ipo kwa ajiri ya kulinda Taifa na mali zake kwanzia ndo mengine yanafata.

Akubali awaachie wenye uwezo na akumbuke hata yeye mwenyewe aliwahi kusema hana mpango wa kugombea 2025 sasa ni nini kasahau? Wananchi tumechoka naye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…